Baba Mkwe wangu ananitishia NISHAURINI

 

.........
Huyo siyo mke...futa tena DELETE KABISA...
 

Mimi naomba nitofautiane kidogo na wale waliokimbilia kulaumu wazazi,kwa sababu zifuatazo:
-Kama wewe ulivyotueleza hapa juu ya kuwa mkeo ndiye mwenye matatizo katika kipindi cha
miaka kumi ya ndoa yenu,ndivyo hata yeye kwa wazazi atakuwa ameeleza juu ya ubaya wa kwako.

- Ulitakiwa kwenda na mkeo kama nia ni kutafuta kujenga ndoa yako,au otherwise iwe ulishaamua kuiua

-Umesema hapo juu kuhusu wazazi wake kukuambia uache kumpa mtoto wao masharti,tutajuaje kuwa
hayo masharti unayompa mkeo kama si chanzo cha mgogoro ndani ya ndoa yako?

Ushauri wangu kwako:
- Kwanza elewa kuwa hiyo ndoa ni ya kwako wewe na mkeo,na ninyi ndio wenye uwezo wa kuijenga
au kuibomoa,na wala si mtu mwingine yeyote nje yenu wawili.

- Ili muweze kupata suluhu ya kweli ya ndoa yenu ningewashauri kwanza kila mmoja wenu asinyooshe
kidole kwa mwenzie kuwa ndiye mkosaji,bali kila mmoja ajiangalie udhaifu alionao kama ndio chanzo
cha mgogoro wa ndoa yenu

- Tafuta nafasi nzuri kaa na mkeo mahali pasipo na vurugu mkiwa wawili tu,kisha kila mmoja aeleze
kinachomkera kwenye ndoa yenu then angalieni namna nzuri ya kuombana msamaha kwa yote
mliyokoseana na kuahidiana kuanza upya,mkiwa makini kila mmoja kutorudia kosa.

- Kuitafuta amani ni gharama ndugu zangu,na amani ya kweli ya ndoa hailetwi na wazazi wala ndugu
kwa sababu siku mnatongozana ndugu hawakuwepo mlikuwa wawili tu,hivyo suluhu na amani ya kweli
ktk ndoa inajengwa na wanandoa wenyewe.

- Mwisho mkiwa bado wawili baada ya kuelezana makosa yenu na kusameheana,mshirikisheni Mungu wenu
kwa kuomba pamoja mkiwa mmeshikana mikono kuwa Mungu awasaidie kuwapa hekima na kujua namna
nzuri ya kuishi ktk ndoa yenu."Nawaombea Mungu awasaidie"
 
Tunaishi as brother and sister na hataki yuko busy na kazi za ofisini hadi nyumbani, kachoka kila wakati. amepoteza sifa za kuwa mke na ana qualify kuwa mama ama dada yangu why should we stay in the same bedroom.

Sitaki kukufariji kabisa kuwa uko sahihi kumrudisha mkeo kwao,kwanza kwani alikuja kujaribu maisha kwako?
jibu ni la ila mmeoana,siamini kuwa mmeishi miaka kumi leo hii ndio uone hana sifa za kuwa mkeo, ndugu
nikushauri ushauri wa bure ambao sikulazimishi kuwa uupokee bali iko siku moja utakuja kuukumbuka utakusaidia
mkeo ambabe umeshaishi nae kwa muda wote huo ndiye mkeo hata kama ana madhaifu yake tafuta namna nzuri
ya kuyaweka sawa. Ukijidanganya kuwa umwache mkeo ukiwaza wanawake wako wengi utapata mwingine,
utakuwa unajidanganya,kwanza nyakati hizi hakuna mwanamke anaweza lea mtoto wa mwanamke mwingine,so
utatesa watoto wako tu,na mwanamke anayeingia kwenye nyumba ambayo anajua huyu jamaa ana mke haji kwa
mapenzi ila atakaa na akili kichwani kwake ya kujenga maisha ya kwake kwanza si yakwenu."Think Twice Brother:
 
Kwenye RED nafikiri ingekuwa solution na hata mimi nilitaka ikiwa vipi niwe free ili wife awe huru ku exercise tabia zake hizo kwa uhuru bila kuingiliwa. Iweje wang'ang'anize kurudi kama vile nao hawamhitaji?

Nani kamkwambia mzazi huwa hamuhitaji binti yake?!! si kweli ila binta akishaolewa si wa familia yake tena
ni wa familia aliyoolewa,otherwise ulitakiwa kumrudisha nyumbani kwenu wewe si kwao.

