Tujiulize sana! Sijui kama Wanaotuongoza wana Akili Timamu

Tujiulize sana! Sijui kama Wanaotuongoza wana Akili Timamu

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,319
Reaction score
3,128
Baadhi yetu tumeona taarifa za sherehe ya mchungaji kutunukiwa u-profesa na chuo cha Amerika. Afisa mkuu wa serikali aliyehudhuria ni Profesa Kabudi. alikuwa ana-smile! Ni huyu huyu ambaye karibuni alikuwa Vatican kuomba Papa aiombee nchi. Ni huyhuyu aliyemwita JPM Mungu. Ni huyuhu aliyeleta dawa ya Madagasca na kusifia kama tiba ya COVID-19.

Siyo huyu tu, wapo wengi ikiwa ni pamoja na huyo waziri wa mambo ya nje ambaye hata ukimwangalia ktk picha, unaona dalili za kitu kibaya kichwani. Bado yupo waziri Mkuu ambaye haeleweki anazungumza nini. Rais hatuna hata la kusema alivyo na tunavyomwelewa.

Je, kweli tunaongozwa na akili timamu au ni sisi tusioelewa hizi ni akili kubwa? Kweli Profesa mzima anayefahamu maana ya mtu kuwa profesa, anaweza kuwa kwenye sherehe ya aina hii? Mwishoni nimeuliza maisha ya Kabudi akiwa Chuo kikuu cha Dar, inasikitisha. Hakustahili hata kuingia serikalini.
 
Back
Top Bottom