Baba yangu anamtaka mchumba wangu!

Baba yangu anamtaka mchumba wangu!

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
16,976
Reaction score
13,435
Habari zenu waungwana natumai muwazima na mnaendelea na mapumziko ya usiku wa leo.

Ni hivi nina mchumba ambaye tumekubaliana nikaiarifu familia yangu kuhusu yeye leo hii baada ya sala ya Ijumaa,lakini,hamadi! ile kufika nyumbani ili niwape taarifa hizi,baba kaniita chemba na kuanza yeye kwa kuniambia afadhali nilivyokwenda kuna kitu alikuwa anataka kuniambia na akasema anampenda sana mchumba wangu huyu(jina kapuni) ila nisimwambie mama.

Basi nilishikwa na kigugumizi na mimi wala sikumwambia kuwa nimekwenda pale kwake ili nimfahamishe hilo,kwa jinsi alivyokuwa ananionesha ni dhahiri naye amempenda sana huyu mchumba wangu na anataka kutuma posa.

Je,nimwambie ya kwamba huyo msichana anayemtamani ndio mchumba wangu mtarajiwa au nifanyeje?

Nalog off
 
sasa unangoja nini kumwambia? au adi amgegede ndio umwambie
Alinichanganya kwa kuwa sikujua kama hata huyo mchumba wangu naye analijua hili ama halijui ndio nataka nikaongee naye kesho.
Nalog off
 
wewe nawe kwa story zako za kutunga zilizo jaa upuuzi unatuchosha..
hayo ni mawazo yako ingawa ya kwamba sikubaliani nawe,ila nakupa uhuru wako wa kuongea ulitakalo.
Nalog off
 
Ulipanga ufanyeje??
Kwanza nataka nimuulize huyu mchumba wangu kama mzee alishawahi kuonesha ishara zozote au walishawahi kukutana faragha,halafu ndio nataka nichukue uamuzi.
Nalog off
 
Mwache aonje tu, kwani ukibisha hakulipii mahali

Naomba kujua dini ya baba yako tafadhali, kwa sababu sisi kwetu dini yetu hairuhusu baba kutamani mkwe
 
Mwache aonje tu, kwani ukibisha hakulipii mahali

Naomba kujua dini ya baba yako tafadhali, kwa sababu sisi kwetu dini yetu hairuhusu baba kutamani mkwe
Baba yangu bado hajajua kama huyu ampendaye ndiye mchumba wangu.
Nalog off
 
Huyu mchumba hana akili yeye?

kwa maelezo ya Baba ni kwamba hajawahi kuongea naye kuhusu lolote lile ila mimi ndiye ninayetaka kumuuliza huyu mchumba wangu kama hajawahi kuongea na baba yangu kuhusu kitu chochote kile?
Nalog off
 
Mi napendekeza uende kwa yule mwingine si ulisema unao wawili? huyo mmoja muachie baba yako.
 
Back
Top Bottom