Baba kalogwa na Mama wa Kambo, nifanye nini?

Baba kalogwa na Mama wa Kambo, nifanye nini?

Na wewe kamloge huyo baba yako uchukue nafasi ya mama wa kambo
 
Sio mchepuko Ila nitasema kweli daima, moyo huwezi kupenda vitu viwili kwa wakati mmoja upendo ukawa sawa lazima Kuna mmoja upendo utazidi
Ila kipindi hiki wanaume wamekua unstable sana,sijui ni globalisation imekua ahead of us,kiasi kwamba tunahisi hatujafanya vitu vingi,we see a beatfull, romantic galz thru Internet doing this and that,and we wish to have that taste in really World,this makes men to step out of their marriage and get trapped in wrong/bad/evil women....May God Help Us
 
Shida sikuhizi upendo wa kweli hamna na wanaume hawapendi kutunza wake wapendeze ka wa mtandaoni ambao ni fake huwezi mlinganisha mama mwenye watoto na slay queen anayedanga na kujiweka smart na mke asiyetunzwa vizuri, pia wengi huoana bila upendo kisa mashinikizo ya kijamii, au mimba matokeo yake upendo usipokuwepo ndio kutendana tu
 
Very true indeed madam,but wahanga ni wazee ,>60's.Kwa vijana ukihesabu muda wanaospend na washikaji ni 88% ya muda wao,na 6%with family 6%sleeping,hawajui homework imefanyikaje ya watoto na unakuta the last time kula chakula ya mkewe hakumbuki most of the time kula bar,huyu atampenda mkewe kweli,sometimes ndo maana wazee wetu walikua wanabeba lunch box....
 
Habarini wana JamiiForums,

Kwanza niweke wazi mimi ndio nilikuwa wale waumini hatuamini kama uchawi upo lakini now nimeamini. Pia niweke wazi familia yangu iko very structured, hata nikisema nichore family tree basi ni issue.

Ebu twende sasa kwenye mada. Baba yangu ana wake watatu wanaofahamika, mmoja alishafariki zamani sana hata mimi sikuwahi kumuona na ndie aliemzalia mtoto wa kwanza, kaka yetu mkubwa. Mke wake wa pili ni mama yangu mimi ana watoto wanne; wawili wa kwanza ni wa kike. Hawa kila mtu na baba yake lakini sio baba yangu mimi, yaani hapa namaanisha tume-share mama ila wana baba zao ila wawili wa mwisho ndio sisi wa kiume, mimi na mdogo wangu ambaye baba yetu ndio main character hapo juu.

Sasa kimbembe kipo kwa huyo mke wa tatu ambae yupo nae mpaka sasa kazaa watoto 6 wote wa kike, huyu mama sijui kamfanya nini mzee maana mzee yupo busy na hio familia kuliko upande huu wetu, mara ya kwanza niliona kama ni masihara haya mambo na mama alishanipiga marufuku kula kitu chochote nitachopewa na huyo mama maana anaweza hata kuniua na sababu kubwa ni kwamba yeye hana mtoto wa kiume.

Sasa maisha yamesonga nikawa nadhani labda mzee hajali hii familia sababu mama ana watoto ambao sio wa kwake lakini nikajaribu kuchunguza nikagundua mzee ana limbwata moja matata sana, yaani si la nchi hii.

Yaani unakuta huku kwetu kuna mtu ambae ni damu yake anaweza kuumwa na kuna hitaji sh laki 3 utasikia sina hela lakini huko kwake ukisikia mtu anaumwa utashangaa anaenda kutibiwa Ujeruman mara India tena kwa gharama zake sio msaada wala wadhamini.

Yaan karibu kila anachoambiwa na familia hii huku hasikilizi, yaani kila utachomwambia jibu ni rahisi: "Pesa hamna". Ukimwambia kuna biashara nataka nifanye, jibu ni rahii: "Pesa hamna". Kitu pekee anachoweza kutoa pesa ni chakula, maji na umeme kwishaaaa.

Sasa mtu unajiuliza huyu si binadamu siku akifumba macho itakuwaje kuna haja ya kuwa na miradi mikubwa ili tuwe na pesa zetu na sio kwamba hela hana, tatizo pesa zote anaweka kwa familia nyingine wanaishi kitajiri, wanaishi kifahari Sabasaba wanaingia mpaka na gari. Wanamilik miradi ming tu sitoitaja hapa kwa sababu za kimaadili. Mkewe licha ya kuwa hajasoma kampa na kazi ofisini kwake. Ngoja niishie hapo. Kifupi ni kwamba kule anafanya vurugu za pesa lakini familia ya huku inaishi kimaskini sana.

