Baba kalogwa na Mama wa Kambo, nifanye nini?

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
1,033
2,000
Habarini wana JamiiForums,

Kwanza niweke wazi mimi ndio nilikuwa wale waumini hatuamini kama uchawi upo lakini now nimeamini. Pia niweke wazi familia yangu iko very structured, hata nikisema nichore family tree basi ni issue.

Ebu twende sasa kwenye mada. Baba yangu ana wake watatu wanaofahamika, mmoja alishafariki zamani sana hata mimi sikuwahi kumuona na ndie aliemzalia mtoto wa kwanza, kaka yetu mkubwa. Mke wake wa pili ni mama yangu mimi ana watoto wanne; wawili wa kwanza ni wa kike. Hawa kila mtu na baba yake lakini sio baba yangu mimi, yaani hapa namaanisha tume-share mama ila wana baba zao ila wawili wa mwisho ndio sisi wa kiume, mimi na mdogo wangu ambaye baba yetu ndio main character hapo juu.

Sasa kimbembe kipo kwa huyo mke wa tatu ambae yupo nae mpaka sasa kazaa watoto 6 wote wa kike, huyu mama sijui kamfanya nini mzee maana mzee yupo busy na hio familia kuliko upande huu wetu, mara ya kwanza niliona kama ni masihara haya mambo na mama alishanipiga marufuku kula kitu chochote nitachopewa na huyo mama maana anaweza hata kuniua na sababu kubwa ni kwamba yeye hana mtoto wa kiume.

Sasa maisha yamesonga nikawa nadhani labda mzee hajali hii familia sababu mama ana watoto ambao sio wa kwake lakini nikajaribu kuchunguza nikagundua mzee ana limbwata moja matata sana, yaani si la nchi hii.

Yaani unakuta huku kwetu kuna mtu ambae ni damu yake anaweza kuumwa na kuna hitaji sh laki 3 utasikia sina hela lakini huko kwake ukisikia mtu anaumwa utashangaa anaenda kutibiwa Ujeruman mara India tena kwa gharama zake sio msaada wala wadhamini.

Yaan karibu kila anachoambiwa na familia hii huku hasikilizi, yaani kila utachomwambia jibu ni rahisi: "Pesa hamna". Ukimwambia kuna biashara nataka nifanye, jibu ni rahii: "Pesa hamna". Kitu pekee anachoweza kutoa pesa ni chakula, maji na umeme kwishaaaa.

Sasa mtu unajiuliza huyu si binadamu siku akifumba macho itakuwaje kuna haja ya kuwa na miradi mikubwa ili tuwe na pesa zetu na sio kwamba hela hana, tatizo pesa zote anaweka kwa familia nyingine wanaishi kitajiri, wanaishi kifahari Sabasaba wanaingia mpaka na gari. Wanamilik miradi ming tu sitoitaja hapa kwa sababu za kimaadili. Mkewe licha ya kuwa hajasoma kampa na kazi ofisini kwake. Ngoja niishie hapo. Kifupi ni kwamba kule anafanya vurugu za pesa lakini familia ya huku inaishi kimaskini sana.

Sasa yote tisa miaka ya apo nyuma kidogo kuna siku nilimwambia mzee nataka nikapige shopping ya nguo akaniambia hana pesa, sikujali maana hilo jibu nishalizoea. Sasa nikasikia mzee anaenda Norway kwenye biashara zake na matembezi humo humo ataenda na mkewe. Sikujali akiwa Norway alinichek kwa Whatsapp nimtumie namba ya kiuno na shati nikamtumia baadae aliporud Bongo akabipigia simu niende kwake kuna nguo kaniletea.

Nilipofika nikaenda mpaka chumbani kwake nikaonana naye tukaongea mawili matatu akaniambia begi la nguo lipo hapo sebuleni kachukue uondoke nalo. Sasa kipindi natoka ndiyo nakutana na huyo mke wake alikuwa kavaa kanga; alikuwa katoka kuoga sikujali mimi nikaelekea sebulen nikafungua begi nikachek pamba nikawa najipanga nilibebe nisepe nalo. He! ghafla nashangaa mzee na yule mkewe wanatoka chumbani wanakuja kwa kasi kama mshale. Niikashangaa wakaniambia chukua suruali moja na shati moja, zengine ziache hapo. Pia mchukulie mdogo wako suruali moja na shati moja.

Sasa nikagundua kuwa mzee alishavurugwa; yaani kipindi natoka pale chumbani yule maza aliwaka. Kingine cha ajabu, yule mama hana mtoto wa kiume. Hizi nguo za kiume za nini? Sasa kipindi nazuga zuga pale sebulen nikawa nasikia hizi tumpe fulani zile fulani na wote aliowataja apo nawajua ni kaka za huyo mama na wafanyakazi wake wa kiume hapo kwake.

Sasa baada ya kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu, kuna siku nikamuuliza dereva wa gari anaye-mdrive huyo mama. Vipi haya mambo mbona sielewi? Akaniambia mdogo wangu sikia nikwambie kitu, unafikir mm sijui kama baba yenu kawatelekeza? Najua sana tu sema nimekaa kimya. Akaniambia huyo mama ni mshirikina na mganga wake yupo Vingunguti, tena akamtaja na dada yake, wote wameolewa ila ndio michezo yao na ajabu ni kwamba kila Jumapili unawakuta church. Mzee wako kafungwa hajielewi.

