Baba mkwe anataka nimpe talaka mwanaye ili tugawe mali. Mama mkwe anaenda kwa waganga aniue ili mwanaye arithi mali zangu

Amina ndugu!
Pole ndugu yangu, maisha haya in hatari! Kama we ni mkristo kumbuka ile hadithi ya yule mwana aliyetaka sehemu ya Mali toka kwa baba yake ili akajitegemee kwa tamaa zake! Si unakumbuka kilichomkuta? Funzo, siku zote Mali za dhuruma huwa hazidumu kwa hilo halina mjadala. Kwakuwa hali imeshafikia pabaya kiasi cha kutishia hadi uhai wako, fanya kutoa talaka mpe sehemu ya Mali anayohitaji muachane kwa amani! Kama walivyo kwisha sema wadau wengine hapo juu haitachukua miaka miwili majibu atayapata huyo mwanamke!! Mungu huwa hachezewi hasa katika viapo vya ndoa. Narudia tena pole sana, Fanya maamuzi ya busara vinginevyo itakucost Mali utatafuta kam ulivyotafuta awali.
 
Hivi Nani alibuni ndoa?
Maana unaishi na adui yako huku ukijifariji Ni ndugu yako.
Ningekuwa Mimi Ni wewe Nampa vitu kibao asepe navyo.
Mali zisizohamishika naandika jina la mtoto na hati nakaa nazo Mimi.
Lakini vyombo vya ndani vyote Nampa na mtaji wa kuanzia maisha.
Aende tu maana inaonekana ni maskini wanataka Mali pamoja na ndugu zake.
Baada ya hapo naanza upya na maisha mengine.
Maana mwanamke akishaanza gubu na vitimbwi vya kutaka muachane huyo sio mwenzio tena.
Ashakuwa adui wa wazi wazi.
 
Asante ndugu kwa ushauri.

Hii ndio shida ya kuoa hohehahe, familia nzima inaanza kukutolea macho wewe na mwisho wa siku lazima wakuue tu,ili wamiliki Mali muwe mnaangalia na uchumi wa mnakooa
 
ASANTENI SANA NDUGU ZANGU KWA SHAURI ZENI HIZI

Nimezipitia kwa umakini sana , nazifanyia kazi na mrejesho wake nitauleta hapa tena ndani ya mwezi huu kua kipi kimejiri baadaya hizi shauri zenu nzuri.

Ahsante na muendelee kunishauri zaidi naamini humu wako baba zetu mama zetu wakubwa zetu na wadogo zetu, ndugu jamaa na marafiki, watajifunza mengi na mazuri kupitia shauri zenu.
Amina!
 
Mjombaa swala lako hilo laitaji uyakinifuu mkubwa sana na utulivu wa hali ya juu katika maamuzi binafsi kama ningekuwa mim kutokana na imani yanguu ningeongeza mkee wa pili hii ndio tiba yake la sivyoo utahangaika sana na hutapata ufumbuzi
 
Kiufupi nimeoa mwaka 2017 na tumejaaliwa mtoto mmoja, ila kuanzia mwezi wa 12 mwaka jana nimekuwa katika hali ngumu na mke wangu katika ndoa, amekuwa hanisikii mimi kama mmewe kila kitu anaendeshwa na wazazi wake .

Sasa imefikia baba yake kumuambia adai talaka arudi nyumbani, nilipojua hiyo njama nikawahusisha wazee wa pande zote mbili ,ila kule kwao wakakataa kuhusika, siku sio chache mke wangu akanishitaki kwenye baraza la wazee kuwa anataka haki yake amechoka kuishi na mimi. Nikaitwa kwenye kikao cha wajumbe, akaulizwa aseme shida yake nini , akajibu kuwa anataka tugawe mali zote kila mtu ajue maisha yake, akaulizwa hizo mali mmechuma na mmeo au ulizikuta? Akajibu nimezikuta.

Akaulizwa ni mali gani mmechuma na mmeo tokea mmeoana? Akajibu hatukacha mali yoyote. Wajumbe wakamjibu kuwa kulingana na alikuta hizo mali zote basi hizo mali hazikuhusu.

Tokea hapo alibadili upepo akawa mtulivu hata ile hali ikaisha, sasa kumbe ile hali ilibadilishwa upepo na kuelekezwa kwa ushirikina, ushahidi niliupata kutoka kwa mtu wa karibu na mama mkwe wangu( mama wa mke wangu) kuwa mama mkwe wako anakuendea kwa waganga akuue mwanae arithi hizo mali.

Sasa kwa haya mafupi naombeni maoni na ushauri.

Nawasilisha!
HAMISHA UMILIKI WA MALI ZAKO ZOTE KWA NDUGU ZAKO.
NA NYARAKA ZAKO ZOTE MUHIMU KABIDHI MAHAKAMANI.

wewe unayo ruhusa kisheria kuiambia mahakama kuwa UKIFA MALI ZAKO NANI ARITHI. e.g YATIMA n.k

Wanawake Mungu ana waona.
Ndio maana mm hata gari yangu hajui kama ni yangu, wala hii nyumba anajua Tumepanga n.k n.k
 
We ndio unamjua mkeo vizuri,kama ni akili zake au za kupandikizwa na wazazi
 
Sheria za JokaJeusi za ndoa.
Kabla ya ndoa.
1. Oa mwanamke Bikra.
2. Usioe Mwanamke Masikini. Iwe wa Mali, Akili, roho n.k.

Baada ya ndoa
1. Usimsamehe Msaliti wa mapenzi.
Kuishi na msaliti ni kuisaliti roho yako. Mwisho wake huwa mauti.

2. Usimsamehe Mwanamke Mshirikina au mchawi.
Ukihisi au kugundua iwe kwa dhahiri au kwa kificho. Kwa picha au maandishi. Kwa maneno au kwa video yakuwa mkeo ni Mchawi au Mshirikina. Fukuza bila hata ushauri.

Kuishi na Mchawi ni kujiloga mwenyewe.

3. Mwanamke akisema umuache yaani muachane. Hata kama alisema kwa kutania au akiwa na hasira au akiwa amedhamiria. Mfukuze siku hiyo hiyo. Kamwe hutokuja kujuta.

Mimi ni hayo tuu. Hayo ya mkeo na mali hayanihusu. Ni maamuzi yako.

JokaJeusi
 
Kuna watu mnapitia mazito sana katika maisha haya. Lakini yanatatulika vizuri kabisa hasa hili lako mleta mada.

Kwanza kabisa sikubaliani na hawa wanaokushauri eti uhamishie umiliki wa mali zako kwa ndugu zako, nakwambia tena kwa herufi kubwa USIFANYE KABISA HUO UJINGA, hata hao ndugu zako ni binadamu kama alivyo huyo mkeo tena pengine utakuta wao ndio wana tamaa na roho za kinyama kuliko hata huyo mkeo, nafsi ya mtu hakuna anayeijua zaidi ya mtu mwenyewe. Unaweza ukamalizana na huyo mkeo salama halafu ukaingia tena kwenye mtihani mwingine wa kuzirejesha mali zako kutoka kwa ndugu uliowaamini. Nashauri hizo mali ziache kwenye umiliki wako.

Pili sikubaliani na hawa wanaosema eti umpe mali huyo mwanamke kisha ukaanze upyaa!! Haloo hakuna udhaifu mkubwa na wa kifala kama huu.. Kufanya hivyo ni kuidhurumu nafsi yako pakubwa sana, yaani mali ambazo umezivujia jasho na damu kwa miaka yote hiyo halafu leo hii zije kukwapuliwa na kahaba tu fulani ambaye hajui hata umezipataje eti unaepusha shari na kulinda usalama wako!!? Hapana kabisa usifanye huo upuuzi hata wakutishe vipi kama ni vita acha iwe vita tu, binadamu wote tutakufa. Na tena inatakiwa wakiaanza kuongelea suala la mali unabadilisha sauti kabisa unaongea kwa sauti kali sana hili wajue una uchungu na mali zako ambazo hazimuhusu huyo kahaba wao.

Cha mwisho ulikosea sana kuendelea kusihi na huyo mwanamke mpaka dakika hii. Yaani ulitakiwa umuache tangu siku alioonesha nia ya kuachana na wewe hasa baada ya kwenda kwenye hilo baraza. Cha kufanya naomba kwanzia leo usilale kitanda kimoja wala chumba kimoja wala nyumba moja na huyo mwanamke, kwani huyo sio binadamu tena kwako bali ni SHETANI sasa kwanini uendelee kuishi na satan nyumba moja? Mpige chini leo hii hii na aondoke kama alivyo asichukue kitu chochote hata la kujifutia viatu mlangoni.. pumbafuu zake
 
Ila wanawake bwana, yaani mtu yuko tayari mtoto wake wa kumzaa mwenyewe akue bila baba sababu tu ya tamaa za mali kama hivi.

Kuna wanaume wengi sana wamekua bila kuwaona baba zao baada ya mama zao kuwatanguliza baba zao mbele ya haki na sababu kuu ikiwa ni tamaa ya kumiliki mali .

Tuwe makini sana na hivi viumbe vilivyo ongea na SHETANI face to face.
 
Kama mama na baba wapo rudi miguuni upate pepo zao na kama hawapo waone hata mashangazi walilie haswa

Ikibid angalia namna pata safar fake ya kikazi ambapo utafanya kazi ya kukusanya data kwa mkeo kisha utapata nafasi nzur ya kuachana naye bila kugawana mali
 
Nashukuru nashukuru ndugu mrejesho nitauleta hapa baadaya kutekeleza ushauri wenu.
Kuna watu mnapitia mazito sana katika maisha haya. Lakini yanatatulika vizuri kabisa hasa hili lako mleta mada.

Kwanza kabisa sikubaliani na hawa wanaokushauri eti uhamishie umiliki wa mali zako kwa ndugu zako, nakwambia tena kwa herufi kubwa USIFANYE KABISA HUO UJINGA, hata hao ndugu zako ni binadamu kama alivyo huyo mkeo tena pengine utakuta wao ndio wana tamaa na roho za kinyama kuliko hata huyo mkeo, nafsi ya mtu hakuna anayeijua zaidi ya mtu mwenyewe. Unaweza ukamalizana na huyo mkeo salama halafu ukaingia tena kwenye mtihani mwingine wa kuzirejesha mali zako kutoka kwa ndugu uliowaamini. Nashauri hizo mali ziache kwenye umiliki wako.

Pili sikubaliani na hawa wanaosema eti umpe mali huyo mwanamke kisha ukaanze upyaa!! Haloo hakuna udhaifu mkubwa na wa kifala kama huu.. Kufanya hivyo ni kuidhurumu nafsi yako pakubwa sana, yaani mali ambazo umezivujia jasho na damu kwa miaka yote hiyo halafu leo hii zije kukwapuliwa na kahaba tu fulani ambaye hajui hata umezipataje eti unaepusha shari na kulinda usalama wako!!? Hapana kabisa usifanye huo upuuzi hata wakutishe vipi kama ni vita acha iwe vita tu, binadamu wote tutakufa. Na tena inatakiwa wakiaanza kuongelea suala la mali unabadilisha sauti kabisa unaongea kwa sauti kali sana hili wajue una uchungu na mali zako ambazo hazimuhusu huyo kahaba wao.

Cha mwisho ulikosea sana kuendelea kusihi na huyo mwanamke mpaka dakika hii. Yaani ulitakiwa umuache tangu siku alioonesha nia ya kuachana na wewe hasa baada ya kwenda kwenye hilo baraza. Cha kufanya naomba kwanzia leo usilale kitanda kimoja wala chumba kimoja wala nyumba moja na huyo mwanamke, kwani huyo sio binadamu tena kwako bali ni SHETANI sasa kwanini uendelee kuishi na satan nyumba moja? Mpige chini leo hii hii na aondoke kama alivyo asichukue kitu chochote hata la kujifutia viatu mlangoni.. pumbafuu zake
 
Sawa ndugu, napenda nikujuze tu kua hili swala saiv liko kifamilia na leo kuna vikao vinaendelea kifamilia kwa ajili ya kufanikisha hili.
Kama mama na baba wapo rudi miguuni upate pepo zao na kama hawapo waone hata mashangazi walilie haswa

Ikibid angalia namna pata safar fake ya kikazi ambapo utafanya kazi ya kukusanya data kwa mkeo kisha utapata nafasi nzur ya kuachana naye bila kugawana mali
 
Miaka 5 mingi, miaka 2 tu zitakuwa zishaisha yaani Mimi kwa akili zangu namuachia Kila kitu, naondoka na begi langu la nguo na vyeti basi. Naenda kupambana, unless otherwise km ni mfanyabiashara unaendelea na biashara zako unampa Mali zngne
Sasa kimbembe ni pale anakapo muachia hizo mali huyo mwanamke halafu yeye baada kuanza upya mambo yakamgomea, kila anachojaribu akiendi. Wakati huo huyo mwanamke kwa upande wake mambo yanaenda poa tu na tena anamleta na bwana yake mpyaa wanaishi nae kwenye hiyo hiyo nyumba aliyeachiwa.

Roho itamuuma sana.
 
Back
Top Bottom