Baba mkwe ndo mchawi wa mtoto wetu

Baba mkwe ndo mchawi wa mtoto wetu

Biblia huandika ya kwamba, amelaaniwa mtu yule mwenye kumtegemea mwanadamu...

Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

. Umemaliza mkuu

Mwenye masikio na asikie

Jamaa badala ya kumuomba Mungu uponyako na kutafuta maspecialist kajikita kwenye nguvu za giza, sijui hajui ibilisi ni mchonganishi na muharibifu? Subiri siku aambiwe mama yake anataka kumla nyama ndo akiki itamkaa sawa
 
[b said:
AMPELEKE AKAOMBEWE ATAPONA KWA IMANI[/b],PIA AMWAMBIE HUYO BABA MTOTO WANGU AKIFA ATAMLA NYAMA PIGA BIT
hapo juu tupo pamoja na nimekuunga mkono,ila hapo red,mhhh....majanga!!!Kwani akimla ndo itatokea nn au itakuwaje?
Mtegemee yesu atamponya mwanao na ww pia?
 
Jamani, nimejitokeza sana hapa. Kabla sijaendelea na kisa hiki, naomba nikuulize swali- Je unaamini kwamba uchawi upo? Mwenzenu imenibidi niamini tu pamoja na kashule kangu kadogo nilikokasotea pale Mlimani, na vyuo vingine. Ni hivi. Tangu tupate mtoto wetu wa kwanza miaka 5 iliyopita, amekuwa akiumwa kila siku. Kama ni hospitali zote za nguvu hapa amepita kwa kulazwa na si mara moja. Wazazi na mtoto wote hatuna ugonjwa wa kisasa. Ugonjwa huo wa ajabu, unamfanya mtoto apoteze fahamu.

Kwa kifupi, hospitali walishindwa. Nikaamua kusafiri zangu mwaka jana baada ya ushauri kwa rafiki yangu anaetoka Nyanda za Juu Kusini! Tukaenda nae kwao. Tulipita kwa watu tofauti wanne tena wanaishi umbali wa kilo mita karibu 60 au 70 kutoka kwa mwingine. Kila tulipofika tu bila kueleza chochote, walisema - "Mmeleta shida ya mtoto huyu". Kila mmoja wa "watalaam hao" alimtaja baba mkwe kwamba yeye ndo chanzo cha matatizo ya mtoto wetu.

Sikuamini moja kwa moja. Nilipata safari ya kikazi ya kwenda hapo Kigoma, nikambeba mtoto pia, nako nikaambiwa yale yale yanayofanana na wale wa Nyanda za Juu kusini (Mbeya na Rukwa).

Cha ajabu, mtoto akiumwa, baba mkwe anakuwa wa kwanza kufika hosp, na kutoa ushauri wake. Tena anahuruma sana, wakati mwingine huwa anaomba kukaa na mtoto karibu mwezi mzima! Kumbe kupindi mtoto akilazwa yeye ndo furaha yake!

Ni kweli nasalimiana nae, nacheka nae, ila namjua kwamba ni mbaya wangu. Hadi leo mtoto hawezi hata kuembea. Amenitia hofu ya kupata hata mtoto wa pili. Mke wangu tumeonge nae sana, nae anasema anamjua baba yake ila hakujua kwamba anaweza kuwa mbaya kiasi hicho! Jamani kuoa tuwe tunauliza, hasa tunaooa hapa Salidalama! Tunakutana tu kwenye daladala au kwenye FB!

Nikimuona baba mkwe, moyo wangu unakuwa mweusi sana! Sijui nifanyeje....

