Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu

Mimi nadhani mahakama zetu badi zinajikongoja. Kwa hali hii inaonekana wengi wapo magerezani bila hatia. Hawa wawili walioachiwa huru inaonekana walihukumiwa bila kosa, sasa je tujiulize huko magerezani kuna watu wangapi wa namna hii na hawawezi kukata rufaa? Inabidi mfumo wetu wa mahakama hapa nchini uangaliwe upya. Au wapewe Majembe Auction Mark?

Kurudishwa kwa nguza na papii sililipingi ila ninawasiwasi mkubwa kama walitendeawa ndivyo, ina maana kwa makosa yao kama yanavyofikiriwa ni
lazima wafungwe maisha? Hamna hukumu nyingine? Waliuoa Maalbina wafungwe maisha, Waliolawiti na kubaka wafunwe maisha, je kuna balance hapo?Mimi nadhani Wangepewa hata 30 ili waweze kujirekebisha. Pia tunaposema kifungo cha maisha ni miaka mingapi? Tunaamini pia hata mtu akifa hua anaendelea kuishi kiroho, hapo napo kifungo kinaendelea?

Unajua jamii ndio msema kweli, pia kilio cha watu wengi hua ni kikali sana. Ukisikia kila mmoja analalamika ujua kuna jambo hapo. Wapo wengi wanahukumiwa lakini jamamii hailalamiki pia wapo baadhi huachiwa lakini pia jamaii hulalamika. Ukiona watu wengi wanalalamikia jambo basi ujue haki haikutendeka. Tatizo kubwa la sheria, kama hujui kujitetea hata kama hukutenda kosa, basi unaweza kuhumiwa kifo ukiwa unaona.
Ila Mungu hua hafichwi kitu, kama haki haikutendeka yeye atalipa. Ila kama pia kuna mkono wa mtu asiyemwogopa Mungu basi atajibu yeye mwenyewe kwake Muumba.
 
katika Jamhuri kosa kubwa kuliko yote ni kosa la uhaini, na kama nakumbuka vyema mzee Mwinyi aliwahi kuwasamehe , jamaa fulani hivi waliohusika na tukio la UHAINI la mwaka 1984....kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, nasema mfano huo kwasababu naamini hakuna mkosaji ambae Rais wa Jamuhuri hana uwezo wa kusamehe......kama nakosea nipo tayari kupokea maoni ya kisheria juu ya hili kwaajili ya kujifunza.
Acha longolongo Rais hawezi kutoa msamaha kwa wabakaji na akifanya hivyo itabidi naye achunguzwe unajua inauma sana mwanao unamlea kwa nguvu zote linakuja jitu lingine linakuaribia mwanao,hapa bw hakuna cha ushauri wala nini afungwe tu na akiachiwa ndo hapo wanauchungu kama mimi huwa tunachukua sheria mkononi
 
wanaweza kukata rufaaa tena, ngoja tuone...ila nina amini watatoka tu ni vile serikali inajishaua tu na inaona noma kuwaachia huru wote kwa pamoja!
 
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=5fThC7zQch0"]http://www.youtube.com/watch?v=5fThC7zQch0[/ame]
 
hii ni kesi ya kubaka ya minors (watoto) hawawezi wakatoa ushahidi hadharani watu wote muwajue halafu wawe wananyooshewa vidole maisha yao yote!
ndio maana ushahidi ulikua wa siri, ila asasi mbalimbali za watoto, kama UNICEF zilikua zinapeleka lawyers wao huko, na kujua yaloyotokea, ndio maana wamenyamaza, yeyote aliyekuwepo wakati hao watoto wanatoa ushahidi anawasikitikia sana hao watoto waliofanyiwa unyama!
 
katika Jamhuri kosa kubwa kuliko yote ni kosa la uhaini, na kama nakumbuka vyema mzee Mwinyi aliwahi kuwasamehe , jamaa fulani hivi waliohusika na tukio la UHAINI la mwaka 1984....kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, nasema mfano huo kwasababu naamini hakuna mkosaji ambae Rais wa Jamuhuri hana uwezo wa kusamehe......kama nakosea nipo tayari kupokea maoni ya kisheria juu ya hili kwaajili ya kujifunza.

Mkuu Nguvumali,
Jaribu kusoma sheria inayosimamia bodi ya misamaha [Parole Board Act] na ndiyo maana hata kwenye misamaha huwa inaweka wazi kwamba wabakaji et al hawapati msamaha wa rahis.
 
the three appellants, together with their relatives cried loudly.

Papii Nguza is the only one that did not cry.

Hata mimi nisingelia kwakweli kwani haijasaidia kitu! Kama nikifungo bado anakitumikia! Na huyu Papii anajua kabisa kwamba kuna 'back stubber' ambaye anawakandamiza, na huyo mtu ndiyemwenye mamlaka hata akisema kesho kwamba watoeni hao 'watatoka'
 
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=EqnvUKFZueA"]http://www.youtube.com/watch?v=EqnvUKFZueA[/ame]
 
Acha longolongo Rais hawezi kutoa msamaha kwa wabakaji na akifanya hivyo itabidi naye achunguzwe unajua inauma sana mwanao unamlea kwa nguvu zote linakuja jitu lingine linakuaribia mwanao,hapa bw hakuna cha ushauri wala nini afungwe tu na akiachiwa ndo hapo wanauchungu kama mimi huwa tunachukua sheria mkononi
acha jazba, nilichouliza kama Rais anaweza kumsamehe mtuhumiwa wa UHAINI, je anaweza kusamehe mbakaji ? usizungumzie MORAL issues hapa, leta sheria na kanuni zinasemaje. je Rais hana mamlaka kisheria kusamehe wabakaji kama akiona inafaa...?
 
