Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 347
Jamani, nimejitokeza sana hapa. Kabla sijaendelea na kisa hiki, naomba nikuulize swali- Je unaamini kwamba uchawi upo? Mwenzenu imenibidi niamini tu pamoja na kashule kangu kadogo nilikokasotea pale Mlimani, na vyuo vingine. Ni hivi. Tangu tupate mtoto wetu wa kwanza miaka 5 iliyopita, amekuwa akiumwa kila siku. Kama ni hospitali zote za nguvu hapa amepita kwa kulazwa na si mara moja. Wazazi na mtoto wote hatuna ugonjwa wa kisasa. Ugonjwa huo wa ajabu, unamfanya mtoto apoteze fahamu.
Kwa kifupi, hospitali walishindwa. Nikaamua kusafiri zangu mwaka jana baada ya ushauri kwa rafiki yangu anaetoka Nyanda za Juu Kusini! Tukaenda nae kwao. Tulipita kwa watu tofauti wanne tena wanaishi umbali wa kilo mita karibu 60 au 70 kutoka kwa mwingine. Kila tulipofika tu bila kueleza chochote, walisema - "Mmeleta shida ya mtoto huyu". Kila mmoja wa "watalaam hao" alimtaja baba mkwe kwamba yeye ndo chanzo cha matatizo ya mtoto wetu.
Sikuamini moja kwa moja. Nilipata safari ya kikazi ya kwenda hapo Kigoma, nikambeba mtoto pia, nako nikaambiwa yale yale yanayofanana na wale wa Nyanda za Juu kusini (Mbeya na Rukwa).
Cha ajabu, mtoto akiumwa, baba mkwe anakuwa wa kwanza kufika hosp, na kutoa ushauri wake. Tena anahuruma sana, wakati mwingine huwa anaomba kukaa na mtoto karibu mwezi mzima! Kumbe kupindi mtoto akilazwa yeye ndo furaha yake!
Ni kweli nasalimiana nae, nacheka nae, ila namjua kwamba ni mbaya wangu. Hadi leo mtoto hawezi hata kuembea. Amenitia hofu ya kupata hata mtoto wa pili. Mke wangu tumeonge nae sana, nae anasema anamjua baba yake ila hakujua kwamba anaweza kuwa mbaya kiasi hicho! Jamani kuoa tuwe tunauliza, hasa tunaooa hapa Salidalama! Tunakutana tu kwenye daladala au kwenye FB!
Nikimuona baba mkwe, moyo wangu unakuwa mweusi sana! Sijui nifanyeje....