Babu wangu wa hiyari kaninunia

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Habari za asubuhi wapendwa wangu

Hapa napo tafutia vitu vya kuchafua meza yangu home basi miezi kama miwili iliyopita nilikutana na babu mmoja kwenye lift na dada wa uji ndiyo hapa babu tukaanza kujuana sababu nilimchokoza babu unakunywa uji nikacheka baada ya kicheko nikamwambia msalimie bibi naye akacheka.

Na kuniambia karibu uji kama utani, nikasema asante , babu akaamua kuninunulia uji nikaona aibu kukataa sababu yule muuza uji angeona nambania rizki me nilitakiwa kushuka kabla yao ila ikanilazimu kwenda hadi kwenye floor ya babu ili nipate uji uroho wangu wa uji tukanywa pale tukabadilishana mawili matatu basi nikaondoka.

Khee kama bahati mbaya tena nikawa kila siku kama wiki nakutana na babu anaiona kwa mbali mjukuu njoo uchukue uji nami naenda offer ya babu ya uji imeenda sasa ni mwezi mmoja na nusu hivi yeye hunisubiri na naenda kunywa uji kwenye floor yake kwa nje tunakula na story huku nikisubiria mda wangu wa kuanza kazi.

Jumamosi nikapima uzito nimeongeza kilo 2 khee nikaamua jumatatu sasa ni muda wa kukimbia uji wa babu kumbe babu naye kaamua kuniwekea bili ya mwezi kabisa ndiyo akawa ananipa taarifa jumatatu mmh nikamjibu babu nimeongeezeka uzito na nahisi ni huu uji wa asubuhi na jioni kama mzazi. embu nione nimeanza kuongezeka na ninaumbo baya akanijibu nitaacha baada ya kumaliza hii bili aliyoweka , nikasisitiza hapana hapa ndiyo nilipomkosea babu yangu.

Tokea jumaatatu jioni babu naona kaninunia hata nimsalimie haitikii, wala akiniona aniiti mjukuu kwa uchangamfu najisikia vibaya kumfanya babu anune lakini pia sipo tayari kunenepa sababu umbo langu nalijua nikijiachia tu nakuwa kama ufunguo sasa nawaza nifanyaje babu yangu awe na furaha tena , natamani kumwambia babu nitakuwa nakuja kukupigia story we huku ukinywa uji ila me sinywi ila sasa hata salamu hapokei.

Hawa walinzi wa jengo wameniuliza leo babu yako mbona akusubiri tena , nikawaza wanaweza hisi babu alikuwa ananitongoza nikakataa jamani kumbe ni uji tu

Siku njema
 
Teh Eti unakuwa kama ufunguo afadhali uwe kama funguo za tri-circle ila sio zile za vitasa vya Meco

au ukawa na umbo kama TANGAWIZI.
daby acha basi utani eti kama tangawizi ha hahhaha
 
habari za asubuhi wapendwa wangu...

hapa napo tafutia vitu vya kuchafua meza yangu home basi miezi kama miwili iliyopita nilikutana na babu mmoja kwenye lift na dada wa uji ...... ndiyo hapa babu tukaanza kujuana sababu nilimchokoza babu unakunywa uji nikacheka baada ya kicheko nikamwambia msalimie bibi naye akacheka.....na kuniambia karibu uji kama utani, nikasema asante , babu akaamua kuninunulia uji nikaona aibu kukataa sababu yule muuza uji angeona nambania rizki.. me nilitakiwa kushuka kabla yao ila ikanilazimu kwenda hadi kwenye floor ya babu ili nipate uji.... uroho wangu wa uji tukanywa pale tukabadilishana mawili matatu basi nikaondoka...

khee kama bahati mbaya tena nikawa kila siku kama wiki nakutana na babu anaiona kwa mbali mjukuu njoo uchukue uji nami naenda ... offer ya babu ya uji imeenda sasa ni mwezi mmoja na nusu hivi yeye hunisubiri na naenda kunywa uji kwenye floor yake kwa nje tunakula na story huku nikisubiria mda wangu wa kuanza kazi , jumamosi nikapima uzito nimeongeza kilo 2 khee nikaamua jumatatu sasa ni muda wa kukimbia uji wa babu ... kumbe babu naye kaamua kuniwekea bili ya mwezi kabisa ndiyo akawa ananipa taarifa jumatatu mmh nikamjibu babu nimeongeezeka uzito na nahisi ni huu uji wa asubuhi na jioni kama mzazi.....embu nione nimeanza kuongezeka na ninaumbo baya akanijibu nitaacha baada ya kumaliza hii bili aliyoweka , nikasisitiza hapana hapa ndiyo nilipomkosea babu yangu ...

