Baba wa familia

Baba wa familia

Mkuu Ntuzu naelewa sana mazin gira ya porini na najua kukutana na issue kamahizo ni jambo la kawaida kabisa haswa yale mapori yenye misitu na vichaka ya tabora huko na kigoma na biharamulo

Mkuu Safari_ni_Safari nini tena aise
 
Last edited by a moderator:
Basi tukarudi Karibu na baiskeli na mbao tukakita wale simba wamesimama tu wakituangalia! Kumbe wale simba walikua wanaogopa kusonga mbele wakiogopa vyuma vya baiskeli vinavyong'aa ya Ile sterling!

Basi tukaamua kuacha baiskeli Na mbao Hapo tukaanza Kukimbia kinyumenyume huku tukiwaangalia hao simba Maana ukiwapa mgongo ni Hatari sn!

Wale simba wakaanza kutufata, na walipokaribia baiskeli wakaikwepa wakapita pembeni then wakarudi njiani kutufukuza!

Tulikimbia sn Siku Hiyo Karibu Dakika 20 ivi huku tunawarushia zile fimbo!
 
Wakati huo tunakimbia hayo maeneo yalikua hayana miti mikubwa yalikua ni mbuga na vichaka na miti midogo!

Tukawa tunakimbia kwa style ya kulindana, hakuna kuachana na km tunageuka na kuwampa simba mgongo tunageuka na Kukimbia kwa kasi then tugeuka tena kuwaangalia simba! Tulifanya hivyo mpk tukafika kule kwa wachanaji porini na tukawa Wengi sasa na uzuri palikua na kambi ya muda Ingawa ilikua sio imara Zaidi!

Basi baada ya Hapo tukawambia washikaji Hapo uzuri kulikua na moto Hapo wamewasha basi tukachukua vigenga vya moto kuifata baiskeli na mbao na wale jamaa huku tukiwa na moto! Na tulienda tukarudi salama! Nililala huko mpk kesho ndio nikawa nakusanya mbao kuzipeleka kwenye kambi!

Ila wale simba Sijui walikuaje Maana walikua wakitufata km hawataki walikua hawakimbii kwa kasi sn! Na kitendo cha kutoachana kilitusaidia sn!
 
Kwa kifupi ndio hivyo ila tulipona na hatukuzurika kabisa!
 
"Ghafla mbaya,simba amekimbia kuti la mnazi"

"Nlikuwepo":bolt:
 
Back
Top Bottom