Babu wa Loliondo na ndoto ya Rais ajaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Loliondo na ndoto ya Rais ajaye

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kiherehere, Mar 28, 2011.

 1. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwa hatua ya awali ya kuoteshwa juu ya dawa ya kutibu magonjwa sugu imefanikiwa...

  Sasa kinachofuata ni hatua ya pili.... hii itausisha na ndoto ya babu ya rais ajeye, ambaye atatokea maeneo ya umasaini... nywele yeupe kama theruji... huvaa miwani ( kwa hatua hiyo yeye atakuwa anajifanya hamjui mtu mwenyewe ... ila atawaachia wapiga kura wenyewe wamjue na wengi wao watakaompigia muhusika ni wale ambao wameamini na kunywa chai ya babu )

  Nawasilisha

  Subirini
   
 2. M

  Mbunge Senior Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMA ingelikuwa hivyo,
  basi ningetarajia CCM
  kuwa imeliona hilo na
  ikafanyia kazi mawazo
  ambayo mwandishi mmoja
  nadhani wa Mwananchi
  ameeleza kwenye
  mtandao. Ninaamini haya
  yakifanyiwa kazi chama
  changu cha CCM kinaweza
  kupeta bila wasiwasi njoo
  mwaka 2015 kwani
  watakuwa wameweka
  ubinafsi nyuma na
  kutanguliza maslahi ya
  Watanzania kwa mara ya
  kwanza toka 1977!!! Soma
  makala haya kwa kirefu
  hapo chini:  LOLIONDO NI UWANJA WA VITA, MAJESHI YETU YAKO WAPI ?
  NINAMUUNGA mkono kabisa yule mwandishi wa Mwananchi aliyethubutu kusema kwamba ajabu ya nchi hii ni kuwa viongozi wetu ni wepesi kutuma majeshi au polisi au FFU kwenda kuzima maandamano ya wapinzani kuliko kutuma majeshi hayo kwenda kufanya jambo jema litakalopunguza matatizo ya wananchi au kuwaondolea shida au dhiki fulani.
  Kinachoshangaza ni kuwa kweli viongozi wetu wamekuwa wagumu au wameshindwa kutupatia tiba ya bure-sawa; nyumba au vifaa vya ujenzi vya bei nafuu-sawa; elimu au mikopo ya elimu ya gharama nafuu-sawa; lakini hivi kweli ndio hao hao wanashindwa kutupatia 'easy access' kwa babu baada ya kuwa wao weshaenda na kunywa kikombe chao na kila siku tunaona picha zao kwenye magazeti na TV wakinywa vikombe kabla yetu bila aibu. Huu ni ubinafsi wa kupindukia, na ni aibu viongozi wa nchi kuwa na ubinafsi wa namna hii!!!
  Ninaamini kwamba kama tuna serikali ambayo inashindwa kutekeleza mawazo ya mwandishi huyu, yaani, kuifanya Loliondo ikapitika kwa urahisi, vyakula, maji, vyoo na huduma zote muhimu zikapatikana bila shida basi ni vigumu kuona ni jinsi gani serikali inayoshindwa kuendeleza tena kwa faida yake na watu wake eneo dogo kama hili litaweza kuendeleza nchi yetu nzima ?
  Loliondo imetufungua wengi macho. Tumeuona ubinafsi wa viongozi wetu uchiuchi. Na hakuna siri tena. Nchi hii ina viongozi wabinafsi. Wanataka kila kitu wapate wao kwanza. Na kwa muktadha huu tusahau kabisa kwamba tuna aina ya viongozi ambao wanaweza wakawatoa watu toka kwenye umaskini wakati viongozi hao wametawaliwa na umimi na ubinafsi. Tuna viongozi wa siasa na wa dini, lakini ona fedheha na vichekesho hii leo ya viongozi hao. Huku baadhi redio zao zikimponda babu wao ndio wamekuwa wakwanza kwenda kupata kikombe.
  Niwaambie ahlili-kitabu kwamba mwenyezi Mungu hawezi kuwa mjinga hivyo kumpa fisadi, mwizi, mabarakala wa wanasiasa, mla mrushwa, mbinafsi karama zake. Na ndio maana kampa babu akijua fika kuwa sio mchafu kama hao wenye majoho ya sufi na vilemba vya hariri lakini ni wachafu kupindukia.

