Babu Masapila afikisha milioni 50/-

Miruko

Senior Member
Feb 8, 2008
173
46
Chururu si ndondondo. Haba na haba ujaza kibaba. Matone Matone ujaza ndoo. Babu Ambilikile Masapila yeye hukusanya sh 500 kutoka kwa kila anayepata kikombe.

Habari za kuaminika makusanyo hayo yamefikisha sh milioni 50. Kutokana na uwiano wa 1:2:2 kwake yeye, kanisa na wasaidizi wake; basi babu kashajiingizia milioni 10/-. kanisa KKKT litapata milioni 20 na wasaidizi wake watagawana milioni 20/-

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati limetangaza kiwango cha fedha ambazo zimekusanywa kutoka kwa wagonjwa wanaokunywa kikombe cha dawa ya Mchungaji Ambilikile Masapila kuwa ni sh milioni 50.

Akitangaza fedha hizo jana, Askofu wa kanisa hilo, Thomas Laizer alisema fedha hizo zimepatikana tangu kuanza kwa tiba hiyo mwishoni mwa mwaka jana, kutokana na mchango wa sh. 500 kutoka kwa kila mgonjwa.

Kutokana na mgao wa fedha hizo kama alivyosema Babu ni kuwa yeye anabaki na sh 100 huku sh 200 zikienda kanisani na 200 kwa wasaidizi wake, yeye atapata sh milioni 10. Kanisa sh. milioni 20 na wasaidizi wake sh milioni 20.

Lakini Babu mwenyewe alishasema kuwa hatatumia fedha hizo hadi Mungu aliyemwotesha kuanza huduma hiyo amwelekeze jinsi ya kuzitumia. Mambo hayo!

Wakati huo huo, Kanisa hilo limekamilisha mipango ya ujenzi wa banda kwa ajili ya tiba ya Mchungaji Ambilikile Masapila ‘Babu’ kijijini Samunge litakalogharimu sh. milioni 100 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya mchungaji huyo.

Jengo hilo litakalohudumia watu 700 kwa wakati moja litakua la mviringo na litajengwa karibu kabisa na babu anakotolea tiba hiyo hivi sasa ambapo kutakuwa na viti vya watu zaidi ya 300, eneo la kutolea dawa, kuchemshia dawa hizo na sehemu ya kuhifadhia hiyo dawa.

Askofu Laiser alisema jana kuwa uamuzi huo umekuja wakati ambao idadi kubwa ya watu wanateseka kumfikia mchungaji huo kwa kuwa katika jua kali, na wakati mwingine mvua wakisubiria tiba.

Alisema ujenzi huo utaanza hivi karibuni huku akiwaomba watu wengine ikiwemo serikali kutoa ushirikiano katika kukamilisha malengo yaliyokusudiwa ili tiba hiyo ipatikane katika mazingira mazuri na yenye tija.

“Kanisa limeona ni wakati sasa wa kujenga jengo hili litakalochukua idadi hiyo ya watu na kutolewa huduma zingine bila ugumu wowote. Tangu kuanza kwa tiba hiyo watu na wagonjwa wanaotoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi walikuwa wakisimama kusubiri tiba hiyo,” alisema Askofu huyo.

 
Wakuu hadi sasa babu amekusanya sh. Milioni 50 hadi jana kutokana na malipo wanayotoa wagonjwa ya sh. 500 kwa kikombe. Kutokana na makusanyo hayo kanisa limepata milioni 20 kwa mgao wa sh.200 kutoka kwa kila mgonjwa pesa mbazo kwa mujibu wa askofu mkuu kanda ya kaskazini Bw. Thomas Laizer zitatumika kuboresha jengo la matibabu.
Source: Magazeti ya leo
 
Babu hakutoa matangazo magazetini watu waende kwake!! wenyewe mmejipeleka kule mpaka mawaziri wenu nao wanapigana vikumbo kutafuta kikombe!

Please leave the poor babu alone! Kama mnaona ni biashara nzuri jaribuni na nyinyi basi!
 
Back
Top Bottom