tokea jumaatatu jioni babu naona kaninunia hata nimsalimie haitikii, wala akiniona aniiti mjukuu kwa uchangamfu najisikia vibaya kumfanya babu anune ... lakini pia sipo tayari kunenepa sababu umbo langu nalijua nikijiachia tu nakuwa kama ufunguo.. sasa nawaza nifanyaje babu yangu awe na furaha tena , natamani kumwambia babu nitakuwa nakuja kukupigia story we huku ukinywa uji ila me sinywi ila sasa hata salamu hapokei....

hawa walinzi wa jengo wameniuliza leo babu yako mbona akusubiri tena , nikawaza wanaweza hisi babu alikuwa ananitongoza nikakataa jamani kumbe ni uji tu

siku njema
We hali ilivyongumu saivi unywe uji wa watu bure tu!jiandae kwenda kuchezea rungu la kipepe
 
We hali ilivyongumu saivi unywe uji wa watu bure tu!jiandae kwenda kuchezea rungu la kipepe
ha hhahaa hapana babu kanikosa hata stori hapati.. itakuwa dada wa uji kamdanganya aniwekee bili labda nitampa lakini hajawi kuomba wala kuonyesha dalili za kuomba
 
habari za asubuhi wapendwa wangu...

hapa napo tafutia vitu vya kuchafua meza yangu home basi miezi kama miwili iliyopita nilikutana na babu mmoja kwenye lift na dada wa uji ...... ndiyo hapa babu tukaanza kujuana sababu nilimchokoza babu unakunywa uji nikacheka baada ya kicheko nikamwambia msalimie bibi naye akacheka.....na kuniambia karibu uji kama utani, nikasema asante , babu akaamua kuninunulia uji nikaona aibu kukataa sababu yule muuza uji angeona nambania rizki.. me nilitakiwa kushuka kabla yao ila ikanilazimu kwenda hadi kwenye floor ya babu ili nipate uji.... uroho wangu wa uji tukanywa pale tukabadilishana mawili matatu basi nikaondoka...

khee kama bahati mbaya tena nikawa kila siku kama wiki nakutana na babu anaiona kwa mbali mjukuu njoo uchukue uji nami naenda ... offer ya babu ya uji imeenda sasa ni mwezi mmoja na nusu hivi yeye hunisubiri na naenda kunywa uji kwenye floor yake kwa nje tunakula na story huku nikisubiria mda wangu wa kuanza kazi , jumamosi nikapima uzito nimeongeza kilo 2 khee nikaamua jumatatu sasa ni muda wa kukimbia uji wa babu ... kumbe babu naye kaamua kuniwekea bili ya mwezi kabisa ndiyo akawa ananipa taarifa jumatatu mmh nikamjibu babu nimeongeezeka uzito na nahisi ni huu uji wa asubuhi na jioni kama mzazi.....embu nione nimeanza kuongezeka na ninaumbo baya akanijibu nitaacha baada ya kumaliza hii bili aliyoweka , nikasisitiza hapana hapa ndiyo nilipomkosea babu yangu ...

tokea jumaatatu jioni babu naona kaninunia hata nimsalimie haitikii, wala akiniona aniiti mjukuu kwa uchangamfu najisikia vibaya kumfanya babu anune ... lakini pia sipo tayari kunenepa sababu umbo langu nalijua nikijiachia tu nakuwa kama ufunguo.. sasa nawaza nifanyaje babu yangu awe na furaha tena , natamani kumwambia babu nitakuwa nakuja kukupigia story we huku ukinywa uji ila me sinywi ila sasa hata salamu hapokei....

hawa walinzi wa jengo wameniuliza leo babu yako mbona akusubiri tena , nikawaza wanaweza hisi babu alikuwa ananitongoza nikakataa jamani kumbe ni uji tu

siku njema
Kumbe we ndo miss chagga
 
Hakunaga cha bure Dunia hii ya leo...babu kakujali kwa lishe ili akubomoe vizuri sasa wewe unaleta machejo.
Mpe mzee wa watu nae ajione mtu kwa hii Dunia.
 
Hesabu gharama mae ili kuona if ukinywa uji kwa kipindi kilichobaki itakuchukua muda gani kurudia hali ya kawaida... Cha kutosahau ni kwamba uji haucheleweshi matokeo chanya... Pia jitaidi sana kumrudishia babu furaha yake maana hawa watu wa umri wanajistukia kwa mengi usijechangia kupunguza siku zake za kuishi kikawaida.... Pia (nong'onezo) nahisi babu alikuwa anarusha mahindi kuelekea bandani sasa umemtoroka ktk mazingira tatanishi..huu ni utani my sister..... Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom