Babu loliondo na stone age period!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu loliondo na stone age period!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kadogoo, Mar 12, 2011.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ikiwa Leo tuko karne ya 21 ya Teknologia na maendeleo ya kiwango cha juu ktk nyanja mbali mbali kama vile tiba kulinganisha na karne zilizopita, nimasikitiko na majonzi makubwa kwa baadhi ya Watanzania wenzetu hasa hao wanaojiita Viongozi wa Dini kutaka kuturudisha Enzi za Mawe au enzi za falsafa za Vita vya MajiMaji!!!! kwa kutuletea Tiba zinazotokana na Ndoto au Maono toka Mbinguni!!!!

  La kusikitisha zaidi Serikali yetu inapokubali shingo upande huduma kama hiyo iendelee kutolewa huku ikijulikana wazi kabisa ubora wa dawa hiyo ni wa hali ya chini na inayotolewa ktk mazingira machafu kabisa ya kutumia kikombe alichotumia mgonjwa mwingine!! Nchi hii ina Madaktari bingwa waliobobea ktk fani zao, Waganga na Wataalamu mbali mbali wenye Ma PHD, Digrii sasa iweje Mchungaji mmoja tu ajitokeze na kudai kaoteshwa na Mungu mwaka 1991!! halafu tiba yake anakuja ianza mwaka 2011?????

  Tumeshuhudia wagonjwa wengi kupoteza maisha baada ya kunywa dawa hiyo na wengine wataendelea kufa huku Serikali ikishindwa kuchukua hatua muafaka kwa kuhofia shinikizo toka kwa baadhi ya watu wanaofaidika na mradi huo uliobuniwa na baadhi ya Vigogo wenye maslahi yao!!!

  Kama Serikali itakubali huduma hii PRIMITIVE iendelee kutolewa na huyu Mchungaji basi tukubali kuwa nchi yetu imeamua kurudi ktk Enzi za STONE AGE na Elimu ya Tiba za kisasa zenye kutegemea LABORATORY EQUIPMENTS zitakuwa hazina faida tena na kutakuwa hakuna haja ya kuwaelimisha Watoto wetu Elimu ya Tiba za Kisasa na badala yake tuwe wategemezi wa NDOTO ZA USIKU TOKA MBINGUNI!!!!!!!!!

  Wakati umefika sasa SERIKALI iamke na kuchukua hatua za haraka kuzuia hekaya hizi za kizamani za kutegemea Ndoto au tabiri za Wachungaji, Mashehe au Waganga wa Kienyeji kwani sasa wanakotupeleka kuna giza kuu!!!!
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hasa Kikwete aliyekuwa wa kwanza Kwenda kuinywa, lakini mbona yeye hajafa au unadanganya?!

  Nakapona ule ugonjwa wa kuanguka mara kwa mara mpaka ana test ndege za kivita sasa!
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Zubeda mambo haya hayataki siasa wala dini. Nakuhakikishia kuwa mawazo yako ndo ya stone age,magumu kama mawe. Kama unadhani Mungu hayupo na umejiumba,ndo unafanya usiku na mchana na mvuna na mawingu kuwepo ndo uendelee na stone age ideas. Ktk ili nakushauri uache UDINI mbali na kumkubali Mungu! Kama hujawai kuumwa mshukuru Mungu wala si kumbeza Mungu! Waulize akina mama Salma na mh.walivoenda uko kwa babu wa maono ndo upate akili. Zubeda umekuwa bingwa wa kupinga mawazo yote yanayohusu imani za watu lakini ktk ili usijaribu kuingiza mambo yako. Elewa kabisa wengi watakaochangia hapa watakushangaa ndugu! Hapa hata angekuwa ustadhi mwenzio akapata maono kama haya wote tutamwamini na akituponya tutamwamini. Hamna sehemu yoyote yenye sharti kuwa mtu akitumia ile dawa basi awe mfuasi wake,hapana. Hapa ni ufunuo uliokuja kuwaponya mataifa! Huwezi kunieleza kuwa we una akili nyingi kuliko waliokubali ikiwemo serikali yako. Unajadili stone Age,we unaielewa historia kweli au umefundishwa kuichukia dunia?unajua miujiza ipi iliyotokea ktk stone age uliyosema?au unaisi kusema stone age unarefer kipindi gani?cha miujiza au? Jifunze na utambue kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza kupitia watu aliowaumba yeye.Usitegemee hata siku moja Mungu atangaze kuwa kuanzia tarehe flan atakuwa sehemu flani akitibu na kufanya miujiza,hapana! Yeye atafanya ivo kupitia Mi na wewe na watu wote wa mataifa! Jifunze kuelewa kuwa Mungu yupo. Nina mengi ya kuongea lakini nahishia apa wala sitajibizana nawe,hata mimi mchungaji si wa imani yangu lakini kwa ili naomba Mungu ampe maono zaidi na maisha marefu. Siku njema.
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Miongo mingapi imepita toka hayo magonjwa yakose tiba yake kutoka kwa wanasayansi?
  Pale zinapogota akili za wanasayansi ndipo zinapoanzia za Mungu. This is the marvellous tremendous truth, whether you like or not!!
  .
   
 5. Fisadi Mkuu

  Fisadi Mkuu Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonekana inakuuma kweli kuona babu wa watu anavyokubalika.Mbona hujamzungumzia Shehe Yahaya au kwa kuwa ni wa dini yako?Na bado babu wa watu atatesa sana hata wewe utaenda tu kwa babu ukatibiwe hako ka ugonjwa kanakokusumbua.
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 713
  Trophy Points: 280
  some people are alive simply because its illegal to kill them.......
   
 7. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,563
  Likes Received: 3,859
  Trophy Points: 280
  With all due respect Zubeda hatuko karne ya 21! tulidanganywa hivyo, tumeamini hivyo , ukweli tunaishi karne ya 15 au 16, haiwezekani dunia mbili zikaishi karne moja, dunia ya kwanza ndiyo wako hiyo karne.

  I am just giving you a challenge; industrial revolution imetokea karne ya 18 huko ulaya na ikawalazimu kuja africa kufuata malighafi.....Je nchi zetu za dunia ya tatu zimefikia hiyo stage??

  tungekuwa karne ya 21 usingeandika ulichoandika maana automatically tungekuwa tunaishi hivyo, kama hauamini wale unaowaita wenye PhD ndiyo walioenda huko, matechnician wa maabara ndio wako huko, Nchi yako haiamini maabara wala tafiti, leo unasema wako karne ya 21!!???

  Tumedanganywa inatosha sasa!

  cheers
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,563
  Likes Received: 3,859
  Trophy Points: 280
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nchi nyingi sana hapa duniani wanatumia dawa za asili wamepanda mabustani makubwa makubwa wanawasaidia watu wao waweze kuzitumia kwa ufahamu zaidi kwa kuwapa elimu India,China,Japani,Thailand,Afrika ya kusinni na zingine nyingi,kwa hiyo tutafute njia bora tuu za kuboresha mazingira ya kutolea dawa,Spiritual healing ni aina ya tiba inajulikana sana hapa duniani unaweza kugoogle ukapata taarifa nyingi tuu,hakuna kosa kwa Babu kutoa dawa hiyo na hata approach anayotumia,,la msingi aboreshewe mazingira full stop.
   
 11. howard

  howard Senior Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  we hizo habari za watu kupoteza maisha baada ya kunywa dawa kakwambia nani? waliokufa walikuwa kwenye foleni na walikuwa hawajamfikia BABU. unaingiza siasa kwenye tiba umechanganykiwa? Bongo bwana kila kitu mtu anawaza vigogo kufaidika hata la babu.
   
 12. U

  Udomasa New Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama vile nakubaliana na wewe dada Zubeda!! Time will tell
   
