Baba Yangu Amebaka Housegirl-Mama Anataka Kuondoka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba Yangu Amebaka Housegirl-Mama Anataka Kuondoka!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chupaku, May 8, 2011.

 1. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wadau wa JF.
  Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
  Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
  Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
  Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
  Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
  Tumsaidieje mama?
  Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
  Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
  Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh ngoma nzito
   
 3. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duh pazito hapa....
  sijui hata nikushaurije,mpime housegal kama hajapata ujauzito au magonjwa,kisha umpeleke councelling....
  huyo mama yenu,mpe time kwanza apone hayo majeraha maana mazito ati,kisha nyie watoto endeleeni kumuomba abaki ingekuwa sio suala zito mngemuomba mtu mzima mmoja aongee naye,ila duh mtaanzaje? poleni sana.
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  Pepo la ngono ndilo linalo msumbua baba yenu. Jikusanyeni na wazee wa ukoo waokoe jahazi.
  Mwisho wa uovu ni aibu
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah!!Poleni sana!

  Waathirika wakuu hapo ni mama na binti wa watu.Kwanza fanyeni kuongea na huyo mtoto wa watu maana anastahili pole si kidogo.Japo aliefanya hivyo ni baba yako nisamehe kusema hivi ila mpelekeni pia hosp kuhakikisha hajapata gonjwa lolote la zinaa kabla ya kumtafutia mtaalamu wa kuongea nae just incase imemwathiri kisaikolojia!Kuhusu baba yenu naogopa kuchangia maana kwa utu uzima huo miaka 30 jela hatomaliza ila nadhani anastahili kua accountable kwa alichofanya!
   
 6. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Nilitamani kumchapa. kweli anastahili adhabu ila ipi sasa? tumeamua kutoongea naye na kaamua kwenda kunywa pombe zake. Akipata ukimwi umri huo ARVs atazimudu?
   
 7. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Housegirl kaondoka ila tunazo contacts zake bado. Hivi babu wa hivyo unaweza hata kumuacha na mjukuu kweli? AArrrgggghhh
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana ila jaribuni kutafuta watu wazima wa kuongea na wazazi wenu ni aibu kwa familia.. vile vile mchunguzeni huyo msichana wa kazi anaweza kuwa yeye ndo chanzo mpaka akabakwa sote tunajua wanaume ni kiumbe dhaifu..poleni sana ngoja nikapate kahawa narudi tena
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  MR hivi mtu anakuaje sababu ya yeye kubakwa??
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Dah mbombo ngafu hapa mpaka nimeishiwa maneno
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Chupaku nakupongeza kwa ujasiri ulioonesha kuweza face tatizo na kutaka kutafuta ufumbuzi, na personally kweli nakubaliana nawe sioni sababu ya kuwambia spouses wenu hilo jambo la aibu sana ili mradi nyie watoto mhakikishe kua wanenu wasiwe karibu nae. Pole pia na the whole issue....

  Katika issue yoote roho imeniuma saana tena saana kuhusiana na binti alobakwa, na kama baba yako kaweza kufanya hivyo at 70 (hizo ni 10 decades but baado hajajaliwa hekima). Najua roho inakuuma sana na ni baba yako ndo mana unamtafutia jinsi ya kumsaidia, utanisamehe saana because najua kiubinadamu lazima utachukizwa nikikuambia kua baba yako ni mzee, kisha pita mda wake ukifananisha na binti.

  Mama yako si weak kama unavyofikiri maana watoto tukiwa watu wazimu tuna tendacy ya ku underestimate what our parents can take or can not take. Na kama kaishi nae miaka yoote hii; ni dhahiri anajua tabia ya babako kutoka nje - ila kitu kinamuuma mama yako ni kitendo cha kusema ni binti wa humo ndani level ya mjukuu na pia kua nyie watoto mmejua. Sioni sababu ya mama yako kuhama mana hapo tayari nae ni kwake hivyo aendelee na maisha yake hapo hapo amu ignore baba yako (najua hutaki niseme hivi but to me its the best option)

  Huyo binti mngejitahidi mmpeleke hospitali kuhakikisha hajapata mimba wala maambukizi ya STDs (she deserves that, na kama hatashitaki its the least you can do)

  Nakuombea kila la kheri katika kuweza kutatua tatizo lenu.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye ipi kushitakiwa anastahili....fikiria kibabu cha jirani kikikubakia mtoto utafanya nini???Mpeni huyo binti na familia yake haki ya kupata haki!Kama hatoshtaki iwe kwa mapenzi yake na sio shinikizotoka kwenu!
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  mmmh.....hapa nimefikiria mengi nimeshindwa hata kutoa ushauri.........duh
   
 14. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kuna wasichana wanajilengesha kweli ila kwa jinsi alivyolielezea tukio lilikuwa tukio la nguvu. Basi tu kabinti kadogo kadogo, angempiga mweleka avunjike kiuno kidogo labda ndiyo ingekuwa adhabu ya kumstahili
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mtu anaejilengesha habakwi bwana....nwy ikitokea binti wa watu kapata mimba muwe tayari kumjalina kumsaidia kulea!
   
 16. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sema tu Preta. Happy Mothers Day!
   
 17. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  thx.......bado najiuliza, nitasema nikimaliza kujiuliza maswali
   
 18. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh je huyo msichana alikuwa analala hapo kwenu na je mlikuwa mnampa siku ya kutoka akatembee na kukutana na vijana wenzie?? kwa umri aliokuwa nao ni lazima damu inachemka labda alianza kuonyesha dalili, tafuteni mtu aongee na mzazi wenu asimulie ilivyokuwa, msisikilize kesi ya upande mmoja
   
 19. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Labda kalianza kumtania babu mara hivi babu mara vile aaahh babu wa watu akajisevia :evil::evil:
   
 20. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160


  Yeah. She deserves the best care in the whole world. Kwa sasa ana hasira sana. Mimi pia nina hasira sana kwa kweli I rally hope she is not pregnant na hana hayo maradhi.
  Its true wazazi wamekuwa na ups and downs zao. Ila hili jamani, aibu sana. Wanawake wote hao huko nje, na hela unazo, who rape someone?
   
Loading...