Babu wa Loliondo sasa yuko hatarini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Loliondo sasa yuko hatarini...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mediaman, Mar 24, 2011.

 1. mediaman

  mediaman Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zilizoandikwa katika magazeti na kusikika katika redio na Televisheni siku kadhaa zilizopita zilieleza kwamba Babu wa Loliondo ameoteshwa na Mungu dawa ya kuwatibu watu magonjwa sugu.

  Wachunguzi na wataalam wa masuala ya kiroho wamegundua kuwa ndoto hiyo ni ya uongo kulingana na Neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia 23:25-32. Neno la Mungu (Biblia) katika mistari hiyo linasema hivi:
  "Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto. Je, mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao...Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA...Basi kwa sababu hiyo...mimi [NIKO KINYUME]na manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema. Tazama, mimi [NIKO KINYUME] na hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA."

  Katika mistari hiyo, BWANA Mungu anazifananisha ndoto na makapi. Hazina maana. Neno lake(ngano) ndilo lenye maana. Maandiko hayo yanaonyesha wazi kuwa Mungu hajamtuma babu kusema wala kufanya hayo anayoyafanya sasa na kwa sababu hiyo yuko matatani au hatarini maana Mungu yuko kinyume naye sasa.

  Vyanzo vingine vya habari kutoka nje ya nchi, vimethibitisha kuwa huyo babu wa Loliondo ni nabii wa uongo. Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa ukitaka kumtambua nabii wa uongo angalia mambo yafuatayo:

  1. Mkazo wake hauko kwa Yesu, bali ni juu ya miujiza kama ambavyo babu asivyolitaja Jina la Yesu. Mkazo wa babu uko kwenye kikombe na huo mti. Watu wengi wanapoona miujiza (kama huo mti wenye sumu kutoweza kuua kama walivyozoea) wanakuwa wepesi kuamini kuwa Mungu ndiye anayefanya miujiza hiyo. Wanasahau kwamba hata waganga na wachawi wa Misri walitenda miujiza kama ile aliyotenda Mungu. Shetani anafanya miujiza na ataendelea kufanya hata zaidi ya huo wa kikombe. Soma 2 Wathesalonike 2:8-12.

  2. Nabii wa uongo hufanya vitu ambavyo haviwezi kuthibitishwa na Neno la Mungu. Badala yake hutaja tu kwamba anafanya hivyo kwakuwa ameota ndoto au amefunuliwa. Katika Biblia tunaona kuwa Yesu alikuwa akiyathibitisha yale aliyokuwa akisema kwa kutaja neno "Imeandikwa". Babu hana ujasiri wa kusema "Imeandikwa, mtapona kwa mti wa mgariga" Hawezi, maana andiko hilo halipo.

  3. Nabii wa uongo husema mambo yasiyotimia. "Atakaponena nabii kwa Jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope." Kum 18:22. Babu alisema wazi wazi kwamba dawa yake inaponya kabisa lakini baadhi ya wale waliokwenda kwake tayari wameishapoteza maisha yao baada ya kunywa dawa hiyo. Na wengine wanakiri kwamba hawajapona kabisa ila wanasikia nafuu tu!

  4. Nabii wa uongo hawezi kuwahubiri watu kwa mkazo waache dhambi zao. "Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri. Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao(Yeremia 23:21-22). Babu wa Loliondo anakazana tu kugawa vikombe badala ya kuwahubiri mafisadi, makahaba, majambazi, watoaji wa mimba, wabakaji, wagomvi, wauache uovu wao. Manabii wa kweli wa Mungu(kama Eliya) pamoja na kutenda miujiza, walihubiri Neno la Mungu kwa ujasiri sana.