 13. Chrizo

  Chrizo JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 583
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 80
  Siwezi nikakushanga maana najua we ni mfuasi wa kakobe. Na una ushahidi gani kuwa huu ni mradi wa vigogo na tunaomba uwataje. La sivyo ufunge hilo domo lako
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Zubeda pole sana. Pole kwa kufiwa na bibi yako! Hizo zote ni hasira tu. Hakika naamini kama bibi angepona wala usengekuwa unasema hayo. Mimi nina kaka yangu nimempeleka kule alikuwa aende India kwa matibabu na tuliteseka sana kupata fedha ya kumpeleka huko! Amini kuwa Mungu ana mipango yake! Sasa hatuzungumzii tena India! Ana nguvu huwezi kuamini. Katika kundi hilo pia kulikuwa na shemeji yangu ambaye alikwisha pelekwa india kwa amtibabu ya figo. Naye alikwenda huko kwa Mchungaji akiwa njiani akaaga dunia. Hili ni changamoto kwetu. Chungu na tamu kwa wakati mmoja. Lakini tunajiuliza hali ya huyu shemeji yetu. Hali yake ilikuwa mbaya sana. Alikuwa amedhoofu sana na hata kutoka Dar kuja moshi shurti kwa ndege! Sasa jiulize ile hali ya barabara na hali ya mgonjwa si kummaliza! Yeye mwenyewe alikiri kuwa figo aliyowekewa imechakachuliwa na ukweli ime-fail. Zubeda na familia yako hamkulazimishwa kwenda huko! Yote ni katika kutafuta ahueni kwa maradhi yanayokusibu. Inakuwa faraja sana pale mgonjwa wako anapopata ahueni lakini huwa chungu sana unapompoteza mpendwa wako.
  Kuna watu hata waliwahi kupewa tiba ya mkojo wako. Yaani wanathubutu kukwambia kuwa ule mkojo wa asubuhi kunywa glasi moja! Fikiria hii, uchafu mtupu! Lakini kwa kuwa mtu anaumwa anakubali kunywa! Na wengine wanatoa ushuhuda kuwa mkojo umewasaidia!
  Amini pia kuwa iko siku kiumbe hiki kiishicho lazima kionje mauti. Mauti yanamkuta mtu fulani mahala fulani na kwa style tofauti. Hivyo amini kuwa aliyekufa ilikuwa ndo style yake tosha! Wewe unaweza fikiri kuwa huo ni upuuzi lakini hata walokuzidi wewe wanaamini kuwa wanaweza kupona. Ni kipi bora, kusubiri wataalamu wanaokaa USA wanaotutangazia kuwa wako njiani kukamilisha dawa ya UKIMWI ama mchungaji aliye hapo Loliondo anayekupa kikombe kimoja cha dawa na unapona kwa imani yako! Na wakigundua hiyo dawa mpaka uje kuipata wewe mlala hoi ni lini? Mimi nikwambie tu tumehangaika sana na huyu kaka yangu kupata tiba huko India! Tungekuwa na hela tushampeleka siku nyingi! Angalia Mungu alivyo wa ajabu. Ameamua kumponyesha hapa hapa kwa kikombe cha shs 500 tu.
  Halafu usiwadanganye watu wangu, watu hawatumii kikombe kimoja kama unavyosema! Huo ni upandikizi wa chuki na fitna zisizo na msingi.
  Katika kila zuri na baya pia limo. Kuishi bahati kifo lazima mpendwa. Poleni tena kwa msiba wa bibi.
   
 15. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  me nauhakika kama hii dawa angetengeneza mzungu kwa hayo hayo majani ungekua wa kwanza kuinywa, jamani tuache kua tunaji dharau wenyewe......nazan unajua yale madawa ya GNLD,FOREVER LIVING,na dawa nyingi za kichina na mwengineyo,mfumo wake ni huu huu wa mitishamba tofauti wao wanaweka kwenye plastic tu,so me nasema hii dawa haina ttz sbbb katengeneza huyu mzee ndo maana mnaona kma ni ya mganga wa kienyeji ila me naona kwakweli hakuna ttz,we kama unaona tabu si mbaya kutokwenda wanaoenda waache waende nasikia jana Dr Hosea wa PCCB kaenda huko ni phd yake ya sheria
   
 16. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ukosawa, naungamkono hoja. %100
   
 17. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Halafu huyu mchungaji kama alioteshwa na Mungu ili atibu watu, ina maana hoyo Mungu amemlazimisha atibie wagonjwa huko kwake? kwani hawezi kuja Arusha mjini penye maji, na huduma mbalimbali kama hoteli na migahawa ya kutosha? inakuaje huyo Mungu amlazimishe kutibia watu porini kusiko na maji wala huduma bora za kijamii? yaani huyo Mungu wake anataka watu wapone au wafe kwa kuharisha na kukaa ktk foleni ndefu?

  jamani tuache ushabiki wa kidini na tuamke kukemea maovu!!!!
   
 18. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kunyweni dawa,theres no problem in trying alternative medicine,afterall haicost kitu zaidi ya jero,kama haifanyi kazi then unaangalia ustaarabu mwengine at least umejaribu lakini....:smash:
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mwenzetu ushakunywa nini, mimi nakubaliana na Zubeda na siku si nyingi mtaona matokeo yake. Huyu babu alitakiwa asimamishwe uchunguzi ufanyike ionekane kweli dawa hizi zinatibu na wamepona wangapi,tena kwa kuthibitishwa na daktari sio mtu hakupata dalili siku moja kwa imani kuwa amepona anajitangaza amepona, nanusa harufu ya janga hapa.
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Zubeda ijapokuwa umetumia maneno makali ila uko sahihi na mtazamo wako na iko siku ataamka mtu atasema wafuasi wake wote ameoteshwa na mungu kuwa kesho ndio mwisho wa dunia tunatakiwa kufa ndio yatatokewa maafa kama ya Mchungaji Kibwetere.
   
Loading...