Mkuu Nguvumali,
Jaribu kusoma sheria inayosimamia bodi ya misamaha [Parole Board Act] na ndiyo maana hata kwenye misamaha huwa inaweka wazi kwamba wabakaji et al hawapati msamaha wa rahis.
asante, acha nami nijaribu kuisoma hiyo sheria, insake of learning......ili kupata maarifa, nakuweza kuwa wakili mzuri wa umma...asie rasmi.
 
Serikali kama imeona kwamba watoto wa mzee nguza hawana hatia,
Je, inampango gani wa kuwalipa fidia ikiwa ni pamoja na kuwarudisha shuleni? Vipi msaada wa kimaisha kwani baba yao hali ndiyo hiyo tena! Serikali mnasemaje?
 
nguza hangeweza kuachiwa labda serikali ije nyingine.....wanaojuwa wameelewa!! hata hao walioachiwa wawili ni at least ..kwa kuwa mahakama ya rufaa ipo somehow free..
unataka kutudanganya nini? au una maana gani hapa! jamani usiseme kitu kama huna ushahidi njooni sinza hapa mfanye uchuguzi wahanga wapo tena wakubwa sasa hivi wanajua kila kitu
 
katika Jamhuri kosa kubwa kuliko yote ni kosa la uhaini, na kama nakumbuka vyema mzee Mwinyi aliwahi kuwasamehe , jamaa fulani hivi waliohusika na tukio la UHAINI la mwaka 1984....kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, nasema mfano huo kwasababu naamini hakuna mkosaji ambae Rais wa Jamuhuri hana uwezo wa kusamehe......kama nakosea nipo tayari kupokea maoni ya kisheria juu ya hili kwaajili ya kujifunza.

Technically parole boards ndizo zinazopendekeza kwa Rais, wafungwa wanaotimiza vigezo vya kuachiwa kwa msamaha wa Rais (Parole). Kina Babu Seya hawakidhi vigezo vinavotakiwa chini ya kifungu cha 4 cha Parole Boards Act, 1994.
 
Shy hili ni swali gumu sana ..hata hao mawakili wamekubaliana na hiyo Hukumu
>>ukweli uko wapi ??
Namkumbuka Seya wa Miparo jamani papiii kipaji kimefifia ,kipaji kimezimwa kama mshumaa katika upepo ....

mama sasa na hao watoto walioharibiwa nani awalipe?
tusiangalie upande mmoja tu, pata picha kama aliyefanyiwa ni mwanao, kwa sababu nna uhakika kosa lilitendeka, ila sio wote wanne walifanya, ndio maana Babu Seya alikua anasema atoke huyo last born wake, anajua mwenyewe alifanya nini! na ndio maana mahakama imewaachia wawili wasio na hatia!
 
wanaweza kukata rufaaa tena, ngoja tuone...ila nina amini watatoka tu ni vile serikali inajishaua tu na inaona noma kuwaachia huru wote kwa pamoja!

Watakata rufaa mahakama gani tena ya juu zaidi ya hii??
 
Kweli lakini ktk maisha lazima kuwepo na chuki kwani watu hawawezi kukupenda wote lazima kuna maadui hata uwe mtenda mema vipi maadui hawakosekani!
 
acha jazba, nilichouliza kama Rais anaweza kumsamehe mtuhumiwa wa UHAINI, je anaweza kusamehe mbakaji ? usizungumzie MORAL issues hapa, leta sheria na kanuni zinasemaje. je Rais hana mamlaka kisheria kusamehe wabakaji kama akiona inafaa...?
Hana mamlaka
 
Watakata rufaa mahakama gani tena ya juu zaidi ya hii??
Wataomba case yao kupitiwa tena!
Kwani sheria inasemaje hapo? Ingekuwa vyema kabla mheshimiwa hajatoka madarakani basi apitishe 'msamaha'
 
Mwanakijiji wewe una uhakika kuwa walibaka ? swala hapa linavyoangaliwa haya mambo hayaeleweki eleweki ndo maana tunashangaa
Kama wote walibaka kwanini wawili watoke wawili wabaki wakati tendo ni lile lile??KUbAkA

Bibie, tuna uhakika kwamba babu seya na papii wamebaka, na tunaweza kuwaita wabakaji bila shaka yeyote, mahakama ya juu kabisa ishathibitisha.

tatizo watanzania mtu akishakua maarufu tunamfia kabisa, au ndio dawa wanazoendea kwa waganga walikoambia wabake, ndio zinatupumbaza?

ushahidi umethibitisha bila shaka kwamba wawili walibaka, sasa mnang'ang'ania mbona wengine wameachiwa, kama hamna ushahidi wa kutosha wafungwe tu?
 
Wataomba case yao kupitiwa tena!
Kwani sheria inasemaje hapo? Ingekuwa vyema kabla mheshimiwa hajatoka madarakani basi apitishe 'msamaha'

sitaki kuamini kama watanzania mnapenda watu waliobaka wasameheewe, basi lisiwe kosa, watu tuwe tunabakana tu tunaendelea na maisha yetu!
 
Back
Top Bottom