TANZIA Babu Njenje Mabruk amefariki dunia alfajiri ya leo

Duh! Kuna watu wanapenda muziki na marehemu mzee njenje na kilimanjaro band yake hawamjui si masihara haya.
Labda kama muziki umeanza kusikiliza hivi karibuni.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Babu Njenje Mabruk amefariki dunia alfajiri ya leo.

MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya Kilimanjaro maarufu kama Wana Njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo Jumapili, Mei 24, 2020 jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu mmoja wa watu wa karibu na Babu Njenje, Babu Ally alisema mzee Njenje amefariki alfajiri ya leo.

"Mzee amefariki alfajiri ya leo na msiba wake upo Upanga hapa alipokuwa anaishi na taratibu zote za msiba zinafanyika hapa nyumbani kwake.

"Alikuwa anasumbuliwa na kiharusi kwa takribani miaka mitano, juzi juzi pia akapata kiharusi kingine, ndugu yangu niache kidogo nipo kwenye kikao," alisema.

Babu Njenje, ambaye ametamba akiwa na bendi ya Kilimanjaro, ameacha watoto wawili mpaka umauti unamfika.
Mkongwe huyu anakumbukwa kwa nyimbo zake kama Njenje, Kinyaunyau na nyingine nyingi zilizowahi kutamba miaka ya nyuma.

Njenje atazikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar leo saa kumi jioni (10:00).

Chanzo: Mwanaspoti
Rest Easy Grand pa....surely you will be missed legendary....
 
Duh! Kuna watu wanapenda muziki na marehemu mzee njenje na kilimanjaro band yake hawamjui si masihara haya.
Labda kama muziki umeanza kusikiliza hivi karibuni.
Ni uwendawazimu au ulimbukeni umewaganda...
Kama mtu haujui wimbo wa Kinyaunyau wa Njenje basi Sitishiki ya Chuchu Sound haufahamu au Chozi la Mnyonge la FM ACADEMIA halijui au kisa cha Mpemba wa Banza Stone nacho hakifahamu... Basi atulie siyo lazima Ufahamu yote.
 
Itakuwa ni wameanza kusikiliza/kufatilia muziki huu ambao wengine tumeacha kusikiliza.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom