Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Baba mkwe, mahari hii imenishinda

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,491
Reaction score
2,563
Leo week ya pili nimeshindwa kabisa kupokea simu ya Baba mkwe na Mshenga wangu.

Iko hivi katika misoto yangu na kukulu kakala za maisha atimae nikajikuta nimedondokea kwa mtoto wa kichaga Kama ilivyo janga kwa wanaume wengi wa mjini.

Mipango ikapangwa na siku ya kufika ukweni kupeleka posa ikafika. Kidume nikajikoki na Mshenga wangu na wadada 3 wa kukodi tukazuka ukweni.

Mambo yalikua shwari hadi pale mjomba mtu akapewa fursa ya kutupangia package ya mahari ili mpango mzima ukamilike.... list ya makorokoro kibao, Mara mkaja wa mama, Bibi, mablanket ya Mama na mashangazi, mbege mapipa matatu, mbuzi 3 wa maziwa na....mwishoni akataja cash money 3 Mil.

Mimi kipindi anataja yale mazaga hata nilikua sifuatilia ,akili yote ilikua inasubiri point ya msingi Cash money.

Badae ikatolewa option ya ku convert the overall cost ika amount Kama 5 Mil. na ushee!

Jitihada za mshenga kupangua bei hazikuzaa matunda. Mbaya zaidi ile tumemaliza events shangazi anatuzuia hakuna kuondoka mpaka tumelipia gharama za maandalizi walioyotufanyia.

Kwa shingo upande nikausukuma mzigo wa M pesa tsh 280, 000 coz walidai laki 3.

Niliporudi lodge usiku mzima sikulala , series nzima ikawa inaji frash back repetitively.

Nika najiuliza kwani wananiuzia mke kisa ni afisa ustawi wa jamii?

Ana kipi Cha ziada ambacho wake wa ndg zangu wameolewa na jumla ya mahari tulizotoa na makokoro yote hata milioni haikufika?

Kwani ana kismat Cha mafanikio? Mbona tangu tuingie kwenye relationship mambo mengi tunakimbizana kwa had-hoc za kufa mtu?

Na mengine mengi ambayo si busara kuyaanika humu.

Alifajiri nikaamua kufanya maamuzi magumu ..."Katu sitorudi tena ukweni." Kwa maana kuwa sitoi tena mahari, mtoto wao nimeshamtia mimba ,wakimtaka waje wamchukue.

Ni hayo tu.....sirudi ukweni tena

Mashemeji zangu wachaga povu ruksa. Ila katu sirudi tena ukweni.
 
Mkuu hiyo 280K mbona huku kwetu unapata mke kabisa. Wewe ndio umefanya ya kula ka sahani 1 ya wali maji ya kilimanjaro na kipapatio cha kuku! Duh..pole sana..waachie wenyewe kwa wenyewe.
By the way % kubwa ya mabinti zao hawana mpya 6X6!
 
Mahari ya milioni 5? Uchagani sehemu gani? Kwanza sisi wachaga tunaamini mahari haishii utalipa mpaka uzeeni.

Labda mshenga wako hakuelewa utaratibu kuna vitu vya muhimu vya kulipa katika mahari ya awali havizidi laki 8.

Vinavyobaki kama mifugo utalipa unavyojisikia mpaka uzeeni.
Pwenti.....................
 
Dah poa braza tunaheshimu maamuzi yako, usirudi tu ukweni, sio sababu ya mahari kubwa ila kuombwa kurudisha gharama ya tafrija ile sio sawa kabisa maana we hukuwaambia waandae tafrija ila ni wao kama wao
 
Mahari ni kikwazo kikubwa sana siku kwa sisi vijana.

Utajiuliza kuwa baada ya mahari hakutakuwa na harusi au maisha ya ndoa?

Je hujaisaidia hiyo familia kumchukua Binti yao na kuishi naye?

Je undugu hatakuwepo kati ya kwao Binti na kwenu katika kusaidiana kimaisha?

Wazazi wanapaswa wajifunze na kujisahihisha la sivyo wataendelea kuongeza idadi za ma-single mothers kila siku.

Mleta mada uko sahihi kabisa 100%.
 
Usihof watajileta tu na bei itashuka

Maish yenyew chenga hya utatoa mahar 5mil bdo harus watajikuta wanatka kubwa another 5mil inakutoka

Au wamekunyima makusud ili usirud wakaona mahar kubwa hyu harud hpa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom