Nilisubiri hata wanipigie kuniita badala yake wananitishia bila hata kujua tatizo lililotufikisha hapo? Hapo nalazimishwa kuishi na tatizo ambalo wao wangekuwa na hekima kidogo kama wazazi wangu solution ingekuwa simple. Wa kuonywa aonnywe na wakupewa pole apewe tuanze ukurasa mpya.
Mimi naomba nitofautiane kidogo na wale waliokimbilia kulaumu wazazi,kwa sababu zifuatazo:
-Kama wewe ulivyotueleza hapa juu ya kuwa mkeo ndiye mwenye matatizo katika kipindi cha
miaka kumi ya ndoa yenu,ndivyo hata yeye kwa wazazi atakuwa ameeleza juu ya ubaya wa kwako.
- Ulitakiwa kwenda na mkeo kama nia ni kutafuta kujenga ndoa yako,au otherwise iwe ulishaamua kuiua
-Umesema hapo juu kuhusu wazazi wake kukuambia uache kumpa mtoto wao masharti,tutajuaje kuwa
hayo masharti unayompa mkeo kama si chanzo cha mgogoro ndani ya ndoa yako?
Ushauri wangu kwako:
- Kwanza elewa kuwa hiyo ndoa ni ya kwako wewe na mkeo,na ninyi ndio wenye uwezo wa kuijenga
au kuibomoa,na wala si mtu mwingine yeyote nje yenu wawili.
- Ili muweze kupata suluhu ya kweli ya ndoa yenu ningewashauri kwanza kila mmoja wenu asinyooshe
kidole kwa mwenzie kuwa ndiye mkosaji,bali kila mmoja ajiangalie udhaifu alionao kama ndio chanzo
cha mgogoro wa ndoa yenu
- Tafuta nafasi nzuri kaa na mkeo mahali pasipo na vurugu mkiwa wawili tu,kisha kila mmoja aeleze
kinachomkera kwenye ndoa yenu then angalieni namna nzuri ya kuombana msamaha kwa yote
mliyokoseana na kuahidiana kuanza upya,mkiwa makini kila mmoja kutorudia kosa.
- Kuitafuta amani ni gharama ndugu zangu,na amani ya kweli ya ndoa hailetwi na wazazi wala ndugu
kwa sababu siku mnatongozana ndugu hawakuwepo mlikuwa wawili tu,hivyo suluhu na amani ya kweli
ktk ndoa inajengwa na wanandoa wenyewe.
- Mwisho mkiwa bado wawili baada ya kuelezana makosa yenu na kusameheana,mshirikisheni Mungu wenu
kwa kuomba pamoja mkiwa mmeshikana mikono kuwa Mungu awasaidie kuwapa hekima na kujua namna
nzuri ya kuishi ktk ndoa yenu."Nawaombea Mungu awasaidie"