  5. Nabii wa uongo hugeuza au kupinga baadhi ya Maneno ya Mungu. Babu wa Loliondo ni miongoni mwa wale wanaopinga ubatizo wa kibiblia wa maji mengi. Badala yake anatetea ubatizo wa watoto wadogo, jambo ambalo halimo katika Biblia. Yesu aliwabariki watoto, hakuwabatiza. Mtawatambua kwa matunda yao! Sio hilo tu anapinga pia agizo kuu la Yesu katika Marko 16:15-18. Katika mistari hiyo watumishi wa Mungu wameagizwa kwenda ulimwenguni mwote kuihubiri Injili na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapate afya. Yeye babu kwa ukaidi alionao toka 1991, badala ya kutoka na kwenda katika miji na vijiji (kama Yesu alivyofanya - Mt 9:35) ili kuwahubiri wenye dhambi na kuwapoza wagonjwa (walioko Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Namibia nk nk), eti ameamua kujenga makao ya kudumu huko huko porini. Hataki kutoka, halafu anasema Mungu amemtuma. Mungu hawezi kupingana na Neno lake.

  6. Nabii wa uongo hunukuu pia maneno ya Mungu. Asilimia kama 95 yanakuwemo kwenye Biblia lakini asilimia kama 5 ni uongo. Shetani alipowadanganya Adam na Hawa alitumia pia maandiko . Hata alipomjaribu Yesu alisema imeandikwa. Mathayo 4:6-7. Yesu alijua lengo lake ni baya akampinga. Babu naye vivyo hivyo, akiwa kanisani Jumapili ananena maneno ya Mungu lakini asilimia kama 5 ya yale anayoyasema yako kinyume na Biblia. Yesu aliwapa wanafunzi wake amri ya kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Yeye babu anasema anatibu magonjwa sugu tu.

  7. Nabii wa uongo hugeuza huduma kuwa biashara, ingawa hapendi ajulikane kuwa anafanya biashara. Miujiza na karama za Mungu hazitolewi kamwe kwa pesa. Yesu aliwaambia hivyo wanafunzi wake pale alipowapa uwezo wa kuponya. Katika Mathayo
  10:8 anasema: "Pozeni(ponyeni) wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure." Hiyo sh 500 anayotoza babu kwa kila mgonjwa sio sadaka kama yeye anavyodai. Sadaka haina masharti. Sadaka hutolewa kwa hiari na kwa moyo wa kupenda (Kutoka 35:29). Si kwa kulazimishwa. Kwa babu usipotoa hiyo 500, kikombe hupati! Babu anadai kwamba maelfu ya watu wanaokwenda kwake sasa hivi ni sehemu ndogo tu maana watu watatoka pande zote za dunia. Dunia ina watu zaidi ya bilioni 6. Hebu sasa jaribu kuwaza, iwapo watu bilioni moja tu duniani kote wanaumwa magonjwa sugu, wakija Tanzania na babu akawatoza sh 500, mwisho wa siku atakuwa amepata sh ngapi? 500x1,000,000,000=??? Kama huo sio wizi wa mchana ni nini? Ndio maana ameibuka nabii mwingine wa uongo, Rombo, na yeye anadai ameoteshwa atoe dawa kwa kipimo cha vikombe viwili. Watanzania, tuamke! Tuwe macho! Hata wenye digrii moja, mbili, tatu, tunakubali kudanganyika kirahisi namna hiyo? Na usomi wetu?

  Babu anasema watu wengi(+wazungu) watatoka nje ya nchi kuja kupata kikombe. Sidhani kama wazungu waliostaarabika wana muda wa kupanga foleni siku 7 wakingojea kwenda kwa babu. Sijui pia kama wazungu waliostaarabika watakuwa tayari kukaa mahali pasipo na vyoo au kwenda kujisaidia porini. Labda wazungu anaowasema ni wale watakaokuja kufanya utafiti kuhusu utendaji kazi wa waganga wa kienyeji na kwanini Watanzania tunaishi kwa dhiki kubwa huku tuna mlima mrefu kuliko yote Africa, madini ya Tanzanite,mbuga nzuri za wanyama, nk, nk, nk.

  Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo [wanaonekana watulivu kama babu alivyo] lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali...Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako...kufanya miujiza...ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

  Kumbe miujiza peke yake sio ishara kuwa aitendaye ametumwa na Mungu.

  Pinga, usipinge, babu wa Loliondo ametumwa na shetani, baba wa uongo na lengo lake ni kuwafanya watu walisahau Neno la Mungu, wasahau ahadi za Mungu, wadharau uponyaji wa kweli unaopatikana katika Yesu Kristo, waweke matumaini yao kwenye kikombe badala ya kumtumaini Mungu, hatimaye siku ile ya mwisho waangamie katika moto wa milele.

