Babu wa loliondo amaliza watu Visiga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa loliondo amaliza watu Visiga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Jul 15, 2011.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Jamani mniwie radhi.Hili siwezi kulinyamazia.Babu wa Loliondo 'ameshaua' watu wanne waliotoka kwake kupata kikombe katika Mtaa wa Visiga Kati,Kibaha Pwani.Watu hao ambao wote walikwenda kwa Babu wakiwa na afya ya kawaida,wamefariki kwa kufuatana.Majina ya Marehemu wote ninayo.Arobaini ya mmoja wao ni leo.Naiomba Serikali itamke tena kuhusu tiba hii ya Babu kuwa au kutokuwa na uwezo wa kuponya magonjwa yanayopigiwa upatu kuponywa:UKIMWI,Kisukari na Kansa.Wapo wengine wawili hapohapo ni taabani.Muda ukipita hivi,Serikali itawajibika.Kweli tena...
   
 2. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  duh! pole kwa wafiwa.
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wapo wengine wengi wamekunywa wapo fit majina tunayo mfano Mrema wa TLP.
  Pole kwa wafiwa na mungu awapumzishe kwa amani waliotangulia.
  Sote tusafari moja!
   
 4. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  tueleze pia jumla wameenda watu wangapi kutoka hapo visga?
  Wanagapi kati yao wamekufa baada ya kupata kikombe na wamekufa muda gani baada ya kupata kikombe?
  Wangapi hawajafa na hali zao zikoje kiafya?
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Tiba ya babu si ya kuzuwia kufa...ni tiba ya magonjwa!
  Mtu wa kufa atakufa tu...tusikanganye watu kwa maneno yenye hisia zaidi kuliko utafiti!
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ninaachoona hapa ni fitina tu kwani kumuita babau wa loliondo ndiye kawaua hao watu si kweli. Inawezekana hata wasingekwenda kwa babu wangekufa na si kwamba kwa babu walikunywa sumu ndio maana wamekufa. Kijijini kwangu watu wote waliokwenda wamepona na kama unavyojua ukienda kwa babu na imani mbili huponi kwani lazima uende ukiamini kwamba ukinywa kile kikombe mambo yako yatakuwa safi. We fikiria unampeleka mtu yuko mahututi na aelewi yuko wapi ni vigumu kupona kwa sababu mtu huyo hana fahamu za ku-exercise faith. Hafikiri wengi waliokufa ni watu ambao ufahamu wao ku-exercise faith ulikuwa umepotea au mtu aliekwenda tayari amekata tamaa na pale akaenda kama formality basi huyo ni vigumu kupona. Hivyo ndivyo ninavyo amini na correct me if I'm wrong.
   
 7. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Waliokwenda kwa ujumla ni watu nane kwa safari ya kwanza.Wakakaa karibu miezi mitatu ndipo walipoanza kufa mmoja baada ya mwingine.Waliosalia kwa safari ya kwanza ni wanne,nao ni wagonjwa sana.Wako wengine walikwenda kwa safari ya pili.Sasa wamejaa mashaka mno.Ni kweli kufa hakuzuiwi na Tiba ya Babu.Lakini,ndio wafe waliokwenda huko tu?! Hivi Mrema ndio yuko fit kweli? Ndio kipimo cha wote kweli? Hilisi jambo la mzaha hata kidogo....it is a serious issue than you can cheaply imagine.
   
 8. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Si Mrema tu wapo wengine hapa ofisini kwetu kuna watu zaidi ya kumi wamenda na wapo fit.
  Sio mzaa nimetoa mfano wa MREMA kwa sababu alikuwa haishi kulazwa KCMC sasa hivi anadunda kutwa yupo bungeni
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  wengine wajanja kaka hawaachi dawa zao walizoandikiwa na dkr
   
 10. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani wapone watanzania wote!wengine hao wlikuwa wakufa tu!Dawa ya Malaria SP ilivyoingia watu walikufa wengi kuliko hao uliowasema,na bado inatumika mpaka leo!wenye alergy za ajabu ajabu walitakiwa kujiepusha!sie watafit tunasema mtaukio uliyoripoti ARE NOT STATISTICALLY SIGNIFICANT (p
   
 11. E

  ESAM JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kwa babu wajinga ndiyo waliwao hakuna cha kupona kwani wamejazwa maroho machafu na ndiyo yanayowaua, hao unaosema wako fit inawezekana unaona wako fit kimwili lakini kiroho ni marehemu. Kwani maisha ni hapa duniani tu? Ni vizuri kupona mwili lakini mtu apone katika msingi ya kisayansi au kuombewa kwa jina la Yesu ili abaki katika mpango wa Mungu ili akifa aende mbinguni. Lakini kwa watu wa ndoto na maono hao ni fungu moja na wachawi,na waganga na Mungu wao ni shetani ambaye kwake ahkuna msamiati wa uponyaji
   
 12. E

  ESAM JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kama ndiyo hivyo kwa babu walikwenda kufanya nini si wangeendelea na dawa zao tu. Kuendelea kupigia debe ndoto za babu wa Loliondo ni kujidhalilisha na kuwadhalilisha watanzania kwamba sisi ni watu wa njozi na by the way a great thinker really thinks greatly and can never be swayed by unsubstantiated illusions
   
 13. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Hivi?
  Kama ile dawa ya yule mzee inauwa, Leo si tungekua tuna janga la kitaifa?

