Baba Mkwe wangu ananitishia NISHAURINI


Mkuu we dini gani?
 
huu ndo ushauri wa mtu mzima mwenye ndoa yake na anayeelewa nini maana ya ndoa

Ndoa haina third part, matatizo uenu haijalishi ni makubwa kiasi gani mnatakiwa kutasolve wenyewe


After 10 years unamrudisha kwao?

Na namshangaa huyo mwanamke aliyebeba virago kwenda kwao aisee

Kaeni nuie watu wazima msolve matatizo yenu sio kukimbilia kwa wazazi mwisho mnaoshia kuwatukana kama hivyo ulivyofanya



 
Kwani tatizo haswa la NDOA yenu ni nini mkuu? inawezekana hao wakwe zako hawana kosa kwa hayo maamuzi kutokana na kutojua tatizo la NDOA YENU kaka. Kaa chini tafakari kabla haujachukua hatua na kufanya maamuzi. Haswa Kama una watoto na huyo binti. Kila mtu atakupa ushauri hapa jamvini...lakini mwisho wa siku wewe ndio Mwenye ukweli wote uliokufanya umvumilie huyo Mkeo. Maana kumvumilia mtu kwa miaka kumi ya ndoa yenye matatizo sio mchezo kaka.
 
Yani umeshindwa kusolve ako katatizo mpka ulete uku??
 
Mwanawakwetu, unanishangaza unaposema mkeo ameenda kwao, kwao ni wapi wakati ulisha mwoa! KWAO NI KULE KWA WAZAZI WAKO. HIVYO ALIKUWA SAHIHI KABISA KUKIMBILIA HUKO KWA SABABU HUKO NDIYO KWAO HALISI. INAVYOONEKANA UMEMCHOKA MKEO. UNGETAKA SULUHU NA MKEO UNGEMWITA MSHENGA ASULUHISHE, NAAMINI ASINGEELEMEA UPANDE WOWOTE. KUNA WATU WAMEKUSHAURI UTAFUTE BI MDOGO, LAKINI WASWAHILI WANASEMA " WEZA ZUNGUKA BUCHA ZOTE LAKNI NYAMA HUWA ILEILE" SULUHISHA NA MKEO USITAKE KUKUZA KUTOELEWANA. NADHANI MMEJALIWA KUPATA WATOTO. JE UKO TAYARI WATOTO WASILELEWE NA MAMA YAO? UCHUNGU WA MWANA WA KWELI ANAUJUA MAMA YAO!
 

asingekuwa na wazazi ungempeleka wapi?
 

Bila shaka huyo mwanamke ni wa degeree na zaid pole,ndoa haina supplementary jikaze komaa nae tu ndio wako
 
Heri mimi sijaoa na kwa mwendo huu kuoa ntakusikia kwenye bomba tu.

Ya nini kutafuta karaha yote hii?
 
Pole sana mkuu, miaka 10 kwa stail hiyo!!!! Kwenu washasolve kama mara tisa huo ni wastan wa kila mwaka mnasuluhishwa mara 1 ondoa zile mnazomaliza wenyewe........ Hv bado unatuambia umedumu kwenye ndoa miaka 10!!!!! Kweli?????

Practically mlishaachana siku nyingi sana...... Kuwa makini mkuu haya maudhi ndio mana wanaume tunakufa mapema sn. Tafuta mke oa nae akizingua piga chini oa mwingine na kuendelea.............
 
Kama ungekuwa ni wewe ungechukuwa hatua gani ? Miaka 10 ni mingi kwa mtoto wa kike ndani ya ndoa huku akitumika + msongo wa ndoa. kama ni mkirto unaambiwa ww + yy wote mmekuwa mwili mmoja. kama ni swala la kutafuta ushauri kwa wazazi mlitakikiwa kwenda wote.
 
Heri mimi sijaoa na kwa mwendo huu kuoa ntakusikia kwenye bomba tu.

Ya nini kutafuta karaha yote hii?
Na siku utakapohitaji kuoa hakuna atakayekutaka, maana utakuwa umekongoroka sana!
 

Umenena Mkuu! Inaonekana binti amelelewa na kufundwa vema na anajijua kama AMEOLEWA ndio maana amewafanya wazazi wa mumewe kuwa kimbilio na ndio wazazi wake! sasa hiki Kidume kisilete hadithi hapa; Mwana Kwetu jirekebishe haraka
 
Last edited by a moderator:
Nilishawaeleza twice mara ya kwanza walielewa na kumwonya na mara ya pili pia


Pamoja na kwamba kwenye maelezo yako mimi sijaona kama ulishawaeleza bado ulitakiwa uende naye na kukaa nao ili kuweka sawa hayo masharti uliyoyaweka na kuona kama yanatekelezeka!
 
Heri mimi sijaoa na kwa mwendo huu kuoa ntakusikia kwenye bomba tu.

Ya nini kutafuta karaha yote hii?

Mkuu kwa sasa ni rahisi sana kusema chochote kwa kuwa kile unachofikiria kuwa unakihitaji kwa mwanamke unakipata wakati wowote unaotaka, Kiranga hujapata kibano cha maisha na ukaona kuwa hawa watu tunawahitaji kwa kiasi gani? kama wenza katika maisha.Mwanamke ni zaidi ya unavyofikiria. Sijui umezaliwa na kulelewa katika mazingira gani? Lakini embu fikiria kama baba yako angeishi kama wewe!! leo hii kiranga ungekuwa na Kiranga??
Kutofautiana katika maisha ya ndoa sio jambo geni ni kawaida tu kila binadamu ana mapungufu yake, pale mwenzanko anapoishia we anzia hapo! jazia mapungufu yake, na maisha husonga mbele
 
Huyo ni mkeo. Hukustaili kumrudisha kwao but ulitakiwa kumpeleka kwenu coz ni wa kwenu toka pale mlipofunga ndoa. Na jina alibadili na kuitwa ubini wenu.

Keep this on mind, fanya yote ktk tofauti yako na mkeo but never kuwashirikisha wazazi and especially wakwe.
 

Ungetueleza na kosa la kumpeleka kwao ndo tungeweza kukusaidi
 
Kamchukue mkeo, wewe ni mkatoriki sawa UPENDO haupotei kama ufunguo wa gari .
Upendo -huvumilia yote.
-hauhesabu mabaya.
-hustahimili yote.
-hauhusudu.
-hautakabari.
-haujivuni.
-haukosi kua na adabu.
-hautafuti mambo yake.
-hauoni uchungu.
-haufura hii udhalimu.
-bali hufurahi pamoja na kweli.
-huamini yote.
-hutimaini yote.
-haupungui neno wakati wote bali ukwapo una bii utabatilika.

narudia tena kamchukue mkeo, kwani waswahili husema wagombanao ndio wapatanao. Kumbuka alimsaliti Yesu, lakini usishangae wapo wote kwenye kiti cha enzi.
 

hakuna kuacha huyo ni mkewako chakufanya hapo hama mbali na wazazi then tafta wazaz wengne wenyeheshma haswa wachungaj watakusaidia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…