Baba mkwe anataka nimpe talaka mwanaye ili tugawe mali. Mama mkwe anaenda kwa waganga aniue ili mwanaye arithi mali zangu

Bixente naona una mtazamo kama wangu.. kuna mmama wa JF huko juu kacomment kwamba ikiwezekna umuachie mali mwanamke we kaanze upya..huyu mmama anazeeka vibaya sana sijui kama angekua mtoto wake wa kiume angemshauri hivyo?

Uchungu wa kumsomesha tangu kindergaten Primary Secondary Chuo hadi uchungu wa mwanae kutafuta mali hausikii?

huyu mama hana mtoto kama anae basi kapata bahati mbaya.
Kylian niamini mimi humu JF wengi ni wanafiki, ushauri wanaoutoa kwenye mada mbali mbali ni tofauti kabisa na ambavyo wange react wao ikiwa kama wao ndio wangekuwa kwenye situation husika.


Tena kama hao wanawake ndio wanafiki sana, naamini kabisa angekuwa kijana wake ndio yuko kwenye hii situation asingempa huo ushauri mwanae hata kidogo tena kuna uwezekano na yeye angeuvaa huo ugomvi hili kuhakikisha mali za mwanae haziondoki.

Jambo kama alikuhusu unalichukulia rahisi rahisi tu na hata ushauri unaoutoa unakuwaga ni rahisi rahisi tu.
 
Sijaoa, lakini haikustairi kuja kuomba ushauri. Ulitakiwa uje na matokeo ya maamuzi ya kiume. Kwamba umemtimua mkeo na kujitafutia ulinzi *shirikishi*
 
Na mimi naomba nkushauri tu, Mpe kila kitu kuanzia Talaka mpaka mali, Anza upya kupitia njia ya kwanza ulioitumia kupata Mali hii anayoitak yeye
Nakwambia hivyo kwa sababu nina ndg yangu wife wake nae alifanya kama hivyo hivyo,na jamaa alimpa kila kitu maan alidanganywa kwamba hadi watoto nao aondoke nao ili jamaa aendelee kuhudumia na Mali ameshampa,Ninavyokwambia hadi sasa hv nauli ya kumtoa huyo wife wa ndg yetu Dar hadi mkoani amekosa mpak jamaa kaamua kumpatia na nauli
ASANTENI SANA NDUGU ZANGU KWA SHAURI ZENI HIZI

Nimezipitia kwa umakini sana , nazifanyia kazi na mrejesho wake nitauleta hapa tena ndani ya mwezi huu kua kipi kimejiri baadaya hizi shauri zenu nzuri.

Ahsante na muendelee kunishauri zaidi naamini humu wako baba zetu mama zetu wakubwa zetu na wadogo zetu, ndugu jamaa na marafiki, watajifunza mengi na mazuri kupitia shauri zenu.
Amina!
 
Mkuu hapo Hakuna ndoa tena mnaishi kwa kuviziana kikubwa uyo shemeji mtie talaka akafie mbele
 
Naomba kupata mjuzi wa kuandika TALAKA anisaidie FORMAT yake, nimeamua kufanya maamuzi magum

Asanteni, ukishindwabkuandika hapa nitumie whsp 0755102030 au pm.
Hayo sio maamuzi magumu hata, ni maamuzi ya kawaida ukiwa kwenye situation mbaya kama hii. Afu wafiadini wale wenye tiketi ya mbinguni mkononi wanabwabwaja eti ufunge na kuomba, yani huwezi nishawishi niishi na jambazi kisa eti nitaomba
 
Piga talaka haraka mno. Ukichelewa watakuwahi. Usile wala kunywa hapo nyumbani na mwisho nenda polisi watakupa protection statement omba onana na mkuu wa kanda yako akuandikie. Hawa ma gold diggers. Kuna vifo mpaka leo sivielewi kabisa kama mzee Mambo Mengi, Tob Cohen huko Kenya. This was a dutch billionnaire. He was killed and dumped in a septic tank in his own house. The so called his wife is in custody. Hiyo ndiyo Kikuyu lady.
Hivyo kuwa makini watakuua kweli.
 
Naomba kupata mjuzi wa kuandika TALAKA anisaidie FORMAT yake, nimeamua kufanya maamuzi magum

Asanteni, ukishindwabkuandika hapa nitumie whsp 0755102030 au pm.

Sikia ndugu yangu, jambo hili usiliendee KWA pupa kuwa mtulivu sana tafadhali.
Fanya tathmini ya kina sana kabla ya kufikia conclusion ya kutoa talaka, itakugharimu sana hapo baadaye endapo kama usipokuwa makini sana kwenye wakati huu wa sasa ulionao.
Take care!
 
Ushauri wangu kwako, hakikisha unamtafuta mwanasheria mzuri nenda kabadilishe majina ya mali zako zote zihamishie umiliki kwa dada yako au mdogo wako/au mama yako/baba awe ndiyo mmiliki wa hizo mali....

Kama imeshindikana nenda bank kakope hela nyingi halafu uweke mali zako zote bond halafu ufungue akaunti nyingine bank hizo hela utakazo zikopa uzihamishie huko kwa siri.... Hapo hata ikitokea ulazma wa kugawana mali.. Mwisho wa picha mali zitarudi bank......

Zipo njia nyingi sana ambazo haziumizi kichwa za kideal na vichwa nazi
watu wa kaskazini katika ubora wetu....yani this is this is the sexy and best solution
 
Tena kama hao wanawake ndio wanafiki sana, naamini kabisa angekuwa kijana wake ndio yuko kwenye hii situation asingempa huo ushauri mwanae hata kidogo tena kuna uwezekano na yeye angeuvaa huo ugomvi hili kuhakikisha mali za mwanae haziondoki.

hahahah kabisa asee.
 
Ushauri wangu kwako, hakikisha unamtafuta mwanasheria mzuri nenda kabadilishe majina ya mali zako zote zihamishie umiliki kwa dada yako au mdogo wako/au mama yako/baba awe ndiyo mmiliki wa hizo mali....

Kama imeshindikana nenda bank kakope hela nyingi halafu uweke mali zako zote bond halafu ufungue akaunti nyingine bank hizo hela utakazo zikopa uzihamishie huko kwa siri.... Hapo hata ikitokea ulazma wa kugawana mali.. Mwisho wa picha mali zitarudi bank......

Zipo njia nyingi sana ambazo haziumizi kichwa za kideal na vichwa nazi

Akienda Bank kukopa Pesa, yaani kuchukua Mortgage loan Ni lazima watamtaka awasilishe benki hati ya kiapo cha ridhaa ya mwenza wake/mke (i.e SPOUSE'S CONSENT).
Je ataipataje hiyo hati ya ridhaa ya mke wakati yeye mume haelewani NA mke wake???

Hata kama mwanamke atakubali kusaini hati ya kuridhia kuwa yeye na mume wake wachukue mkopo WA nyumba Benki, (i.e Spouse Consent), huyo mwanaume atakuwa amejikaanga zaidi KWA mafuta yake mwenyewe KWA sababu AUTOMATICALLY HUYO MWANAMKE ATAKUWA MMOJA WA WAMILIKI HALALI WA HIYO NYUMBA ITAKAYOWEKWA REHANI KTK MKOPO HATA KAMA HUYO MWANAMKE HAKUSHIRIKI KUJENGA HIYO NYUMBA.Hapo hapo hiyo nyumba itageuka na kuwa MATRIMONIAL HOUSE/PROPERTY hata kama huyo mwanamke aliziikuta tayari ilishajengwa wakati alipoolewa NA huyo mwanaume.
 
Ninyi watu mara nyingine mnafeli wapi!? Sasa kama ishu ni mali na alizikuta we mpe tu halafu aondoke uanze upya!! Halafu tafuta zingine ndani ya miaka mitano tu, uangalie kama hutokuja kupigiwa magoti
Kama kuna nyumba kazikuta KWA hiyo mwanaume anatakiwa amuachie mwanamke nyumba hizo??Au unamaanisha nini??
 
Mjombaa swala lako hilo laitaji uyakinifuu mkubwa sana na utulivu wa hali ya juu katika maamuzi binafsi kama ningekuwa mim kutokana na imani yanguu ningeongeza mkee wa pili hii ndio tiba yake la sivyoo utahangaika sana na hutapata ufumbuzi
Looh, pole sana ndugu! KWA hiyo ukiongeza mke WA Pili utakuwa umetatua matatizo au umeyaongeza matatizo???
 
Mmmh sasa wasubiri nini wataka ekewa damu ya hedhi kwa chakula muache tuu ila hakikisha unamhudumia mtoto ila unapaswa kumuacha huyo mwanamke
 
Kuna watu mnapitia mazito sana katika maisha haya. Lakini yanatatulika vizuri kabisa hasa hili lako mleta mada.

Kwanza kabisa sikubaliani na hawa wanaokushauri eti uhamishie umiliki wa mali zako kwa ndugu zako, nakwambia tena kwa herufi kubwa USIFANYE KABISA HUO UJINGA, hata hao ndugu zako ni binadamu kama alivyo huyo mkeo tena pengine utakuta wao ndio wana tamaa na roho za kinyama kuliko hata huyo mkeo, nafsi ya mtu hakuna anayeijua zaidi ya mtu mwenyewe. Unaweza ukamalizana na huyo mkeo salama halafu ukaingia tena kwenye mtihani mwingine wa kuzirejesha mali zako kutoka kwa ndugu uliowaamini. Nashauri hizo mali ziache kwenye umiliki wako.

Pili sikubaliani na hawa wanaosema eti umpe mali huyo mwanamke kisha ukaanze upyaa!! Haloo hakuna udhaifu mkubwa na wa kifala kama huu.. Kufanya hivyo ni kuidhurumu nafsi yako pakubwa sana, yaani mali ambazo umezivujia jasho na damu kwa miaka yote hiyo halafu leo hii zije kukwapuliwa na kahaba tu fulani ambaye hajui hata umezipataje eti unaepusha shari na kulinda usalama wako!!? Hapana kabisa usifanye huo upuuzi hata wakutishe vipi kama ni vita acha iwe vita tu, binadamu wote tutakufa. Na tena inatakiwa wakiaanza kuongelea suala la mali unabadilisha sauti kabisa unaongea kwa sauti kali sana hili wajue una uchungu na mali zako ambazo hazimuhusu huyo kahaba wao.

Cha mwisho ulikosea sana kuendelea kusihi na huyo mwanamke mpaka dakika hii. Yaani ulitakiwa umuache tangu siku alioonesha nia ya kuachana na wewe hasa baada ya kwenda kwenye hilo baraza. Cha kufanya naomba kwanzia leo usilale kitanda kimoja wala chumba kimoja wala nyumba moja na huyo mwanamke, kwani huyo sio binadamu tena kwako bali ni SHETANI sasa kwanini uendelee kuishi na satan nyumba moja? Mpige chini leo hii hii na aondoke kama alivyo asichukue kitu chochote hata la kujifutia viatu mlangoni.. pumbafuu zake
What is the way forward?????
Umewapinga tu wenzako Lakini haukutoa suluhisho Sahihi juu ya matatizo aliyonayo.

Daima Kumbuka ya kwamba, mwanamke akienda kumshitaki mwanaume wake kwa kutaka wagawane Mali walizonazo, tayari huyo mwanamke anazo asilimia hamsini (50%) za ushindi.Hii Ni kutokana na masuala ya haki sawa ya 50/50 yaliyopo hapa duniani KWA sasa.

Huyo mwanaume asipokuwa makini NA mwangalifu sana KWA sasa anaweza kuingia hasara ya kupokonywa Mali zote ulizochuma peke yake, ambazo huyo mwanamke hakushiriki kuzichuma.
 
Hapo hamna solution,lengo lao ni mali,na ukizubaa watakuua kweli,sasa cha kufanya,chukua mkopo bank mkubwa tu,mali yako iwe collateral,fungua account ya siri bank zisunde huko hizo fedha,
hakikisha unashindwa kurejesha mkopo bank waje wapige bei,
rudi kupanga chumba kimoja,bedsitter ,maisha yaanze from zero ,atakimbia mwenyewe na matusi juu utayaoga ,wahi sasa wakati bado umezaa nae mtoto mmoja family ikiongezeka itakuwa ngumu

Hivi huwa mnafanya kwanza tathmini ya kina juu ya suala husika kabla ya kutoa ushauri ?
Unazijua vizuri Taratibu za mkopo WA nyumba/mortgage loans??

Kama umeoa au kuolewa, kamwe benki haiwezi kukubali kukukopesha pesa NA kuweka rehani nyumba yako pasipo kuwasilisha Benki hati ya ridhaa ya wenza/mwenza wako, yaani Spouse's Consent, kamwe benki haiwezi kukukopesha pesa bila ya hiyo hati.Labda kwa kufoji documents.
 
Mtoa maada bado yupo!? Wasije wakakuwahi maana huku kutishiana uhai Dah!!! Utani.
Aisee Mpe anacho kitaka mzee baba uendelee kudunda.
 
What is the way forward?????
Umewapinga tu wenzako Lakini haukutoa suluhisho Sahihi juu ya matatizo aliyonayo.
Pasi na shaka na wewe ni mmoja wapo ya hao waliomshauri amuachie mwanamke mali zake zote kisha akaanze upya kununua kwanzia kopo la kuogea😎!! Naeshimu mawazo yako.

Way forward nimetoa hapo, ampe talaka huyo mwanamke na jana ndio ilipaswa iwe mwisho wa kulala nae nyumba moja.
Daima Kumbuka ya kwamba, mwanamke akienda kumshitaki mwanaume wake kwa kutaka wagawane Mali walizonazo, tayari huyo mwanamke anazo asilimia hamsini (50%) za ushindi.Hii Ni kutokana na masuala ya haki sawa ya 50/50 yaliyopo hapa duniani KWA sasa.
Pamoja na kwamba tuko katika zama za third wave feminism na tunaongozwa na misandric legal system, lakini sheria zetu za ndoa bado hazijafikia uonevu kiasi hicho. Sheria zetu zinasema mtawagawana kile kilichopatikana tayari mkiwa ni wana ndoa. Sasa kama huyo mwanamke alikuja na high heels tu, basi ataondoka na hizo hizo high heels.
Huyo mwanaume asipokuwa makini NA mwangalifu sana KWA sasa anaweza kuingia hasara ya kupokonywa Mali zote ulizochuma peke yake, ambazo huyo mwanamke hakushiriki kuzichuma.
Acha kumtisha mwenzio kwenye hamna, apokonywe mali zote kwa misingi ipi hasa? Naomba chukua time jielimishe kuhusu sheria za ndoa kisha uondokane na huu uoga na ujinga(sio tusi) inaonekana hujui kabisa chochote kuhusu sheria za ndoa hasa hapo kwenye talaka.
 
Pasi na shaka na wewe ni mmoja wapo ya hao waliomshauri amuachie mwanamke mali zake zote kisha akaanze upya kununua kwanzia kopo la kuogea😎!! Naeshimu mawazo yako.

Way forward nimetoa hapo, ampe talaka huyo mwanamke na jana ndio ilipaswa iwe mwisho wa kulala nae nyumba moja.Pamoja na kwamba tuko katika zama za third wave feminism na tunaongozwa na misandric legal system, lakini sheria zetu za ndoa bado hazijafikia uonevu kiasi hicho. Sheria zetu zinasema mtawagawana kile kilichopatikana tayari mkiwa ni wana ndoa. Sasa kama huyo mwanamke alikuja na high heels tu, basi ataondoka na hizo hizo high heels.
Acha kumtisha mwenzio kwenye hamna, apokonywe mali zote kwa misingi ipi hasa? Naomba chukua time jielimishe kuhusu sheria za ndoa kisha uondokane na huu uoga na ujinga(sio tusi) inaonekana hujui kabisa chochote kuhusu sheria za ndoa hasa hapo kwenye talaka.

Naheshimu mawazo yako japokuwa sikubaliani nayo KWA kiasi Fulani.
I'm experienced enough in this matter, so I know what I am talking about.
Kumbuka, ugumu mkubwa ktk Kesi kama hizi Ni kuthibitisha uhalali WA umiliki wa Mali hizo beyond the reasonable doubts kuwa Mali husika zinazobishaniwa zinamilikiwa na/au zimechumwa NA mwanaume peke yake au kuna nguvu ya mwanamke pia ilishiriki ktk kuzichuma?????Hapa ndipo huwa kunakuwa NA UTATA mkubwa sana kupita kiasi, Here, the strongest evidences must produced to prove the facts beyond the reasonable doubts.Hapo ndipo Wanaume wengi wanapoangukia, NA hatimaye kusababisha Mali kugawiwa KWA wanandoa ktk kiwango sawa cha 50% kWA 50%.
 
Back
Top Bottom