Habari zenu waungwana natumai muwazima na mnaendelea na mapumziko ya usiku wa leo.
Ni hivi nina mchumba ambaye tumekubaliana nikaiarifu familia yangu kuhusu yeye leo hii baada ya sala ya Ijumaa,lakini,hamadi! ile kufika nyumbani ili niwape taarifa hizi,baba kaniita chemba na kuanza yeye kwa kuniambia afadhali nilivyokwenda kuna kitu alikuwa anataka kuniambia na akasema anampenda sana mchumba wangu huyu(jina kapuni) ila nisimwambie mama.
Basi nilishikwa na kigugumizi na mimi wala sikumwambia kuwa nimekwenda pale kwake ili nimfahamishe hilo,kwa jinsi alivyokuwa ananionesha ni dhahiri naye amempenda sana huyu mchumba wangu na anataka kutuma posa.
Je,nimwambie ya kwamba huyo msichana anayemtamani ndio mchumba wangu mtarajiwa au nifanyeje?
Nalog off