  Viongozi wa serikali nao walivyokwenda na kupata dawa ndio ikawa wamemaliza kazi yao. Wakati kiungwana na kistaarabu kwa miiko ya uongozi wao wangelistahili kuwa wa mwisho kabisa baada ya wagonjwa wa kikwelikweli kwenda kutibiwa kwa urahisi na bila matatizo yanayojitokeza sasa.
  Je, amiri jeshi wetu na majeshi yake wanatafsiri neno VITA kuimanisha nini? Na je, mahala panapohitaji akili, vifaa na mijiguvu ya kijeshi hivi unaweza kuwatuma wakuu wa mikoa ambao hata kama wana historia ya kuwa wanajeshi akili zao sasa hazifanyi kazi tena kijeshi na wamekuwa hana tofauti na raia wa kawaida?
  Vita sio tu pande mbili zenye silaha kupambana au kuuana. Vita ni hali yoyote ile ambayo inaweza ikasababisha ugumu, dhiki, maradhi, ulemavu na hata kifo kwa wananchi. Hali kama hii ikijitokeza kama tulivyoona kwa wenzetu Wajapani na majeshi yao huwa ni sawa na hali ya kivita.
  Wananchi wanaoingia Loliondo hivi leo ni sawa na wale wanaoingia Uwanja wa Taifa kutazama mpira wa miguu kwa mwaka mzima. Na mapato ambayo yanaweza kutokana na dawa ya babu kwa serikali na wananchi yanaweza kuwa mara 10 ya yale yanayopatikana toka uwanja huo wa taifa. Lakini serikali na viongozi wake kwa akili yao wameona ni bora kusaidia mabilioni mpira uendelee na hauendelei lakini serikali hiyo hiyo na viongozi wake wanaona uchungu kutoa bilioni chache ili barabara Loliondo ipitike na huduma bora na nzuri zipatikane wakati wote na kuliondolea taifa hili aibu ya kukutwa watu wake hukoNgorongoro wanakwenda kujisaidia vichakani na takataka zinatupwa ovyo kama viongozi hao hawakwenda kwenye mkutano wa mazingira huko Rio, Brazili na kwingineko duniani.
  Tatizo kubwa lililojitokeza katika njia ya Arusha-Samunge ni ubovu na uduni wa barabara. Tanroads, Majeshi yetu na Wizara ya Utalii na Wizara ya Afya zinaweza kwa pamoja kuhamasisha uwekezaji utakaochangia tu sio kwa barabara hiyo kujengwa na kufikia kiwango cha kupikitika misimu yote bali pia kila baada ya kilomita kadhaa kuwe na mahema au majegno 'pre-fabricated' ambayo mamlaka ya Utalii wa Afya na Tiba (itakayobeba jukumu la kusimamia na kuendesha mradi) litakodisha kwa wageni toka ndani na nje ya nchi pamoja na wafanyabiashara mbalimbali watakaoendesha huduma muhimu zinazohitajika wakati wote na wale waelekeao Loliondo.
  Gharama zozote zilizotolewa na kila mmoja wao zitalipika na faida juu kwa muda wote huduma hii ya dawa ya babu itakavyoendelea. Je, wizara husika na majeshi yetu zinataka nini zaidi ya hili ?
  Karibu mwezi sasa unayoyoma na kinachoonekana kwenye njia ya kwenda kwa Babu kule Samunge ni vifusi vya mchanga na changarawe lakini hakuna greda, matrekata, kreni wala chombo chochote kinachoweza kuwa na msaada kwa wananchi wanaoteseka huko.
  Basi au lori likikwamba 'wagonjwa' wakiwa mababu, mabibi, watoto na wananchi wengi wasio na nguvu hulazimika kufanya kazi hiyo ngumu.
  Viongozi wetu wameamua baada ya wao kwenda kunywa kikombe kwa babu kuwa kuna mambo yenye umuhimu zaidi kuliko kushughulika na mazingira, barabara na Usalama katika kwenda Samunge na kwamba ikiwezekana kama tunavyopenda miteremko ni kuwazuia wananchi kwenda kwa babu. Ninadhani huu utakuwa mkakati mbovu na kama wazungu wanavyosema unaweza uka'backfire' kwa viongozi na hasa ikigundulika bado baadhi ya viongozi wetu watakuwa wanaingia kwa babu kwa helikopta au njia nyingine ambazo ni nyepesi na rahisi zaidi.
  Kwa kutambua kuwa hali ya eneo hilo la Loliondo, mazingira yake na kaumu ya watu iliyokusanyika huko ni sawa na hali ya KIVITA ningelitegemea WAHESHIMIWA SANA VIONGOZI WETU wangeliamrisha mara moja majeshi yetu kuelekea huko na kwenda kupambana na adui mazingira kwa hali na mali hadi kieleweke.
  Kuna kile kinachoitwa ubia kati ya serikali, sekta ya umma na sekta binafsi hebu basi safari hii tuuone angalau ukifanya kazi kidogo kumkomboa mnyonge wa Tanzania anayemtegemea babu ambaye tiba yake ni shilingi mia tano tu na kinachogomba sasa ni usafiri. Na usafiri unakuwa ghali kwa sababu serikali imeshindwa kutumia rasilimali fedha na rasilimali watu iliyo nayo kufanya lile linalohitajika ili kushusha gharama hiyo na kuondoa shida na dhiki kwa wananchi wake.
  Hivi mawaziri, matajiri na wakubwa wengine mliokwishakunywa dawa hamkuona kwamba kukiwa na majiko yanayotumia gesi kule Samunge uchemshaji dawa ya babu itakuwa ni rahisi.
  Je, hamuwezi kumsaidia babu kupata masufuria na birika outomatiki lenye kuchukua lita 250-500 na likawa linaweka dawa kwenye vikombe outomatiki bila kumchosha babu?
