Babu wa Loliondo ashitakiwe ICC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Loliondo ashitakiwe ICC

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ismase, Apr 11, 2011.

 1. ismase

  ismase Senior Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi wana Jamii Forum kwani babu wa Loliondo asishitakiwe katka mahakama ya kimataifa? wengi watanishangaa kwa maoni yangu lakini naamini na ninachokisema na nitakisimamia. Babu wa loliondo anasababisha mauaji ya halaiki ya watanzania na hata wajinga wa nchi jirani. hii ni kutokana na uzushi wake wa kusema anatibu magonjwa sugu ikiwemo ukimwi, magonjwa ya moyo, kisukari kansa na pumu.

  kutokana na uzushi huu maarufu sasa kama kikombe cha babu, watu wengi wamepoteza maisha na baadhi ya miili kutelekezwa porini. kwa mjibu wa vyombo vya habari hadi wiki jana watu takribani 78 walishapoteza maisha yao. hatuwezi kuwalaumu wagonjwa moja kwa moja kwani wao wanahangaika hata wakiambiwa kuleni nyama ya mtu ili mpone watafanya hivyo. Ila lawama ni lazima ziwe juu ya babu, serikali yake na maaskofu wenzake wanao-support uongo huu mtakatifu.

  ukiachilia mbali wanaotangazwa kufa kufuatilia kukumbilia kwa babu, bado wengi mitaani wanapoteza maisha kwa kuacha kunywa dawa za kurefusha maisha wakiamni babu kawaponya. madaktari wanadhibitisha hakuna hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepona baada ya kunywa kikombe.

  Natoa wito kwa jumuiya za kimataifa, ili kunusuru maelfu ya raia wasio na hatia kuendelea kupoteza maisha yao, waingilie kati na kumkamata babu mara moja ili wamepeke the hague kujibu tuhuma za mauaji ya halaiki. kama wakenya wametumbukizwa huko, babu ana kinga gani ya kisheria?
   
 2. Pilimi

  Pilimi Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Lakini watu walikufa wengi mwanzo kutokana na utaratibu wa kwenda kule haukuwa planned vizuri kama sasa.Vile vile hata ma hospitalini watu huwa wanakufa,je na hao madaktari washitakiwe ICC?
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hizi ni tuhuma porojo!
  Babu kamwita nani?
  Huko mahospitallini watu wanakufa wangapi kwa cku?
  Kwa mfano muhimbili kila cku watu wanakufa wengi tu bac vile hospital huwezi kuuliza.
  Hao mahututi wameshindikana kwa hospital wanaanza safari ya mbali na ya taabu kwenda kwa babu lazma wapatwe na madhara zaidi.
  Babu alishasema watu mahututi wasiende kwake , but watu hawasikii.
  Na kwaidadi ya watu waliokufa kama ni hiyo na ukiangalia idadi ya number iliyoenda kwa babu, babu anajitahidi sana..!
   
 4. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi wameshurutishwa kwenda kwa babu? mimi sioni sababu ya kumlaumu babu ni kama vile mwanaume unakwenda kwa malaya halafu unawalaumu malaya kwa uwepo wao!
   
 5. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 9,994
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Hivi mtu akifia njiani wakati anapelekwa hospitali ya Muhimbili, daktari atashtakiwa?
   
 6. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Kama ni kushitakiwa nadhani hata wahuburi wa baadhi ya makanisa yanayojiita ya kiroho nao washitakiwe. Ukiangalia na kusikiliza mahubiri yao utasikia akiwaambia waumini wao " njooni hapa kuna nguvu ya MUNGU ya uponyaji wa magonjwa yote sugu (kama yale anayotibu babu wa loliondo) na watu wanaenda na hawaponi na wanakufa.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,381
  Likes Received: 28,156
  Trophy Points: 280
  Logic zingine bana....
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,494
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 280
  Kwani kamshika nani mkona na kumlazimisha kwenda? Hajawahi kujitangaza badala yale walotibiwa naye ndo wanaomtangaza. Mwisho mahakama za Tanganyika hazijashindwa kufanya kazi yake hata wampeleke ICC. Ushauri: file kesi na mashtaka ulonayo kisha peleka mahakamani!
   
 9. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Subiri tu!atapelekwa iwapo waziri au mtoto wa kigogo atakapokufa.mtanzania wa kawaida hana thamani!
   
 10. w

  warea JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio maana watu wanajinyonga, serikali haifuatilii! Watu wanauwana, watu wanasema wanajipeleka wenyewe?
  Kumbe siku hizi mtu akitaka kuijinyonga si kosa la jinai, maana anajinyonga mwenyewe!
   
