Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,578
- 28,701
Peleka kanisani tu huyo mtoto wapige maombi mbona kitamnukia huyo baba mkwe...
Pole sana mkuu Wiyelele, kwa hakika hakuna kitu kinauma kama mtoto kuumwa aisee. Niliuguliwa mtoto mimi nilikuwa nalia kila siku ninavyomuona anateseka. Yaani nilihangaika naye katika hospitali kubwa kumbwa zote za Dar. CCBRT, Regency, hizi temeke, amana kulikuwa kama kwetu. Tukamwona Dr. wa watoto sijui yupo mmoja anaitwa Koya, tukaenda kwa mwingine huko Sinza, lakini hakuna ambako mtoto alipata unafuu. Tukampeleka kwenye maombi, hakuna kitu. Baadaye tukapewa tu taarifa, (japo hatukwenda kwa mganga) kwamba kuna jirani yetu anayetufanyia hivyo. Halafu kama vile ni coincidence, huyo jirani alikuwa akija tu home, mtoto anamkimbia, hilo likatuongezea imani kwamba inawezekana jirani anahusika.
Lakini siku isiyo na jina alizidiwa, tukatoka naye kwenda hospitali ya kawaida tu, ndogo kabisa ya binafsi inaitwa Cardinal Rugambwa pale ukonga. Tukakutana na mama ambaye alimwangalia mtoto kwa muda mrefu, akatafakari kwa muda mrefu. Akatuuliza maswali mengi kuhusu hali ya mtoto, akamwandikia afanyiwe vipimo kadha wa kadha, na kutuandikia dawa ambayo pale hospitali haikuwepo, tulikwenda kununua pharmacy kwa gharama kubwa kiasi. Lakini huwezi amini katika muda wa siku tatu tu, mtoto alikuwa ameshaanza kupata nafuu. Na tangu amalize ile dozi hajawahi tena kupata homa ya aina ile.
Ninachoweza kusema hapa, ni kwamba usikate tamaa, na angalia sana usije kujikuta unajenga uadui na huyo baba mkwe halafu siku ya siku ukaja kugundua kwamba hahusiki kwa lolote. Itakuwa ni aibu sana. Mimi baada ya mwanangu kufanyiwa vipimo na kupona, nilianza kumwonea aibu yule jirani, japo sikuwahi kumuuliza. Linapokuja suala la imani za ushirikina kwa kweli linatakiwa lichukuliwe kwa uangalifu mkubwa sana. Ni bora uendelee kuhangaika huku na kule kutafuta suluhu. Ikiwezekana mpeleke kwenye maombi pia. lakini pia kama huko ulikoenda waliweza kujua kama baba mkwe ndiye anayemsumbua mtoto kwanini hawakumtibu mtoto na kumkinga na huo uchawi wa baba mkwe?
Mimi nafikiri kwa sasa punguza hiyo imani ya uchawi kwa kuwa itakuharibia mahusiano yako na watu wengine ambao yumkini hawahusiki kabisa. Lakini pia hali ya huyu mtoto uliyenaye sasa isikukatishe tamaa kupata mtoto mwingine, maana hujui kama ugonjwa wake ni wa kuzaliwa nao au ni acquired. So usimfundishe Mungu kuhusu afya za watoto wako.
Kwa imani yangu, hakuna nguvu ya uchawi inayoweza kuyashinda maombi. Mpeleke kanisani akaombewe kabla hujaamua kuwatumia hao waganga kwa ajili ya kinga. Lakini pia huna sababu ya kumchukia baba mkwe wako, kama hao waganga wana uwezo wa kukupa dawa za kumuokoa mtoto, wewe mtibu mtoto na baba mkwe endelea kumpenda na kumjali kama kawaida.
mleta mada samahani, naona na wewe mwenyewe tayari ushatengenezwa na huyo Baba Mkwe. Ni kama hujielewi na huna mpango wa kuchomoka kwenye janga hadi upoteze mtoto.
DO SOMETHING MAN, GET OUT OF THAT SHIT!
TOKA!!!
TOKA!!!
Nasema TOKA kwenye minyororo ilifunga akili zako.
Wiyelele TOKAA !!!
TOKA umuokoe mtoto wako.
+ zaburi 109Soma zaburi ya 35 utaona jinsi inavosisitiza wewe msomaji kumuomba Bwana wa Majeshi aingilie kati.
Unakumbuka neon linasema waombeeni adui zenu? ........... lakini haisemi tuwaombee nini... aisee kuna silaha kibao za vita aisee, upanga, mawe ya barafu, moto, mshale, rungu yaani hivi vyote ukivitumia katika ulimwengu wa roho mbona utasikia habari yake huyo mbaba. ........... Dawa ya wachawi ni kuamka saa sita usiku na kusali maana huo ndio muda wao wa kufanya uchawi wao. Na unaposali sio unalia lia haya ni maombi ya vita.