Ni wiki imepita tangu nimrejeshe kwao wife kwa mara ya kwanza tangu tuoane miaka 10 iliyopita kutokana na kutozingatia makubaliano tunayowekeana kama couple na jeuri, ubabe pamoja na kiburi. Lengo la kumpeleka si kumfukuza bali ili wazazi wamhoji na kumshauri baada ya wazazi wangu kufanya kazi hiyo miaka zaidi ya 9. Wazazi wangu (mwanaume) wamekuwa kimbilio la mke wangu kwa zaidi ya miaka 9 hata pale mkosa anapokuwa ni yeye akiamini wao nitawasikiliza zaidi pale wanapoomba nimsamehe wife. Kwa upande mwingine hajawahi kimbilia kwao licha ya kuwa jirani na tunapoishi kwa kuona ndugu zake watamwona ameshindwa kuishi ktk ndoa. This time nimemwambia aende kwa wazazi wake na then tutaongea mambo yote pale baada ya wiki moja.
Siku mbili baada ya kufika kwao Mama yake kaanza kulaani mimi(mume) kumpa binti yao masharti ya kuishi ktk ndoa na kusema ni marufuku mimi kumpa masharti binti yao. Kwa tone hiyo hiyo siku nne baadaye baba mkwe kanipigia simu KUNITISHIA KWAMBA atamleta KWA NGUVU BINTI YAKE huku mama yake akisema nisipofungua nyumba wakati wa kumleta WATAVUNJA MLANGO WAMWINNGIZE NDANI.
Cha ajabu hawa wazazi wa binti hawajawahi niuliza tuna ugomvi gani, tometofautiana nini bali kunilaumu hata bila kunisikiliza. Hali hii inanifanya niamini kuwa ujeuri, ubabe na kiburi cha binti yao ambaye ni mke wangu kinakuzwa na hawa wazazi wake kwa kutokuwa rational.
Ndugu zangu wanachukulia huu kama udhalilishaji na vita isiyokuwa ya lazima ya ukoo na dharau kwa upande si wa ndugu zangu tu bali hata kwa mume wa binti yao.
NISAIDIENI BUSARA ZA KU REACT!!!!