  "AONYWAYE MARA NYINGI AKISHUPAZA SHINGO, ATAVUNJIKA GHAFLA..." Mithali 29:1.
   
 2. Stevemike

  Stevemike Senior Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nimekuelewa kabisa maana neno la Mungu ndicho kipimo. Sasa kuna watu wasiojua biblia na hata wengine wasio na muda wa kuisoma wanataka kukutukana sasa hivi, jambo linalonikera sana. Badala ya kujibu hoja kwa hoja au maandiko, wanatumia mawazo yao na kutoa majibu ya kejeli sana. Haya sasa msikie huyu anayekuja!
   
 3. mediaman

  mediaman Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waache watukane tu. Hiyo inatujulisha kuwa shetani ameumbuka! Maana yeye akijua umegundua ujanja wake anajaribu kutumia hoja ya nguvu kukupinga. Alijaribu kushindana na Mungu kwani alishinda? Alipigwa mwereka "puu" akaanguka kutoka mbinguni...
   
 4. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Acha upuuzi wako bana!! wewe kama hauamini si ujikalikie tu kimya nyumbani kwako? wewe mchochezi nini!!?
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kirapuu............. Sorry!!!!!!
   
 6. mediaman

  mediaman Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG][​IMG]Piga hiyo kengele uwaite watu waje wasikie hoja zako. Au na hiyo kengele ni kirapuu?:teeth:
   
 7. mediaman

  mediaman Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUJIKALIKIA ndio nini?
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Maana yake ni shut the hell up. Ndiyo maana yake.
   
 9. Nditu

  Nditu Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Toa upupu wako shetani mkubwa wewe. Tutaendelea kuyahama masinagogi yenu mliyoyageuza bucha za kutuchinjia kiuchumi kwa "Jina la Yesu" mnayemkufuru na kumdhalilisha bila aibu. Mnatumia ujanja ujanja kutuibia. Nyinyi ni wabaya na hatari zaidi ya babu kwa maana kwa nje mnajionyesha wanyenyekevu lakini ni wabaya hata kushinda mbwamwitu! Tulipoacha madhehebu yetu kujiunga nanyi tulifanya hivyo kukidhi shauku zetu za kujinusuru na shidaa na matatizo yetu mlizokuwa mmeahidi kuzifanya historia.Mlitukamua hadi tone la mwisho wa damu bila huruma na sasa Mungu ametuonea huruma na kututumiaa mjumbe wake kuokoa binadamu (Tulioumbwa kwa mfano wake) bila hila, ghiliba, utapeli, uchochezi wala inda.. mnasema katumwa na shetani! Mnalia njaa? Nyinyi mna usafi gani hadi mumhukumu na kumwombea mabaya mwenzenu? Ni mungu yupi mwenye kuwasikiliza nyinyi mlio wasengenyaji, wachochezi, mnaojikweza, matapeli, baadhi yenu ni malaya wa kutupwa, masonic, na wafuasi waaminifu kwa ibilisi? Na bado mtaendelea kuumbuka hadi mfanye toba na kuzitupa hirizi zenu mlizotoa Nigeria na India.
   
 10. mediaman

  mediaman Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana. Stefano alipowahubiri wale watu katika Matendo ya Mitume na kuwaambia ukweli, walimsagia meno wakamtupia mawe na kumuua. Bwana Yesu akusamehe maana hujui ulisemalo na akuwezeshe kuurithi uzima wa milele maana uzima wa sasa ni wa kitambo tu. Amina
   
 11. s

  siyenda Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapa nchini na mahali pengine nje ya nchi kuna wachungaji waliojitengenezea majina makubwa na kuwaambia watu watoe sadaka ili MUNGU awatendee miujiza watu wametoa magari pesa nyingi na hao watumish wanatembelea magar ya kifahal maisha mazuri watoto wanasoma nje ya nje mtaji wao ni wagonjwa na wenye kuonewa na shetan wamewaombea bila mafanikio zaid sana wanazid kupanua makanisa na kujenga vitega uchumi kwa kuwanyang'anya wananch ardhi na kubomoa viwanda vyao, lakin maskin ya MUNGU babu hana hata bango la kumtangaza watu wameona wenyewe wameamin na wanakwenda. Hajasema huku kuna miujiza njoo upone na kupiga sana kelele ni wewe na matatizo yako unaenda,jaman achen ugomvi babu pesa nyingine anapeleka sadaka hao mitume wamefanya huduma kama ya babu na sadaka wanatoa wapi? Babu anaish kijijin nyumba isiyo na hadhi gari hana hebu linganisha maisha ya babu na watumish wengine wa MUNGU
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi mtoa mada hii anajiona yeye anaenda mbinguni????????? teh teh teh:lol::lol::lol::lol:
   