Mkuu tangaza vita sasa dhidi ya uchawi hapo ndani kwako. Kabidhi maisha yako kwa Yesu Kristo naye atajishughulisha na watesi wako. Huo uchawi ndo ushaanza nyumbani kwako na dawa pekee ni wewe kujisalimisha. Huyo mtoto atatembea na hakuna baya litakalokujia tena (only and if only you surrender your life unto Jesus)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Alafu hawa wanaojishauwa yesu ni jibu ndio wa kwanza kupanga folenu kwa waganga kwendenu zenu na ngozi za uongo mlizojivisha
 
Jamani, nimejitokeza sana hapa. Kabla sijaendelea na kisa hiki, naomba nikuulize swali- Je unaamini kwamba uchawi upo? Mwenzenu imenibidi niamini tu pamoja na kashule kangu kadogo nilikokasotea pale Mlimani, na vyuo vingine. Ni hivi. Tangu tupate mtoto wetu wa kwanza miaka 5 iliyopita, amekuwa akiumwa kila siku. Kama ni hospitali zote za nguvu hapa amepita kwa kulazwa na si mara moja. Wazazi na mtoto wote hatuna ugonjwa wa kisasa. Ugonjwa huo wa ajabu, unamfanya mtoto apoteze fahamu.

Kwa kifupi, hospitali walishindwa. Nikaamua kusafiri zangu mwaka jana baada ya ushauri kwa rafiki yangu anaetoka Nyanda za Juu Kusini! Tukaenda nae kwao. Tulipita kwa watu tofauti wanne tena wanaishi umbali wa kilo mita karibu 60 au 70 kutoka kwa mwingine. Kila tulipofika tu bila kueleza chochote, walisema - "Mmeleta shida ya mtoto huyu". Kila mmoja wa "watalaam hao" alimtaja baba mkwe kwamba yeye ndo chanzo cha matatizo ya mtoto wetu.

Sikuamini moja kwa moja. Nilipata safari ya kikazi ya kwenda hapo Kigoma, nikambeba mtoto pia, nako nikaambiwa yale yale yanayofanana na wale wa Nyanda za Juu kusini (Mbeya na Rukwa).

Cha ajabu, mtoto akiumwa, baba mkwe anakuwa wa kwanza kufika hosp, na kutoa ushauri wake. Tena anahuruma sana, wakati mwingine huwa anaomba kukaa na mtoto karibu mwezi mzima! Kumbe kupindi mtoto akilazwa yeye ndo furaha yake!

Ni kweli nasalimiana nae, nacheka nae, ila namjua kwamba ni mbaya wangu. Hadi leo mtoto hawezi hata kuembea. Amenitia hofu ya kupata hata mtoto wa pili. Mke wangu tumeonge nae sana, nae anasema anamjua baba yake ila hakujua kwamba anaweza kuwa mbaya kiasi hicho! Jamani kuoa tuwe tunauliza, hasa tunaooa hapa Salidalama! Tunakutana tu kwenye daladala au kwenye FB!

Nikimuona baba mkwe, moyo wangu unakuwa mweusi sana! Sijui nifanyeje....

naamin unadini xo imani yko itakuponya nenda mskitin ama kanisni ukiamin mtot akiaombewa lazma apone afu utaona miujiza ya mungu
 
Wewh mtoto!
Back to sender tena? Aisee!
YESU NI JIBU!!!!!!!!!!!!!!!!!! Sali zaburi ya 35 na onana na padri/pastor utaona maajabu ya bwana! Uimpa BACK TO SENDER MOJA harudii tena.

Mimi akienitenda kunilaza bedrest mwezi mzima nimempa BACK TO SENDER nae yuko bedrest wiki 2, hoi an apata dripu double double! Nae mwezi kitandani utamhusu!

Akishanena kwa lughaa akaachia BACK TO SENDER!!!!!!!!!!!Game over!
 
Hebu jaribu kumkabidhi mikononi mwa Mungu kwanza kwa sala na maombi kwa imani,,,,,,,,, hakika naye atakujibu siku na saa usiyotarajia, usikate tamaa Mungu wetu ni mwaminifu!!!!!!!!
 
