Baba yangu siku ya nne fahamu hakuna

Baba yangu siku ya nne fahamu hakuna

Sala na nmaombi nayaelekeza kwa Mungu anyuooshe mkono wake na kuamsha fahamu za baba, amen

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wakuu naomba kuwasalim, naomba msaada na faraja zenu pia maombi, baba yangu alipata ajali ya kugongwa na pikipiki, hajaweza kupata fahamu hadi sasa, nimeamua kuleta hapa jukwaani kwa kunipa faraja ndugu zangu.

Wanajamvi nashukuru kwa maombia yenu nasema asante sana! Ilahali ya baba yangu bado sio nzuri kabisa. Naomba maombi yenu yaendelee.
 
Wakuu naomba kuwasalim, naomba msaada na faraja zenu pia maombi, baba yangu alipata ajali ya kugongwa na pikipiki, hajaweza kupata fahamu hadi sasa, nimeamua kuleta hapa jukwaani kwa kunipa faraja ndugu zangu.

Father of goodness and love, hear our prayers for the sick father of a member of our JF community and for all who are in need. Amid mental and physical suffering may he find consolation in your healing presence. Show your mercy as you close wounds, cure illness, make broken bodies whole and free downcast spirits. May he find lasting health and deliverance, and so join us in thanking you for all your gifts. We ask this through the Lord Jesus who healed those who believed.
Amen.
 
MUNGU muumba wa Mbingu na Nchi,ambaye ni baba wa huruma,tena usiyeshindwa,nawe nimwingi wa rehema. Nakuomba kwa wema wako,na huruma yako mponye mtumishi wako,na wale wote wanaokutumaini wewe Baba wa Mbinguni.
Baba,mrejeshee afya yake ya awali mtumishi wako,huku ukiwatazama wale wanaohangaika juu ya afya ya mja wako.
Kwa kuwa mkono wako Baba una nguvu,uwezo na mamlaka,yote utayatimiza kwa utukufu na ukuu wa jina lako.
 
Anza mfungo maalum kwaajili yake siku tatu kavu labda maji kidogo ukijisikia vibaya!
Shindana na roho ya mauti na muombe Yesu wa Nazareti kupitia Roho Mtakatifu amponye.
Amini Yesu yule yule aliyemfufua Razaro alituhaidi kuwa sisi tutafanya makubwa zaidi tukiamini!
Damu ya Yesu imfunike mzee wetu!
 
Mkuu samilakadunda pole kwanza kwa mtihani huo.
Pili napenda kukujulisha kuwa mtegemee Mungu kwa kila jambo.
Omba sana, kama ni Muislamu au Mkristo funga angalau siku tatu huku ukisali.
Pole sana.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu naomba kuwasalim, naomba msaada na faraja zenu pia maombi, baba yangu alipata ajali ya kugongwa na pikipiki, hajaweza kupata fahamu hadi sasa, nimeamua kuleta hapa jukwaani kwa kunipa faraja ndugu zangu.

poleni sana God will show the way
 
Pole sana Mkuu namuombea Baba yako Mungu amponye ili arudie katika hali yake ya kawaida kabla ya ajali ya pikipiki. Poleni sana.
 
nawashukuru wapendwa kwa upendo na kujali kwenu kwa kunitia nguvu katika kipindi hiki kigumu, baba yangu hadi sasa anatumia oxgen machine ingawa hali ya jana na leo leo angalau anafumbua macho kwa mbali ! Mungu awabariki.
 
Pole sana kiongozi, lakini tumwamini Mungu maana yeye hufanya yawezekane yale yanayoonekana hayawezekani machoni mwa mwanadamu
 
Back
Top Bottom