 13. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Hosea 4:6.
  Yohana 9:25.
   
 14. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu moja alikuwa kipofu na bwana YESU akamfungua macho yake siku ya sabato. Kwa wayahudi hii ilikuwa ni dhambi kwa mujibu wa TORATI. Wayahudi walipomuuliza (Aliyeponywa) kwa lengo la kumtega ili wapate kumshitaki YESU, Yeye aliwajibu kwamba" kama huyu(Yesu ) ni mwenye dhambi mimi sijui ninachojua ni kwamba mimi nilikuwa kipofu na sasa ninaona". Nadhani wanaokwenda kupata kikombe cha BABU pamoja na kuombewa sana makanisani( hasa ya kiroho)wameteseka muda mrefu na magonjwa mbalimbali na kama kweli dawa ya babu inawaponyesha wao hawajali kwamba BABU anatibu kwa nguvu za GIZA au kaoteshwa na MUNGU muhimu kwao ni afya. Mungu anaweza kutumia njia mbalimbali kusaidia viumbe vyake, pengine kweli katumia njia ya kikombe cha BABU. Nadhani tumwache MUNGU aitwe MUNGU
   
 15. s

  seniorita JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Njia za Mungu hazichunguziki, ni juu sana na mawazo yake pia ni juu sana...
   
 16. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  hawa watu waliojiunga Machi 2011 wanamatatizo kwanini babu tu?kwani manabii na Mitume wengine hawaikemei?
   
 17. S

  Strategizt Senior Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hujagundua ndugu hawa ndo walewale waliokimbiwa na waumini makanisani sasa wanahaha. Sasa kama babu wa Loliondo anadangaya si ukae kimya tu na uwaache hao watu unaosema kwamba sio wastaarabu waende.Eti anasema wazungu hawawezi kwenda kwa babu.... kwa taarifa yako wazungu wapo kwa babu kama kawaida.
   
 18. S

  Strategizt Senior Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sawa kabisa namimi nakusupport nimeshindwa kuona ki button hapo juu lakini nafikili mediaman amepata somo, maana toka alivyojiunga Jamii Forum threads zake zote ni za kumpinga babu kwa nguvu nahisi ni kati ya wale watu waliokimbiwa maeneo ya Mwenge. Teh teh teh:gossip::teeth:
   
 19. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kinachowauma ni nini? Mapato yamepungua nini?
   
 20. apakati

  apakati Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema Dunia ina watu zaidi ya bilioni 6. Hebu sasa jaribu kuwaza, iwapo watu bilioni moja tu duniani kote wanaumwa magonjwa sugu, wakija Tanzania na babu akawatoza sh 500, mwisho wa siku atakuwa amepata sh ngapi? 500x1,000,000,000=???

  Ndo shida yako kubwa labda ipo hapo!!!! Bilioni 500 inakunyima usingizi, ila zile ulizochotewa EPA n.k wala hazikunyimi usingizi. Halafu unasemaje wizi pale mtu anapofanya kazi na kulipwa. Ni sawa na wewe ugundue kitu leo, tuseme ugundue mseto ambao mtu akijipaka mara moja hatajipaka losheni wala mafuta tena na atanukia apendavyo daima, mfano tu, so ukianza kuuza kwa jelo, si lazima nawe utauza dunia nzima na kupata kama babu, kwani ugomvi?
  Mbona Nokia zinauza sana mtaani haikunyimi usingizi, nahisi watu 20m wenye simu Tanzania tu walau 15m ni Nokia, sasa 15,000,000x30,000 (chukulia simu ni TZS 30,000 tu) mbona hapo hapakunyimi usingizi?
   
Loading...