Baba mtarajiwa, nini natakiwa kufanya?

Usaidizi.
Nguo za mtoto zinatakiwa kufuliwa kila mara. At the same time anyonyeshe au ambembeleze, atahitajika kula kwa wakati na kupumzika.

Tafuta mtu wa kumsaidia hizo kazi.

Kukandwa.
Hili swala hua anafanyiwa na upande wa kwao kama ni yatima ujue hilo linatakiwa kuwepo.

Uwepo wako.
Mimi narudi nyumbani saa tano au sita. At that time narudi nakuta mtu anabembeleza mtoto huku anasinzia so I usually helped at night. Na kumvalisha pampers dogo.

Pia safari za kliniki. Akizaliwa baada ya siku saba mtarudi kliniki, nilidhani ni ishu ya saa moja ila ilichukua saa kumi.

Nyumba safi.
Kwakua umesema wote mko stable financially najua hili lishafanyika.

It's funny watching your kid grow. Binti yangu alizaliwa mwaka jana mwaka huu naweza hold naye convo, kuna jina halipendi now mpwa wangu akamuita 'Nyaubi' akajibu 'Nyaubi bibi yako'

I know siyo tabia nzuri but I laughed.
Nyaubi bibi yakooo... Binti ni noumaaa.

Mwambie namsalimia sanaa binti yetu
 
Yaani huwa mnadinyana tu na hamjui matokeo yake, ona sasa baba mtarajiwa hata hajui nini cha kufanya mtoto akizaliwa!!!

Jiandae kumlipia mtoto bima ya afya (watoto huwa wanapata maradhi mara kwa mara)...

Jiandae kumnunulia mtoto nguo za watoto jozi za kutosha, zile baby blankets, jiandae kununua diapers (kwa wastani mtoto mdogo huvaa diapers 8 hadi 12 kwa siku, kila baada ya masaa mawili hubadilishwa), kuna mafuta ya watoto, beseni la kuogea, mataulo mawili, wipes, maziwa ya kopo (kama maziwa ya mama hayatoshi), vichupa vya mtoto kunyonya maziwa ya kopo, vichupa vya kuhifadhia maziwa ya mama...

Nunua kipima joto kile cha digital, nunua sabuni za kufulia nguo (ziwe zile za watoto au ukishindwa ziwe za kipande, usitumie hizi jamii za kina Omo maana zina harufu kali kwa mtoto na nyingine huleta aleji ya ngozi), usihangaike kununua midoli kwa sababu haina msaada kwa mtoto mchanga...

Kuwa na hifadhi ya hela kwa ajili ya 'imejensi'
Nilichotaka kujua zaidi ni hivyo vikorokoro ila mambo mengine kama bima sijui nini yatakua covered 100% kwa sababu sio mimi baba yake tu, hata mama yake ana bima ya afya ya kiwango cha juu kabisa.
 
Hongera sana daddy to be, vitu vya muhimu kunzia mama kujifungua mpaka malezi ya mtoto, kuna nguo nguo za mtoto nk, ila pia ni muhimu mkapanga na mama mwenyewe na atakuadvise anahitaji vitu gani, then ukavinunua maana ana sisters, mama, ma aunt zake nk hao wote wanaweza kumuelekeza vitu muhimu vya kununua. Wewe andaa pesa tu.
 
Yaani huwa mnadinyana tu na hamjui matokeo yake, ona sasa baba mtarajiwa hata hajui nini cha kufanya mtoto akizaliwa!!!

Jiandae kumlipia mtoto bima ya afya (watoto huwa wanapata maradhi mara kwa mara)...

Jiandae kumnunulia mtoto nguo za watoto jozi za kutosha, zile baby blankets, jiandae kununua diapers (kwa wastani mtoto mdogo huvaa diapers 8 hadi 12 kwa siku, kila baada ya masaa mawili hubadilishwa), kuna mafuta ya watoto, beseni la kuogea, mataulo mawili, wipes, maziwa ya kopo (kama maziwa ya mama hayatoshi), vichupa vya mtoto kunyonya maziwa ya kopo, vichupa vya kuhifadhia maziwa ya mama...

