TANZIA Babu Njenje Mabruk amefariki dunia alfajiri ya leo

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,238
Babu Njenje Mabruk amefariki dunia alfajiri ya leo.

IMG-20200524-WA0024.jpg

MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya Kilimanjaro maarufu kama Wana Njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo Jumapili, Mei 24, 2020 jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu mmoja wa watu wa karibu na Babu Njenje, Babu Ally alisema mzee Njenje amefariki alfajiri ya leo.

"Mzee amefariki alfajiri ya leo na msiba wake upo Upanga hapa alipokuwa anaishi na taratibu zote za msiba zinafanyika hapa nyumbani kwake.

"Alikuwa anasumbuliwa na kiharusi kwa takribani miaka mitano, juzi juzi pia akapata kiharusi kingine, ndugu yangu niache kidogo nipo kwenye kikao," alisema.

Babu Njenje, ambaye ametamba akiwa na bendi ya Kilimanjaro, ameacha watoto wawili mpaka umauti unamfika.
Mkongwe huyu anakumbukwa kwa nyimbo zake kama Njenje, Kinyaunyau na nyingine nyingi zilizowahi kutamba miaka ya nyuma.

Njenje atazikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar leo saa kumi jioni (10:00).


Chanzo: Mwanaspoti
 
Oooohhh
Mmekisha zoea (haloooooh)
Kusemwa semwa na watu
Yakwao hawa yaoni
Kazi kusema ya watu
Basileo na wambia
Maneno yenu sijali
Mtabki ivyoivyo
Ya kwangu yani nyokea eeeh
Wacha Wacha waseme
Watasema mchanaeeh
Usiku wata lala
Wacha Wacha waseme



R.I.P Mr Njenje
 
Back
Top Bottom