Mwanakwetu,
Nimekusoma na kuwasoma washauri wako nami natamani nikupe ushauri kidogo tu.
Kwanza, hujasema ndoa yako ni ya Kimila, kiserekali,Kiislam au Kikristo.
Sasa, mimi nakupa ushauri wa ndoa ya Kikristo kwani umekaa na huyu bidada miaka 10 bila kuvuta mchuma mwingine ndani. Hii inaonesha unamheshimu sana mkeo na hilo ni zuri.
Sasa, cha ajabu ni jinsi ulivyoamua sasa kutafuta ushauri kwa yeyote atakayekuhurumia. We, kumbuka, mkeo ni wewe wala si vinginevyo. Mi nimeoa na sasa ni 40yrs. Hajawahi kwenda kwao, ugomvi haukosekani, tena nataka kukufahamisha kwamba kule kwao mimi sithubutu hata kujilinganisha, wanacho. Lakini, alinipenda, ananipenda na tunapendana.
Tumesimamia masharti yetu, kwamba atamwacha baba na mama yake nami nitamwacha baba na mama yangu nasi tutaungana na kuwa mwili mmoja.
Tutagombana lakini hakuna mtu mwingine ataingilia kati ugomvi wetu. Tutaumaliza wenyewe. Mithali moja inasema; Ndugu wakigombana, inua jembe ukalime wakipatana chukua panga ukavune. Huo ndio ukweli wa mambo. Hakuna awezaye kukupatanisha na mkeo. Ni wewe mwenyewe na yeyetu. Mnaishi pamoja tena kwa amani na furaha kuliko jinsi ambavyo ungeishi na mama yako mzazi. Fikiri, ukiugua tumbo la kuhara, mkeo atakuosha tena bila hata kinyaa lakini mama atakuangalia vibaya tu.
Kosa lako kubwa ni kwamba umewatusi wakwe zako. Ati mpokeeni mwanenu mmfundishe adabu. We ndiyo huna adabu kabisaaa. Umekaa na mtoto wa watu 10 yrs leo umrudishe kwao. Umempa mshahara na kiinua mgongo ikiwa atashindwa kupata adabu huko aendelee na biashara yanke huko huko? Mbona tunakosa heshima hivi jamani? Je huyo bidada atakurudisha lini kwenu ukafunzwe adabu na wazazi wako weyeee?
Nakushauri, nenda kule kwa wakwe zako, kaombe radhi, chukua mzigo wako uurudishe mwenyewe nyumbani kama ulivyo utoa.