Mimi huwa naamini binti akishaolewa hapo kwao wazazi wanatakiwa kugawa chumba chake kwa mtoto
mwingine,sasa wewe ndugu unamrudishaje mkeo kwenye ukoo ambao alishatoka??hukutenda haki ila jeuri.
Neno la Mungu linasema atamwacha baba na mamayake na kuambatana na wewe na kuwa mwili mmoja,sasa
unapomrudisha kwao ambako alitoka miaka tisa iliyopita wewe umeona ni sahihi kweli? kuwa binadamu ndugu yangu
mfuate mkeo mkae chini myamalize,nasikitika ukisema wote ni wasomi,halafu mnarudishana kwa wazazi!!! elimu
yenu inawsaidia nini sasa' Please narudia Think Twice"
 
Pole mdogo wangu, sina yakini kama ushauri wangu utasaidia kwani tumesikia ya upande 1 bado upande wa 2(mkeo), kwa mazingira haya waweza pokea ushauri unaopendeza kwa sura ilhali unaingizwa kwenye matatzo makubwa ambayo kuchomoka kwako itakuwa ngumu au utakuwa umechelewa kuchukua hatua muafaka. 2. Kwa hatua yoyote unayopanga kuchukua fikiria majaliwa ya watoto wenu(kama wapo). 3.Kumrudisha mke kwa wazaz wake sio sawa kwani hapo umeonyesha kutawaliwa na mfumo dume. Hapo kwako(aliko olewa) ndio kwake kihalali na sio kwa wazaz wake. Je, kama ungekuwa wwe ndo mwenye makosa yeye angekurudisha kwa wazazi wako? Yumkini kwa maelezo yako we ndie mwenye nguvu kiuchumi ktk familia kuliko mkeo na ndio sababu wazo la kumrudisha kwa wazaz wake limepata msingi kichwani mwako. Fikiria kinyume chake ambapo mkeo ndie mdau mkuu kiuchumi hapo nyumbani. 3.Yawezekana mkeo amekuvumilia kuliko ulivyo mvumilia, na umekuwa ukijitahidi kumbadilisha kuliko wewe kubadilika. 4. Kitendo cha kumrudisha kwa nguvu kwa wazaz wake bila ridhaa yake wala kuwataarifu wazaz wake kwanza juu ya matatzo ya bnti yao, hapo hukutumia busara kwani huenda wange waita wote wawili au kukutana wazazi wa pande zote mbili kutafuta suluhu ya kweli.
 
 
nilichojifunza hapa ni kuwa baada ya miaka 10 mwanamke unarudishwa kwenu kama nazi koroma inavyorudishwa gengeni
 
Ukiona mtu anaingiza masuala ya mfumo dume, mwogope
 
Sijui ulitumia utaratibu ganu kumrejesha kwao, ulimpa barua? ulimwambia tu nenda? Ulimpeleka mwenyenyewe? ali....... sijui!!!!. Kwa maoni yangu ungefunga safari pamoja naye hadi kwa wazazi wake, na kwa kuwa hujawahi kufanya hivyo na yeye amekuwa akikimbilia kwa wazazi wako, basi na wewe ilikuwa zamu yako kwenda kwa wazazi wake na kuwaeleza kwa kina yale yanayojili katika ndoa yenu. Kama alikwenda peke yake, kumbuka kila mwamba ngoma ngozi huivutia kwake, hivyo alipata nafasi ya kuwaeleza yote mabaya juu yako na kuyaongezea chumvi na bizari, huku akibubujikwa na machozi ya kinafiki, nao akamwamini na kuanza kukutisha. Jitahidi basi kuwaona wakwezo uso kwa uso mkiwa pamoja na mkeo ili myazungumze, miaka 9 ni mingi ndugu yangu, kuoa tena unaweza ukatumbukia pabaya zaidi na ukazeeka kwa shida.
 

Mungu aingilie kati ndoa yako.

Nafikiri huo ubabe anaoufanya ni kutoka kwa wazazi wake. Je una watoto? kama ndiyo nahisi kama watapata tabu sana, kwa hasira uliyonayo huwezi kuona hiyo shida watakayopata, mpaka utakapokuwa umefanya maamuzi magumu. Rudi kanisani kwa mchungaji aite familia yako na yake kaeni myazungumze nina imani mtapata muafaka.
 
