Baba yangu ameparalyse upande mmoja na hawezi kuongea

sassy girl

Senior Member
Sep 19, 2020
112
172
Habari madoctor na waganga wauguzi wa JF

Mwenzenu nimeamka na taarifa sio nzuri kiupande wangu baba yangu ameparalyse upande mmoja na hawezi kuongea miezi mitatu nyuma alifiwa na dada yake wa pekee alipohudhuria msiba baada ya kuzika siku ya tatu yake akawa anauliza majirani hapa nini kinaendelea mbona watu wamejaa..!? ilibidi wamshangae wachache wakamuelewesha kinachoendelea baada ya wiki kuisha ilibidi arudi kwake

Wakati anasubiriwa asindikizwe stand akauliza tena swali lile lile huku akitaka kujua ile mizigo ya nani na inaenda wapi (mizigo yake alipatiwa kijijini arudi nayo mjini kama zawadi) Ndipo watu wakapata mashaka wakampeleka hospital ikabainika kuwa amepatwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu akapewa vidonge atumie na maelezo akifika dar aende hospital

Alipofika Dar akaenda hospital wakasema apatiwe vipimo ,vikabainika moyo umestuka wakampatia dawa na wakasema hzo dawa zitamsaidia na akiendelea nazo basi Tatizo Lake litaisha ,akawa anaendelea vizur alirud hali yake ya kawaida ,

Leo asubuhi amepatwa na strock mguu,mkono na kuongea haongei kiukweli nimelia na kutumia sana naandika huku moyo wangu unaumia Naombeni kujua hv mgonjwa wa kupalalyse anaweza kupona? Au tumfanyaje naombeni ushauri babangu anamiaka 55 , naombeni mnitie hata moyo
 
Pole sana mkuu. Jaribu hii.
20201016_143329.jpg
20201016_143421.jpg
 
pole sana mdogo wangu
usivunjike moyo usisikitike maradhi tumeumbiwa wanawaadamu
kwa sisi waislam tunasema MARADHI ni ibada kama zilivyo IBADA zingne
hvyo unapopatwa na maradhi au mmoja wapo wa karibu anapopatwa na maradhi kwanza unapaswa umuombe MUNGU akufanyie wepesi
na mm pia namuombea kwa MWENYEZIMUNGU amfanyie wepesi mzee wetu apate kupona kwa haraka na INSHALLAH kwa uwezo wake atapona

mamaangu alipatwa na stork akiwa na miaka 40 wakati huo
alipopatwa na hali hiyo BIBI mwenyenyumba wa jirani akashauri asipelekwe hosptari mpk asomewe DUA kwanza akaja shekhe akamsomea takrbani saa nzima kisha tukaelekea hosptari

nikajiuriza kwann asipelekwe hosptari kwanza nikaja kujua baadae 70% ya stork huusika na mambo ya kishwahiri 30 iliyobaki ndo pengne huwa ya kisekura ambapo hutegemea na historia ya mgonjwa ambapo huusishwa na umri na baadhi ya maradhi ya UZEE hasa kiharusi

Bibi jirani alisema umri mdogo sana yule kupatwa na stork ya ghafra hvyo ili hali ana historia ya magonjwa mazito
hvyo pia mjitahidi kuangaika tiba mbalimbali atapona tu
sasa ni miaka zaidi ya ishirini bi mkubwa ajawahi pata stork tena ni tiba tofauti tofauti(mbadala) au sisi Waislam tunaita tiba za KISUNNAH ndizo zilimsaidia akapona kabisaa
 
Pole sana dada, cha msingi zingatieni ushauri wa daktari, lakini pia kuna dawa pia za kawaida ambazo hutumika kuchuwa mgonjwa, hizi hupatikana kwa matabibu wetu watumiao dawa za miti shamba na baadhi ya mafuta, humu jamvini wamo na naamini watauona uzi wako watakuja na njia mbadala za kuweza kumsaidia baba apate nafuu na apone kabisa inshaallah.
 
Pole sana Mkuu..!! Stroke mara nyingi husababisha Paralysis lakini ikiwapata watu wenye Umri mkubwa mara nyingi kupona inakuwa changamoto japo Inawezekana Physiotherapy husaidia kumrudisha mtu kuwa na uwezo wa kufanya mambo ambayo alikuwa anafanya zamani so changamoto ni Healinga na reformation ya Blood vessels zilizopata shida kichwani na pia tayari mzee alikuwa na changamoto ya ishu ya moyo. Poleni sana maana Gharama za kumhandle mgonjwa wa stroke alielazwa ICU sio suala dogo...
 
Pole sana
Usife moyo
Kuugua kwake sio mwisho wa mwisha yake
Muhimu kufuata ushauri wa madaktari
Mzidishe Upendo Huruma na Faraja
Upo ushuhuda wanaishi miaka mingi tu wanachopoteza ni hali ya kujitegemea
Mungu azidi kukupa nguvu
Pole sana Mkuu
 
Kuhusika kwa ushirikina ni kwa sisi tu waafrika au ni worldwide?

Na sidhani Kama stroke Ina umri maalum, lifestyle na ulaji mbovu unaweza pelekea mtu akapata stroke kutokana na magonjwa ya moyo.
 
Pole sana kwa changamoto hii. Kuwa makini sana usije kuangukia kwenye mikono ya wauza tiba asili watakula pesa yako na tiba zao za uongo.
Mgonjiwa aendelee kuhudhuria clinic hospitali hasa mazoezi then aendelee na dawa alizoandikiwa ataimprove
 
Pole sana mdogo wangu kwa huu mtihani unaopitia, hivi kupoteza kumbukumbu ndio dementia?? Mimi naomba niongee kiukweli, chakufanya sasa hivi ni kutafuta mhudumu atakayemuhudumia hapo nyumbani, sidhani km Haya maradhi yana tiba, utapoteza hela yako bure,
 
Mimi nina baba yangu mdogo alipataga hii kitu.

Bahati nzuri yeye mwenyewe anajiweza kwa mazoezi,basi akapatiwa tiba nyingi nyingi za mitishamba na kisunna lakini akawa na slow improvement.

Bahati kipindi cha corona huu mchanganyiko wa vitunguu swaumu,pili pili,limao na tangawizi ndio ulio mpa nafuu zaidi kuliko zile za mwanzo za miti shamba.

Bado anadundika fulani lakini ni tofauti na mwanzo alikuwa hasemi na akisema humuelewi,hatembei na mkono haunyooki. Wataalam wanaweza saidia hili,kwenye huo mchanganyiko unayeyusha damu na kutanua mishipa ya damu na kyifanya ipite vizuri.Wagonjwa wengi huwa ni damu kwenye mfumo wa fahamu kuganda haswa kwenye uti wa mgongo.

kwa vile hakuna dawa nafikiri wenye ushuhuda wa huu mchanganyiko mtatoa maelezo yanayo ridhisha.
 
Back
Top Bottom