  Ukiniuliza kama ile dawa inaponya nitakwambia sijui! Lakini ukiniuliza kama inaua nitakwambia hapana, Kwasababu watu wato ninaowajua wamekunywa bado wako hai, ila kupona sijui kwasababu mimi sio daktari.
   
 14. A

  Anold JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kuhusu Dawa ya Babu kama inatibu au haitibu sina maelezo, ila ieleweke kuwa Babu ameshasema hana uwezo wa kuzuia ''KIFO'' hili ni lamsingi sana kujulikana kwa wale wote wanaokwenda kwa Babu. Maana kuna watu wapo mahututi au magojwa yao yamefikia hatua mbaya lakini wanaona BABU ndiye anayeweza kuwafanya waepuke kifo. Mimi binafsi nina ndugu wakaribu ambao walikwenda wakisumbuliwa na Kisukari lakini baada ya kurudi hali zao ziliimalika japo pia kuna waliokwenda waliporudi hawakukaa sana wakaaga dunia, sasa kinachotakiwa kueleweka kwa jamii hii ni kuwa, Dawa ya Babu haina nguvu ya kimiujiza ni dawa kama dawa za HOSPITALINI ambazo hata zenyewe pamoja na utafiti na uhakika wa kuponyesha magonjwa lakini hazijawahi kuzuia kifo zaidi ya kusogeza muda wa kufa. Hivyo watu wajue kufa kwa mwanadamu ni lazima.
   
 15. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Mbona tunashindwa kuwa Great Thinkers,kwani nani alisema kikombe cha babu kinazuia kifo ?! kwa bahati mbaya sana binafsi kuna watu ambao sijui wangeona hii post yako wangekutendaje,kwani wakikumbusha maisha kabla ya kikombe yalivyokuwa yamejaa mateso na maisha baada ya kikombe,hakika watakulaani,binafsi mama mkwe wangu ambaye sukari na moyo kupanuka ilimfanya awe na maisha ya kitandani karibu kila siku atakushangaa na kukusikitia sana,ni bahati mbaya sana wote waliotumia kikombe hawana uwezo wa kuandika shuhuda zao JF,lakini shuhuda nyingi zingetolewa hapa,waliopona ni wengi sana ukilinganisha na hao waliokufa ambao wangekufa anyway kwani hata waliopona sasa bado watakufa.Let us think Great...
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Na 2tambuwe kwamba ukienda kwa Babu ukiwa na mambo yako ya kichawi,kinafiki hakika itakula kwako tu. Inatakiwa uende na uwe umejitakasa. Wengi wameenda na wakapigwa STOP wasiguse KIKOMBE na wakang'ang'ania na hatima yao ni kutangulia kaburi. Kwa mfano hapa kwe2 Arusha Mjini kuna mama mmoja alienda na kupigwa STOP akiambiwa akajirekebishe ndiyo aje lakini akazunguka upande wa pili na akapata kikombe akaambiwa okey umeng'ang'ania kunywa haya nenda zako. Baada ya wiki 3 kwenda ya 4 kapatwa na ugonjwa wa ghafla na ikampiga chini na baada ya mazishi niliohudhuria mimi na washikaji hakika mama huyo kazikwa na baada ya muda kama saa kumi na moja jioni kwa sabbu yule mama ni mkristo na aliwekewa msalaba ikiwa ishara ya ukombozi, hakika msalaba ikaanza kuungua moto mpaka ikaisha yote wa2 walijitahidi kuuzima bila ya mafanikio. Kwa hiyo mambo ya kule Samunge ni ya IMANI tu. NAWAKILISHA!
   
 17. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kama ni mchawi ukienda kwa babu kupiga ki-cup huponi ndugu lazima ufe!!!
   
 18. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nina Mdogo wangu aliyekuwa na kifafa ambacho alikuwa kwa wiki si chini ya mara moja lazima aanguke. Lakini tangu arudi toka kwa Babu March mwaka huu mpaka leo hajawahi kuanguka na anaendelea kukata Kili yake bariiiiiiiiiiid billa wasiwasi wowote na leo tunakwenda kula nae Mbusi saaafi pale Marangu bar Kimara.
   
 19. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao zao siku zilifika
   
 20. n

  neyro JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 232
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  ni lazima wajae mashaka inawezekana wote walipanga njama "kumjaribu babu" so imekula kwao .ofkoz washauri wapigwe sala ya toba wlobaki hai ili wafe kifo kitakatifu. kuhusu wenye nguvu za giza kujitaksa kwanza ni very true kwani yupo mama mmoja after kunywa on da way home kichaa hadi leo NI KWELI NA AMINA
   
Loading...