Hapo tatizo ni huo ujirani wa wazazi wake kama nyumba ni yako pangisha hamia sehemu ingine mbali kabisa ukiona anaendelea na vituko mteme mazima ukishindwa kumtema sababu ya watoto na kadhalika muondoe mawazoni tafuta nyumba ndogo furahia maisha
 


Pole sana mkuu. Lakini maelezo yako si yawazi kiasi cha kufanya wanajamvi kufunguka kimapana!

Mathalani, unaposema mwanamke huyo ana jeuri, kiburi na dharau ni katika mambo gani?
Tupe mazingira yenye kuonyesha mambo hayo!

Nina wasiwasi kuwa huenda huyo mwanamke ni mwanaharakati wa kutaka kutokomeza mfumo dume; mwisho wa siku unamwelewa vibaya na kumuita mwenye dharau, kiburi na jeuri.

Funguka mkuu. Nitarudi baadae.
 
Pole kaka.mi nakupongeza kwa uvumilivu na busara zako.Nakushauri uende kwa wakwe zako na kuwaeleza kwamba umemfuata mkeo,Usitake maelezo wala wewe kujadili kitu pale ili uone watasemaje.wakikupa nenda nae kwako usimwulize kitu.kesho yake mpeleke kwa wazazi wako akae huko kama wiki kwamba utakwenda mzungumze huko.ukienda baada ya wiki wambie nafuata mke wangu pia usitake mazungumzo na nyumbani usizungumzie hayo tena.uone atabadilika au la!
 
 
Kabla ya yote tuambie ni masharti yepi uliyompa huyo bi shemeji?
 
Mwanakwetu,
Nimekusoma na kuwasoma washauri wako nami natamani nikupe ushauri kidogo tu.
Kwanza, hujasema ndoa yako ni ya Kimila, kiserekali,Kiislam au Kikristo.
Sasa, mimi nakupa ushauri wa ndoa ya Kikristo kwani umekaa na huyu bidada miaka 10 bila kuvuta mchuma mwingine ndani. Hii inaonesha unamheshimu sana mkeo na hilo ni zuri.
Sasa, cha ajabu ni jinsi ulivyoamua sasa kutafuta ushauri kwa yeyote atakayekuhurumia. We, kumbuka, mkeo ni wewe wala si vinginevyo. Mi nimeoa na sasa ni 40yrs. Hajawahi kwenda kwao, ugomvi haukosekani, tena nataka kukufahamisha kwamba kule kwao mimi sithubutu hata kujilinganisha, wanacho. Lakini, alinipenda, ananipenda na tunapendana.
Tumesimamia masharti yetu, kwamba atamwacha baba na mama yake nami nitamwacha baba na mama yangu nasi tutaungana na kuwa mwili mmoja.
Tutagombana lakini hakuna mtu mwingine ataingilia kati ugomvi wetu. Tutaumaliza wenyewe. Mithali moja inasema; Ndugu wakigombana, inua jembe ukalime wakipatana chukua panga ukavune. Huo ndio ukweli wa mambo. Hakuna awezaye kukupatanisha na mkeo. Ni wewe mwenyewe na yeyetu. Mnaishi pamoja tena kwa amani na furaha kuliko jinsi ambavyo ungeishi na mama yako mzazi. Fikiri, ukiugua tumbo la kuhara, mkeo atakuosha tena bila hata kinyaa lakini mama atakuangalia vibaya tu.
Kosa lako kubwa ni kwamba umewatusi wakwe zako. Ati mpokeeni mwanenu mmfundishe adabu. We ndiyo huna adabu kabisaaa. Umekaa na mtoto wa watu 10 yrs leo umrudishe kwao. Umempa mshahara na kiinua mgongo ikiwa atashindwa kupata adabu huko aendelee na biashara yanke huko huko? Mbona tunakosa heshima hivi jamani? Je huyo bidada atakurudisha lini kwenu ukafunzwe adabu na wazazi wako weyeee?
Nakushauri, nenda kule kwa wakwe zako, kaombe radhi, chukua mzigo wako uurudishe mwenyewe nyumbani kama ulivyo utoa.
 

What a good advice !
Be blessed.
Mwana kwetu chukua ushauri huu.
 
Kiukweli ndugu unabusara sana. Wengine twajifahamu ningekutana na wazazi kauzu namna hiyo ningewasubiri sana kwa hamu..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…