  Itawagharimu kiasi gani kumrudishia asubuhi na mapema kabla hamjaondoka hapa duniani Mwenyezi Mungu na viumbe wake kile kilicho haki kwao na ambacho nyie hamwezi kamwe kuondoka nacho siku yenu ya mwisho?
  Mapendekezo ya Taratibu bora
  Wanaoingia Samunge kwa miguu hata kama wanatokea karibu watibiwe wao kwanza kisha wanaokuja na magari ndio wapewe kikombe. Hii ni haki ya hao wanaotembea kwa miguu kutokana na dhiki waliyoipata na ugumu wa maisha walionao na pia ni watu wanaoishi jirani na babu. Vinginevyo babu anaweza kuwahudumia hawa alfajiri hadi saa tatu na ndio ashughulike na wanaokuja kwa magari.
  JKT na majeshi yetu wajenge kambi kwa ajili ya wanaokwenda Samunge kupata tiba pale Karatu na vijiji jirani. Katika kambi hizo kila huduma ipatikane lakini wananchi wote walipe gharama hizo kwa JKT na wenzao.
  Katika kambi hizo kutakuwa na makambi ya rangi kijani wanaostahili kuondoka siku ifuatayo; rangi njano wanaostahili kuondoka baada ya siku mbili; rangi brauni wanaostahili kuondoka baada ya siku tatu; rangi buluu wanaostahili kuondoka baada ya siku nne; rangi nyekundu wanaostahili kuondoka baada ya siku tano; rangi nyeusi wanaostahili kuondoka baada ya siku sita na rangi nyeupe wanaostahili kuondoka baada ya wiki moja. Kama kila kambi itakuwa na watu 2,000 idadi ya watu kwenye kambi hizo wakati wote itakuwa ni 14,000.
  Ikiwa serikali itaweza kumpatia babu majiko ya gesi au umeme na birika outomatiki la kuweka dawa kwenye vikombe basi idadi ya waendao kupata kikombe inaweza kuzidi ile ya 2,000. Kwa vyovyote itakavyokuwa kwa wakati huu watu wanaoingia Samunge wasizidi idadi babu anayoweza kuwapa kikombe kwa siku wale wengine wote wakibakia kwenye makambi yaliyotajwa hapo juu.
  Wanaozidi idadi ile ya elfu kumi na nne waendelee kukaa Arusha ambako watajitegemea hadi watakaporuhusiwa kuelekea Loliondo kwa taratibu zitakazowekwa na utawala wa mkoa lakini utakaofuata usawa na haki kwa wote bila upendeleo kwa yeyote yule. Ingelifaa utaratibu wa kihasibu, FIRST -IN, FIRST-OUT (FIFO) ndio utumike kwa magari yote yanayoindia Arusha au kutoka Arusha kuelekea Loliondo.
  Hizi tabia za Kiswahili, kizaramo za kuyaangalia mambo na kuyalegezea macho na misuli na sasa akili hivi zitatufikisha wapi. Hali ya Loliondo jamani inahitaji wanaume watoke. Na wanaume wetu sana zaidi ya majeshi na FFU ni nani ? Badala ya Fanya Fujo UOne tunataka tuone Fikeni Fanyeni Usafiri Uwepo!~
  Hivi serikali yetu na viongozi wake wamekwishakaa na kutathmini wananchi wenye matatizo wanaoelekea Loliondo watawaona vipi ikiwa mambo haya yatafanyika:
  . Jeshi na zana zake kutumika kuhakikisha pamoja na kuwepo mvua barabara inapitika kwenda kwa babu wakati wote;
  . Vyoo vya 'kuassemble' kijeshi vinajengwa papo kwa hapo kwa mamia;
  . Mifereji ya maji inachimbwa pembeni ya barabara na huko Samunge ili hata kama mvua ikinywesha watu waendelee na kazi zao kama kawaida;
  . Jenereta babu kubwa zinapelekwa huko na umeme unazalishwa wa kutosha ili pasiwe na haja ya watu kuendelea kukata miti na kuligeuza eneo hilo jangwa kutokana na mahitaji yao ya nishati;
  . Babu anapatiwa majiko kadhaa ya umeme kumsaidia kuchemsha dawa wakati wote;
  . Babu anapatiwa mashine ndogo kama ile ya mitambo ya soda au maji inayosaidia kuweka dawa katika vikombe na yeye asiwe na kazi ya kuchota dawa hiyo kila siku iendayo kwa Mungu;
  . Taratibu zinafanyika za kuwa na matanki na maji mengi ya mvua kadri iwezekanavyo yanategwa na kujazwa kwenye mapipa hayo kwa matumizi ya leo na kesho;
  . Visima virefu vinachimbwa na mabomba kuwekwa ili kuhakikisha kwamba maji katika eneo hilo sio tatizo tena;
  . KIna mama lishe wanasaidiwa na mabenki na taasisi zingine za Kifedha kwenda kufungua biashara yao huko katika mazingira safi na yanayokubalika;
  . Viongozi na mashirika mbalimbali ya kidini yanachangia kwa hali na mali kuwe na misikiti, makanisa na maeneo ya kuswalia kwa sababu hapatakuwa na shida tena ya maji na huduma kama hizo;
  . Serikali na viongozi wake bila roho ya kwanini inahakikisha kuwa wakazi wa Loliondo kwa kila hali wanasaidiwa kunufaika na 'neema' hii iliyoletwa toka mbinguni ili waondokane milele na umaskini wa kupindukia.
  Nina hakika serikali namna hiyo itapendwa na kuheshimiwa na wananchi wake ndani na nje ya wilaya ya Ngorongoro kwa namna ambayo haijawahi kutokea katika historia yetu.

