Mwampamba!
Unapaswa kudharauliwa na mtu yoyote makini aliyekuwa anasoma shutma zako kwenye FB wall yako na maelezo uliyo kuwa unayatoa hapa JF.
1. Ulikuwa una sema chadema ni chama cha kikanda na ukabila wakati kumbe Baba, mama yako na wewe mwenyewe mlikuwa na nafasi ndani ya chadema! Hiyo dhana na mantiki ya ukanda na ukabila inakuje?
2. Ulikuwa una mporomoshea matusi na dhihaka Dr Slaa kumbe na wewe una wazazi walioko chadema tena mama diwani! Vipi ulikuwa una watukana kama ulivyo kuwa unamtusi na kumtolea maneno ya hovyo Dr Slaa?! Kama jibu SIO wewe ni kijana mwenye tabia gani za kuigwa?!
Umeongea mengi kutafuta huruma lakini kama elimu yako imekusaidia hukutakiwa kuandika hiki "2015 nitakuwa mbunge hata kwa chama kinachoitwa kitunguu swaumu,Nia si ubunge,Nia nikuonesha ni namna gani naweza siasa zozote zile ndani ya jimbo la mbozi"
Kwa wabobezi wa mantiki watakuhumu kwa ombwe la kimantiki ndani yako lakini kwa uroho na ujinga wa kuwaona watu wa Mbozi wanaweza kukuchagua wewe tu na si mtu mwingine.
Kila jema na lenye kheri mbunge wa chama cha vitunguu swaum unaye jikaanga na mafuta yako tayari kwa kuliwa.