hapo muende mkapate msaada wa kiroho kutoka kwa mchungaji au padri, ila nikutahadharishe kidogo ,kama aliyesabisha ugonjwa huo ni "mwanga" tu basi hamtapata tabu,ila kama ni mchawi hapo mjiandae kusimama ki-imani,maana ni vita mmeitangaza na mjiandae kushambuliwa zaidi
 
ajue tu kwamba umejua yeye ndio chanzo ,ngoja nikusimulie kitu nilipomaliza chuo sikutafuta ajira nikajiajiri huko upanga -mazengonilikuwa na biashara yangu ilikuwa inalipa sana sasa mhindi mmja akafungua na yeye vimbwanga vikaanza hapo leo dawa mlangoni kesho kishimo hella ikaanza kupotea na kupotea biashara ikaniendea vibaya renew capita na wewe sasa alikuwa amezoea natumia gari fulani siku hiyo nikaja na gari nyingine tena tinted nikamsubiria wee kama 3hrs kweli akaja akakaa pale mlangoni akaanza kuchimba nikashuka paaaaap nilimlamba makofi nikamjazia na watu pale nikamchamba kisawasawa nakuhakikishia hakuendelea kunichawia haya mambo usiyaogope mpe laive.
ila kwa huyu AMPELEKE AKAOMBEWE ATAPONA KWA IMANI ,PIA AMWAMBIE HUYO BABA MTOTO WANGU AKIFA ATAMLA NYAMA PIGA BIT
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta lakini pia hongera sana kwa ujasiri wako. Ila tatizo nililoliona hapa ni kwamba ni scenario mbili tofauti..at least wewe ulimuhisi huyo muhindi na ukamvizia na kwa bahati ukampata. Ila sasa huyu ndugu kasikia tu kwa kuambiwa na hao waganga!! Ushahidi hana tofauti na wewe ulivyomkamata akipiga tukio. Suluhu hapa ndugu arudi kwa Yesu maana hakika hakuna kisichowezekana machoni pake!!!! Na pia kumwambia ukweli mbaya wake ni vizuri kama angekuwa kaonyeshwa nani mbaya wake kwa namna yoyote ile na Mungu wake (ni suala la kiimani zaidi). Ni hayo tu.
 
Uzi huu umenifanya nijiulize, hivi tunajua hata tunaloamini katika hizi dini zetu?
 
Yesu ndio jibu mkabidhi shida zako yeye kweli hayo mambo yapo lakini usipomwendea yeye hutafanikiwa pole sana
 
Kwanza umekwenda hospital zip na zip, pili mtoto anazimia tu au anapata degedege, tatu wakati wakujifungua mkeo alipata shida yeyote na je alilia vizuri na sasa hivi ana umri gani mtoto na anafanya nini sasa. Yaani anakaa au anasimama
 
Fanya faster kwa maunyau au kwa yahya hussein achen unafk kila mtu yesu yesu anaweza kwenda kwa yesu huku hana iman?hata yesu mwenyewe alisema kwa yule kipofu imani yako imekuponya.mkuu nenda kule unakoamin
 
Ulipoenda kwa hao waganga woote Mtoto alipona?
Kama hakupona kwa nini? Walisemaje?
 
Nikuweke sawa tu kwamba mtoto wangu anao ma specialist both at Muhimbili and Aga Khan. Nikutajie hapa baadhi yao. Muhimbili yuko Dr. Massawe, ambae pia ana clinic pale Morocco. Aga Khan yupo Dr. Lakhan na Dr. Guboja. Amwewahi pia kuangaliwa na ma specilist wa pale Masaki mara kibao (Doctors without Boarders). Amepima vipimo vya ubongo na moyo. Kama ni kusali, tumempeleka kwa wachungaji na pia kuombewa na wahubiri mashuhuri. Tunapeleka hata nguo zake kwenda kuombewa.
Ni kweli nimechanganya vitu, fine, lakini, kwanini Baba Mkwe ndo apatikane na watu wasiomjua? Tena wengine walikua wanatuonesha kwenye kioo! Kwa nini mke wangu aseme hivi "Najua Baba mbaya lakini sijui kama anaweza kutufanyia hivi".....

. Umemaliza mkuu

Mwenye masikio na asikie

Jamaa badala ya kumuomba Mungu uponyako na kutafuta maspecialist kajikita kwenye nguvu za giza, sijui hajui ibilisi ni mchonganishi na muharibifu? Subiri siku aambiwe mama yake anataka kumla nyama ndo akiki itamkaa sawa
 
Ulipoenda kwa hao waganga woote Mtoto alipona?
Kama hakupona kwa nini? Walisemaje?

