- Thread starter
- #41
sasa kama hizo za kisasa zimeshindwa?inakuaje hapo?
Hazijashindwa ila sisi wenyewe wagonjwa ndio tunasababisha dawa zisifanye kazi! Mfano mgonjwa wa Kisukari anapewa dawa na kuambiwa afanye mazoezi ya mara kwa mara na kupunguza kula vitu vitamu badala yake anakula dawa halafu anakula ugali na nyama choma sufuria nzima, huku akiteremshia kwa COCA COLA na jioni bia mpaka alewe unafikiri atapona? au mwingine anapakia Pilau iliyokaangwa na nyama ya mbuzi huku akinywa chai iliyojaa sukari baada ya hapo anachoka kwa viungo vya pilau na kukimbilia kitandani na kuuchapa usingizi unategemea hiyo dawa ya Kisukari kufanya kazi!!!
Hakuna njia ya mkato ili upone au kupunguza makali ya maradhi hatuna budi kufuata masharti ya dawa au tutegemee Mtu mwingine ajitokeze na kugawa dawa ya kuwa Tajiri!!!!!