  Kama nilivyokwishasema hali ya Loliondo, Samunge ni hali ya kivita na siyo ya kawaida. Ni hali ya kufa au kupona. Panahitajika mtazamo na msukumo tofauti kuliko uliopo hivi sasa.
  Viongozi wetu walipojitokeza kwenda kunywa kikombe walifanya hivyo chapu chapu na barabara na njia zikasafishwa kama sio anga kuachwa jeupe ili wafike salama na wapate kile walichokitaka. Hii ingawa kidogo ni tofauti na baba wa Taifa alivyokuwa, kwa maana ninaamini yeye angelisubiri watu wote waende kwanza kupata kikombe na yeye akawa wa mwisho kabisa. Yaani, kwa maneno mengine kwenye mapambano yeye alikuwa mtu wa kwanza mbele, na kwenye tiba au kupata heshima alijiweka wa mwisho kabisa. Haya yametufunza tu ile tabia ya kukosa ubinafsi nchini imezikwa na sasa ni ubinafsi wa viongozi wote tena kwa sana.
  Kwa kuwa hali hii ni ya kivita, pengine kwa akili yangu ndogo ninaamini ni wanajeshi wanaostahili kutumika kuleta unafuu kwa wananchi. Tukumbuke vita sio tu hali ya majeshi mawili kupambana bali pia ni jeshi kupambana na mazingira magumu na ya hatari kwa kuwa wanajeshi wameandaliwa vizuri zaidi kupambana na hali hiyo kuliko raia. Hii ilikuwa ni changamoto kwao kuona kama wakipewa fursa hiyo wanaweza kuigeuza hali inayotishia maisha ya watu ikawa ni hali ya kuwavutia na kuwakurubisha wengi zaidi na zaidi, na hata nje ya mipaka yetu.
  Kila mtu iwe masikini au tajiri, askari au raia, mwanamke au mwanamme, muislamu mkiristo, fisadi au watu safi, CCM au upinzani wote tunahitaji huduma hii na tusije wasikiliza vichaa wachache wanaojiona wao ni watakatifu mno na wanaweza eti kumchagulia Mungu yule wa kumpa na yule wa kutompa. Kama Nabii Issa alivyesema nawaambia basi kati yao mmoja wao arushe jiwe la kwanza kama yeye naye hana dhambi wala ugonjwa na anachungulia pia kaburi !
  Hatuhitaji maisha plus kwa raia. Lakini wanajeshi wanaweza wakaidhibiti hali hiyo na wakageuza eneo hilo si tu kuwa zuri na salama kwa wananchi bali pia kazi yao ikawapatia kipato cha uhakika wanajeshi kwa miezi mingi ijayo. Maana wao ndio watakaostahili kulipisha kila gari inayoingia Samunge tozo (na kuwakatia wilaya kiasi fulani); watajenga prefabricated houses za kuwakodishia wageni; watatengeneza vyoo na bafu safi za kulipia; watauza vyakula na maji; watalinda mali za raia; na kama hali ikiruhusu wanaweza pia kukodisha ndege na helikopta za jeshi kuwapeleka wale wenye dhiki na shida zaidi ambao hawawezi kuhimili usafiri wa barabara.
  Kwa kuwa wanajeshi wetu wanampenda, wanamheshimu na wanamtii amiri jeshi wao ninaamini kinachosubiriwa ni amri yake tu kwamba kitu fulani kifanyike na kitu hicho kikafanyika siku ya kwanza, ya pili, ya tatu na kuendelea hadi hali ya kugeuza eneo la Loliondo kuwa kivutio cha Utalii wa tiba ikakamilika.
  Nimalizie tu kwa maneno ya hekima ya Baba wa Taifa Amiri Jeshi wa Kwanza wa Majeshi huru ya Serikali ya Muungano wa Tanzania: ' LINALOWEZEKANA LEO, LISINGOJE KESHO !'
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Lowasa ni mkiristo mwezetu anafaa. maana siku hizi sifa ya kwanza ni dini yako.
   