Tangu March mwaka huu, hali yanke imebadilika. Ameumwa mara moja tu na hapotezi tena fahamu.
 
Nakumbuka kuna siku nilimtazama hadi machozi yalinitoka, aliinamisha kichwa chini tu bila kusema kitu. Kweli ananikosea sana. Mama mkwe hana tatizo lolote. Tatizo ni huyu baba.

Hapa bado hujanisaidia sana, naomba ushauri. Ni kweli nakuelewa na kusali nasali pia, tena sana. Ila ilinibidi niache kwa muda nishughulikie swala la mtoto.
Pole sana mkuu Wiyelele, kwa hakika hakuna kitu kinauma kama mtoto kuumwa aisee. Niliuguliwa mtoto mimi nilikuwa nalia kila siku ninavyomuona anateseka. Yaani nilihangaika naye katika hospitali kubwa kumbwa zote za Dar. CCBRT, Regency, hizi temeke, amana kulikuwa kama kwetu. Tukamwona Dr. wa watoto sijui yupo mmoja anaitwa Koya, tukaenda kwa mwingine huko Sinza, lakini hakuna ambako mtoto alipata unafuu. Tukampeleka kwenye maombi, hakuna kitu. Baadaye tukapewa tu taarifa, (japo hatukwenda kwa mganga) kwamba kuna jirani yetu anayetufanyia hivyo. Halafu kama vile ni coincidence, huyo jirani alikuwa akija tu home, mtoto anamkimbia, hilo likatuongezea imani kwamba inawezekana jirani anahusika.

Lakini siku isiyo na jina alizidiwa, tukatoka naye kwenda hospitali ya kawaida tu, ndogo kabisa ya binafsi inaitwa Cardinal Rugambwa pale ukonga. Tukakutana na mama ambaye alimwangalia mtoto kwa muda mrefu, akatafakari kwa muda mrefu. Akatuuliza maswali mengi kuhusu hali ya mtoto, akamwandikia afanyiwe vipimo kadha wa kadha, na kutuandikia dawa ambayo pale hospitali haikuwepo, tulikwenda kununua pharmacy kwa gharama kubwa kiasi. Lakini huwezi amini katika muda wa siku tatu tu, mtoto alikuwa ameshaanza kupata nafuu. Na tangu amalize ile dozi hajawahi tena kupata homa ya aina ile.

Ninachoweza kusema hapa, ni kwamba usikate tamaa, na angalia sana usije kujikuta unajenga uadui na huyo baba mkwe halafu siku ya siku ukaja kugundua kwamba hahusiki kwa lolote. Itakuwa ni aibu sana. Mimi baada ya mwanangu kufanyiwa vipimo na kupona, nilianza kumwonea aibu yule jirani, japo sikuwahi kumuuliza. Linapokuja suala la imani za ushirikina kwa kweli linatakiwa lichukuliwe kwa uangalifu mkubwa sana. Ni bora uendelee kuhangaika huku na kule kutafuta suluhu. Ikiwezekana mpeleke kwenye maombi pia. lakini pia kama huko ulikoenda waliweza kujua kama baba mkwe ndiye anayemsumbua mtoto kwanini hawakumtibu mtoto na kumkinga na huo uchawi wa baba mkwe?

Mimi nafikiri kwa sasa punguza hiyo imani ya uchawi kwa kuwa itakuharibia mahusiano yako na watu wengine ambao yumkini hawahusiki kabisa. Lakini pia hali ya huyu mtoto uliyenaye sasa isikukatishe tamaa kupata mtoto mwingine, maana hujui kama ugonjwa wake ni wa kuzaliwa nao au ni acquired. So usimfundishe Mungu kuhusu afya za watoto wako.
 
Kwanza umekwenda hospital zip na zip, pili mtoto anazimia tu au anapata degedege, tatu wakati wakujifungua mkeo alipata shida yeyote na je alilia vizuri na sasa hivi ana umri gani mtoto na anafanya nini sasa. Yaani anakaa au anasimama

Mtoto alizaliwa vizuri tu. Anatibiwa Muhimbili na Aga Khan.
 
Back
Top Bottom