 11. m

  mams JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 615
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Chukueni ripoti ya wanaokufa wakiwa njiani kwenda mahospitalini na wanaokufa wakiwa hospitalini na pia ongezeni na wanaokufa baada ya kutumia dawa hizo. Baada ya hapo mlinganishe na hiyo ya kwa babu ndio muamue jinsi ya kujadili!
   
 12. w

  warea JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anawalazimisha watu waende Loliondo kisaikologia!
  Subiri uumwe upime uwezo wako wa kuamua!
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,709
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Kukaa na chuki dhidi ya jambo au mtu fulani, kunaweza kukuharibia hata uwezo wa kufikiria.
  Yaani mtu anakuja na post ya kumpeleka Babu ICC? Simple reasoning tu (nje ya chuki) itakupa ukweli kuwa hilo jambo haliwezekani...

  Ni rahisi hata kuishtaki hospitali ya serikali kwa kushindwa kumtibu mgonjwa kwa vile wajibu wa hospitali ni wa kisheria, lakini huwezi kumshitaki babu wakati hajakuita. Na hata ukienda usipone, ana jinsi ya kujitetea, kuwa hukuwa na imani....

  Chuki zingine hizi, mngezipeleka kwenye kuchukia ufisadi na umasikini, tungefika mbali sana.
   
 14. w

  warea JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye red ni hatari!
  mtu akijinyonga ni kosa ua si kosa? watu wanaoacha madaktari na kwenda kwa babu ni sawa na kujinyonga. Wanapaswa kulindwa au kushitakiwa kwa kutaka kujiua.
   
 15. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kaka, ICC wanapelekwa watu wanaoshtakiwa kwa kesi za war crime, crime against humanity, genocide etc. Lazima idadi ya watu iwe kubwa, method ya mauwaji iwe ya kukusudia na mara nyingi kuwe na target maalum kama dini, kabia, jinsia etc.
  Kwa kesi ya Babu hivyo vitu havipo na hawezi pelekwa ICC.
  Ila nadhani serikali ya TZ inatakiwa kuchukulia hatua. Kama watu wanakufa hospitali, ao njiani wakienda hospitali, angalao idadi ya wanao pona inaonekana kua juu.
  Kwa kesi ya Babu Kwanza ni kama hakuna daktari alie jitokeza kuhakikisha kua asilimia kubwa ya wagonjwa walipona, na wachache tu ndio waripotiwe katika vifo.
  Pili, ingawa Babu mwenyewe anasema wagonjwa wasiache dawa za hosii, anasema anaponya. kusema tu hivo ni sawa na kuwaambia watu waache dawa, na hiyo inawapelekea kufa.
  Tatu, kweli serikali imejaribu kuweka order pale, ila mazingira bado hayaswihi kwa kuwahudumia wagonjwa.
  Kwa sababu zote hizo mimi ningeshahuri Babu apigwe suspension, dawa yake ifanyiwe uchunguzi kujua kama inadhuru ao inaponya, statistics za wagonjwa ziwe recorded, huku ujenzi wa mazingira bora ukiendelea. Ikiwa uchunguzi huo utaleta result nzuri basi Babu apewe leseni kama traditional practitioner na alipe kodi kama kawaida.
   
 16. L

  Loloo JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe mia kwa mia ismase ila kukusahiisha kidogo sio icc ni mahakama yetu hapahapa hajamshika mtu mkono ila anawashawishi na hilo ni kosa yeye na wale viongozi wote wanaompromote asingitoa mabango kila siku kwenye vyombo vya habari kutusahaulisha dowans na ukali wa maisha watu wasingejazana huko kwanza nani amepona ukimwi?a mere traditional healer pretend to be the hand of God using charm and magic{mauzauza)
   
 17. E

  Emma505 Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani ndugu zangu sikieni. Siku zote muhitaji ndio anayemfuata babu kule, watu hawaendi kule kama vipofu wamepata ushuhuda kwa watu wengine. Halafu kila mtu anapewa kama jinsi anavyohitaji kwa imani yake katika kupona ugonjwa wake. Hata ktk maandiko matakatifu yameandikwa "KWA IMANI UTAPONA" (Hii ni sehemu tu ya neno).
   
 18. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,547
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Sahau mpango huo wa kushitaki ndugu yangu. Hiari yashinda utumwa hata itumiwapo kwa kujidhuru.
  Wewe jitahidi kuwashawishi watakaokusikiliza kwamba hakuna tija kwenda kwa babu. Usianze na mimi - nilikwishashawishika tayari.
   
 19. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Babu akienda icc nashauri aekwe jirani na charlse taylor ictoshe juzi clouds wametoa ushuhuda hakuna aliyepona na babu kawaita watu km amesema anaponya ina maana kawaita wa2 na kapanga bei
   
 20. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,664
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Miafrika Ndivyo Tulivyo
   
Loading...