Duh! Niliona maisha kama movie vile; nilitamani niwe kama Mshana Jr. Nilitamani niwe mganga; nilitamani iniwe mlokole mwenye nguvu; nilitamani niwe hata shehe nikamnasue mzee huko aliponasa.

Naombeni ushauri nifanye nini maana nimefuatilia ni kweli anaenda kwa mganga. Hata pale ofisini kwake nilimweka chemba secretary anieleze ukweli akaniambia ni kweli huyu mmama ni mshirikina, kamfunga vilivyo baba yako.

UPDATE

Nashujurun sn wadau nimesoma comment zote watu wana michango tofaut tofaut yaan mpaka Cristian Ronaldo katajwa humo yaan jamii forum bwana unaweza kuwa na mihasira lkn ukaishia kucheka tu

Pia naomba niweke waz kuwa ishu ya step mother jwenda kwa waganga apk vingungut sio siri inafahamika kabisa na ukoo mzima na ata ofisin anapofanya kaz mzee kila mtu anajua ila wanaogopa kumwambia sababu ya cheo so wazee mnaodai ni LOVE BLIND sikubalian na nyiny hata kidogo

Pia kitendo cha mm kuanzisha thread hii haina tofaut na kutangaza vita baridi COLD WAR nimejaribu kuhaduthia ktk mlolongo ambao watu washindwe kujua mm na nan lkn naamin kuna ambao washajua mm na nan japo wahusika naamin hawapo jamii forum lkn wanaweza kupewa na baadh ya watu wanaowafahanu humu na uyo mmama akipata hz habar brake ya kwanza ni vingungut ila ntachokuja kufanya hatakaa aamin macho yke

Sasa turud kwenye solution mm shida yngu hapa ni kumfungua mzee hz kamba alizofungwa na si vinginevyo nataka aish kwa akili zake na sio akili za kushukiwa na mtu awe huru na mbinu kuu za kufanya hivyo ni tatu tu dini.dawa za sili na waganga

Kuhusu waganga sina ufahanu nao sn na sijui nawezaje kuwatumia ili wafungue hzo kamba

Dini hapa namanisha mashehe na mapadri hawa kidogo nawafahamu ila tatizo din siku hz zimevamiwa qachungaaj aamekuwa weng mno sijui wap naweza kumpata mchungaji wa kwel kutatua hili swala
Mshana Jr tunaomba msaada wako please kuna dawa gan ya asili inaweza kufungua hz kamba za mzee
 

zed B

JF-Expert Member
Jul 12, 2018
562
1,000
Mkuu pole sana tena sana. Hawa wamama wakufikia ni changamoto kubwa sana na ukiwakuta unaweza kusema mama si ndiyo huyu lakini mioyoni mwao ni balaa nyoka kabisa na ndiyo utawakuta kanisani kwenye jumuiya huumkosi yaani full Unafiki.

Kiukweli Cha msingi hapo mkuu Tafuta shehe au Mchungaji anaeeleweka Kama unaona vipi nawe mzamie ukouko Apo msipokua makini mtapotezwa na pengine na wewe ukaharibiwa hii imenitokea na Nina mifano dhahiri mi niliovyogundua ile hali nilizidisha Sana kumtendea wema mwisho wa siku kumbe naonekana boya. Mpumbavu.

Kuwa makini Sana Tena Sana dah
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
13,886
2,000
Usichukulie masihara bibie izi Mambo Kama hazijakukuta unaweza kuchukulia simple. Hapo amna Cha mapenzi ni uchawi kwenda mbele..
Hamna uchawi ni upendo tu kuwa uyaone maisha yalivo. Love is blind oooh
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
13,886
2,000
Nikue mara ngapi mkuu af mapenz gani ya upande mmoja tu uku wengine wakisota Kama kuoa kaoa mwenyewe wake wawili iweje awatenge wengine kwa huduma zilizojaaa ubaguzi.

Mambo mengine wanaume ndy chachu ya matatizoy
Huyo mmoja kamkonga moyo wake na ni soulmate tofauti na hao wengine hajawapenda na unaambiwa upendo haugawanyiki
 

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
1,033
2,000
Mkuu pole Sana Tena Sana. Hawa wa mama wakufikia ni changamoto kubwa Sana na ukiwakuta unaweza kusema mama si ndiyo huyu lakini mioyoni mwao ni balaa nyoka kabisa na ndy utawakuta kanisani kwenye jumuiya huumkosi yaani full Unafiki.

Kiukweli Cha msingi hapo mkuu Tafuta shehe au Mchungaji anaeeleweka Kama unaona vipi nawe mzamie ukouko Apo msipokua makini mtapotezwa na pengine na wewe ukaharibiwa hii imenitokea na Nina mifano dhahiri mi niliovyogundua ile hali nilizidisha Sana kumtendea wema mwisho wa siku kumbe naonekana boya. Mpumbavu.

Kuwa makini Sana Tena Sana dah
Upo sahihi kabisa kumtendea wema huyu mmama ni kazi bure yaan kama ana mapepo fulani kuna wakati hata kumuamkia naona ni ujinga maana kuna siku moja nilimuamkia vizuri tu cha ajabu sasa baada ya kama dakika 2 akaanza kusema wewe fulan mbona hujaniamkia yaan mpaka yule houseboy wake akabak anashangaaa tu naada ya kuondoka nikamuuliza yule houseboy huyu mama akusikia nilivyonuamkia yy mwenyewe akaniambia mm nimebak mdomo waz

Na nahic ile kes kwa mzee ilifika
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom