Baba kuingiza wanawake ndani kipindi mama amesafiri

Baba kuingiza wanawake ndani kipindi mama amesafiri

Busara ni kukaa kimya kama hujui lolote. Kama unaweza kujimudu kupanga geto lako, na mahitaji mengine basi umwambie baba mwenyewe na siyo mama yako.

Mzee wako anafanya makosa tena makubwa sana ila kumfunga paka kengele ni ngumu mno.
Huwezijua chanzo cha yeye kufanya hayo. Usikute mama yako anampa mgongo miaka yote au wanalala mzungu wa nne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapige picha, yaani tafuta ushahidi hlf mjulishe mama. Mzee wako hajitambui mkomeshe.
Hapa utapata ushauri wa kinafiki tu. Angekuwa mama ndo anaingiza vidume ungeshauriwa vzr.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asi thubutu kumuonesha picha mama yake asije akamuua na presha buree....( Za kuambiwa changanya na zako)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu hii imekaaje nipo nyumbani kwa mda na mama mzazi amesafiri kwenda dar kuwaona ndugu zangu wengine. ila mzee naona ana tabia ya kuleta wanawake ndani naona inakuwa too much naona kama hamheshim bi mkubwa.
Mpaka Leo unaishi kwenu mkuu? Hama kaishi hata kwenye mtaro, hayo ya baba na mama nakuhusu nini? We ndo huna akili jiongeze mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba kama huyu asiye na staha kwa watoto wake hafai kabisa. Maadili hana Mzazi huyu kabisa. Mijitu kama hii sijui ni kwa nini isigongwe gari tu ikafia mbali. Mpaka kijana amekuja hapa jamvini maana yake imemgusa na kisaikolojia ni mbaya mno.
 
Mueleze haya maneno mtu mwenye hekima amkalishe Baba yako. Akileta magonjwa ndani mama yako atakua mhanga pia anakufundisha nini wewe mtoto wake?

Una babu, Baba mkubwa au hata kiongozi wa dini, uyaweke wazi baba yako aitwe pasi mama yako kufahamishwa.
 
Nakumbuka kuna dogo alikuwa anamuona baba yake anaingiza wanawake hivyo hivyo kiasi mama yake akiwa safari
Akapata ushauri kwa jamaa yake mmoja
Yaani kila dingi akiagana na demu dogo nae akawa anatongoza na kubeba mzigo
Mwisho akaona amuonyeshe kabisa baba yake akamtolea mlango wa mbele wakati baba akiwa kakaa nje
Ndio ulikuwa mwisho wa uzinzi wa baba yake
Akomeeee


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom