Baba Majirani mbona wanatuchukia?

Hivi mara baada ya babu kufa, hakutuachia mrithi? nakumbuka marehemu babu alikua na wazee wenzie waliokuwa na maono kama yake, twaweza kwenda kuwaona hao?

baba kawa mkorofi kaota mapembe baada ya kumrithi babu hataki kusikia la mtu hata la marafiki wa babu amelewa ubaba hadi mila na desturi alizoachiwa na babu kazifungia kwenye kibuyu na kutupa baharini kila anachofanya kimekuwa adui kwa watoto na majirani
 
Na Babu naye aliwakaribisha Mjairani wote akawasomesha na wengine akawa vyumba vya uwaani waishi bila kupa kodi nab walipo jiweza akawapa uraia. aaa jamanii Babu alifika hadi kwenda kuwagomboa walipo 'Ganda !! mmmh leo hii eti wanatusengenya na kupwagaa sijui Baba umewakosaniii? alafu majirani wanatutangazia mabaya kwa wegeni.
 
huyu huyu baba etu Mpendwa!!! Kama ni kweli basi kazi tunayo na safari bado ni ndefu maana tutamalizaje safari yetu pasipo kuwa na majirani???
 
Halafu baba jana majirani wamekutana kwenye ile klabu yenu ya ujirani, wewe hawajakuita eti wanaona umewageuka na huaminiki. Sisi wanao sasa tunaogopa hata kuwatembelea majirani, hasa wale wa kule kwa mzee kimbau mbau kwani hapa kwetu tumewafukuza
 
hahahahaaa nilikua sijaiona hii mkuu, kwani baba ana amslahi gani na hawa watu?? nauliza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…