 4. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Ukristo na wizi wapi na wapi kaka. Yule ni mwizi tu
   
 5. Mental Retard

  Mental Retard Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  :
  Hapana si kweli... Lowasa si mwizi hata kidogo! kujiuzulu kwake ilikuwa ni ajali ya kisiasa tu. Ameonewa sana, ametukanwa sana na kudharauliwa sana tu... :angry:

  Kama alivyosema muungwana - siku si nyingi historia itamtendea haki anayostahili :drum:
   
 6. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  yes Lowasa si mwizi hata kidogo na pili ni zamu ya mkristo mwenzetu baada ya zamu ya muislamu kupita........
  Lowasa for presidential 2015............go Lowasa go
   
 7. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  kwa ushahidi upi uliokuwa nao kwamba Lowasa ni mwizi?
  mahakama ipi iliyothibitisaha ya kuwa Lowasa ni mwizi?
  kujiuzulu si tija kwani wangapi waliojiuzulu hapa tanzania?
  Mungu ibariki Tanzania......Mungu mbariki Lowasa
   
 8. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hata kikwete ni mwizi alisame wezi wa epa na kwa dini yake na yangu na KIKWETE mwizi sisi tutajuaje
  kama hakupata mgao, kidini mwizi na anayemwacha aibe wote wezi
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hali inazidi kuwa mbaya.
   
 10. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Ilo umeliona leooo!!!??
   
 11. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Akili yako mbofu mbofu. We si mmoja wao Mkristo hawezi kuwa na akili mbofu kama zako.
   
Loading...