Nunua kipima joto kile cha digital, nunua sabuni za kufulia nguo (ziwe zile za watoto au ukishindwa ziwe za kipande, usitumie hizi jamii za kina Omo maana zina harufu kali kwa mtoto na nyingine huleta aleji ya ngozi), usihangaike kununua midoli kwa sababu haina msaada kwa mtoto mchanga...

Kuwa na hifadhi ya hela kwa ajili ya 'imejensi'

Nyongeza

Kabla ya kujifungua

Kuna vifaa ya kujifungulia ataambiwa hospital.

Kanga na vitenge doti za kutosha.

Pesa ya hospital kama hana bima lakini hata Kama anayo pesa ya matumizi mengine lazima iwepo.

Andaa chumba cha mtoto vizuri, ondoa vumbi kila mahali, chumba kiwe safi sana.
 
Acha ujinga, simama kama Baba! Financially stable ndio mnyama Gani? Je kama Kuna kidume chengine ndio kinamfanya awe stable?

Ndio shida ya wanaume.
Wakiona ke anajiweza basi wanafikiri hatakiwi kutunzwa wakati hela zenyewe hazitoshi.

Ni kina Mo tu ndio wenye financial stable wengine wote fedha hazijawahi kutosha.
 
Mleta mada hauko serious kimaisha na unachokifanya ni kucheza bahati nasibu.

Kwa mfano, unawezaje kuzaa na girlfriend na kuona ufahari?
Unawezaje kumlea vyema mtoto ambaye haishi naye?
Unajisikiaje mtoto wako kulelewa na single mother?

Kuweza kukusaidia tu hapa, malezi bora ya mtoto yanategemea mambo makuu matatu;
1. Uhusiano kindoa wa wazazi.
2. Misingi ya kiimani na kijamii ya wazazi
3. Ukaribu wa wazazi kwa mtoto
 
Make sure uchungu usizidi masaa 5!! Zaidi ya hapo unaweza kosa mmoja wao au wote!! C section ndo unyama wenye 90%
 
Nilichotaka kujua zaidi ni hivyo vikorokoro ila mambo mengine kama bima sijui nini yatakua covered 100% kwa sababu sio mimi baba yake tu, hata mama yake ana bima ya afya ya kiwango cha juu kabisa.
Bima tumia yako ndio heshima ya kiumeni mtoto anatumia ubini wako kwa nini akatiwe bima ya mama? Pia hata kama mama yake ana uwezo wa kununua ndege gharama zote za kutunza mtoto anatoa baba. Utagongewa mchana kweupe kama una akili utakuwa umenielewa
 
Wakuu habari za wakati huu.

Girl Friend wangu anatarajia kujifungua ndani ya mwezi mmoja hivi ama zaidi kidogo.

Sasa kama baba mtarajiwa ni kitu gani ama maandalizi gani natakiwa kufanya kabla na baada ya kujifungua.

Girl friend wangu anaishi kwake na mimi naishi kwangu, yuko financially stable ila I want to support her kwa vitu vyote vinavyohitajika.

Naomba kujua nahitaji kuandaa nini na nini ili niweze kupanga Budget yake mapema.

Ahsante.
Epuka mpango ya kando (MYK)
 
Kama hakuna sababu ya kusafiri usisafiri, kaa na tulia na wife home maana lolote kinaweza tokea na msaada ni wewe, kama huna kipato cha uhakika weka akiba ya kutosha kwa ajili ya dharura kama itatokea, tafuta msaidizi wa nyumbani kama huna, nyakati hizi wanawake wanakuaga na msogo wakiwaza hiyo siku ya kujifungua so kaa nae, mtie moyo na sema nae habar njema. Nunu maternity bag lenye mahitaji muhim yakupokelea kichanga, mnunulie na mkeo kama maternity bra, kanga n.k
 
Back
Top Bottom