Ikiwa Leo tuko karne ya 21 ya Teknologia na maendeleo ya kiwango cha juu ktk nyanja mbali mbali kama vile tiba kulinganisha na karne zilizopita, nimasikitiko na majonzi makubwa kwa baadhi ya Watanzania wenzetu hasa hao wanaojiita Viongozi wa Dini kutaka kuturudisha Enzi za Mawe au enzi za falsafa za Vita vya MajiMaji!!!! kwa kutuletea Tiba zinazotokana na Ndoto au Maono toka Mbinguni!!!!
La kusikitisha zaidi Serikali yetu inapokubali shingo upande huduma kama hiyo iendelee kutolewa huku ikijulikana wazi kabisa ubora wa dawa hiyo ni wa hali ya chini na inayotolewa ktk mazingira machafu kabisa ya kutumia kikombe alichotumia mgonjwa mwingine!! Nchi hii ina Madaktari bingwa waliobobea ktk fani zao, Waganga na Wataalamu mbali mbali wenye Ma PHD, Digrii sasa iweje Mchungaji mmoja tu ajitokeze na kudai kaoteshwa na Mungu mwaka 1991!! halafu tiba yake anakuja ianza mwaka 2011?????
Tumeshuhudia wagonjwa wengi kupoteza maisha baada ya kunywa dawa hiyo na wengine wataendelea kufa huku Serikali ikishindwa kuchukua hatua muafaka kwa kuhofia shinikizo toka kwa baadhi ya watu wanaofaidika na mradi huo uliobuniwa na baadhi ya Vigogo wenye maslahi yao!!!
Kama Serikali itakubali huduma hii PRIMITIVE iendelee kutolewa na huyu Mchungaji basi tukubali kuwa nchi yetu imeamua kurudi ktk Enzi za STONE AGE na Elimu ya Tiba za kisasa zenye kutegemea LABORATORY EQUIPMENTS zitakuwa hazina faida tena na kutakuwa hakuna haja ya kuwaelimisha Watoto wetu Elimu ya Tiba za Kisasa na badala yake tuwe wategemezi wa NDOTO ZA USIKU TOKA MBINGUNI!!!!!!!!!
Wakati umefika sasa SERIKALI iamke na kuchukua hatua za haraka kuzuia hekaya hizi za kizamani za kutegemea Ndoto au tabiri za Wachungaji, Mashehe au Waganga wa Kienyeji kwani sasa wanakotupeleka kuna giza kuu!!!!