Sasa yote tisa miaka ya apo nyuma kidogo kuna siku nilimwambia mzee nataka nikapige shopping ya nguo akaniambia hana pesa, sikujali maana hilo jibu nishalizoea. Sasa nikasikia mzee anaenda Norway kwenye biashara zake na matembezi humo humo ataenda na mkewe. Sikujali akiwa Norway alinichek kwa Whatsapp nimtumie namba ya kiuno na shati nikamtumia baadae aliporud Bongo akabipigia simu niende kwake kuna nguo kaniletea.

Nilipofika nikaenda mpaka chumbani kwake nikaonana naye tukaongea mawili matatu akaniambia begi la nguo lipo hapo sebuleni kachukue uondoke nalo. Sasa kipindi natoka ndiyo nakutana na huyo mke wake alikuwa kavaa kanga; alikuwa katoka kuoga sikujali mimi nikaelekea sebulen nikafungua begi nikachek pamba nikawa najipanga nilibebe nisepe nalo. He! ghafla nashangaa mzee na yule mkewe wanatoka chumbani wanakuja kwa kasi kama mshale. Niikashangaa wakaniambia chukua suruali moja na shati moja, zengine ziache hapo. Pia mchukulie mdogo wako suruali moja na shati moja.

Sasa nikagundua kuwa mzee alishavurugwa; yaani kipindi natoka pale chumbani yule maza aliwaka. Kingine cha ajabu, yule mama hana mtoto wa kiume. Hizi nguo za kiume za nini? Sasa kipindi nazuga zuga pale sebulen nikawa nasikia hizi tumpe fulani zile fulani na wote aliowataja apo nawajua ni kaka za huyo mama na wafanyakazi wake wa kiume hapo kwake.

Sasa baada ya kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu, kuna siku nikamuuliza dereva wa gari anaye-mdrive huyo mama. Vipi haya mambo mbona sielewi? Akaniambia mdogo wangu sikia nikwambie kitu, unafikir mm sijui kama baba yenu kawatelekeza? Najua sana tu sema nimekaa kimya. Akaniambia huyo mama ni mshirikina na mganga wake yupo Vingunguti, tena akamtaja na dada yake, wote wameolewa ila ndio michezo yao na ajabu ni kwamba kila Jumapili unawakuta church. Mzee wako kafungwa hajielewi.

Duh! Niliona maisha kama movie vile; nilitamani niwe kama Mshana Jr. Nilitamani niwe mganga; nilitamani iniwe mlokole mwenye nguvu; nilitamani niwe hata shehe nikamnasue mzee huko aliponasa.

Naombeni ushauri nifanye nini maana nimefuatilia ni kweli anaenda kwa mganga. Hata pale ofisini kwake nilimweka chemba secretary anieleze ukweli akaniambia ni kweli huyu mmama ni mshirikina, kamfunga vilivyo baba yako.

UPDATE

Nashujurun sn wadau nimesoma comment zote watu wana michango tofaut tofaut yaan mpaka Cristian Ronaldo katajwa humo yaan jamii forum bwana unaweza kuwa na mihasira lkn ukaishia kucheka tu

Pia naomba niweke waz kuwa ishu ya step mother jwenda kwa waganga apk vingungut sio siri inafahamika kabisa na ukoo mzima na ata ofisin anapofanya kaz mzee kila mtu anajua ila wanaogopa kumwambia sababu ya cheo so wazee mnaodai ni LOVE BLIND sikubalian na nyiny hata kidogo

Pia kitendo cha mm kuanzisha thread hii haina tofaut na kutangaza vita baridi COLD WAR nimejaribu kuhaduthia ktk mlolongo ambao watu washindwe kujua mm na nan lkn naamin kuna ambao washajua mm na nan japo wahusika naamin hawapo jamii forum lkn wanaweza kupewa na baadh ya watu wanaowafahanu humu na uyo mmama akipata hz habar brake ya kwanza ni vingungut ila ntachokuja kufanya hatakaa aamin macho yke

Sasa turud kwenye solution mm shida yngu hapa ni kumfungua mzee hz kamba alizofungwa na si vinginevyo nataka aish kwa akili zake na sio akili za kushukiwa na mtu awe huru na mbinu kuu za kufanya hivyo ni tatu tu dini.dawa za sili na waganga

Kuhusu waganga sina ufahanu nao sn na sijui nawezaje kuwatumia ili wafungue hzo kamba

Dini hapa namanisha mashehe na mapadri hawa kidogo nawafahamu ila tatizo din siku hz zimevamiwa qachungaaj aamekuwa weng mno sijui wap naweza kumpata mchungaji wa kwel kutatua hili swala
Mshana Jr tunaomba msaada wako please kuna dawa gan ya asili inaweza kufungua hz kamba za mzee
Narejea kijiweni nitakuja hapa
 
Hata Kama ni mapenzi.. huyo mdogo ana kaushetani.

Kama mzee Kanunua nguo.. kazifikisha na kazigawa tayari.. ikawaje akazing'ang'ania!?

Kwani ukipendwa na ukahudumiwa na wale wakahudumiwa kinaharibika nini!?

Huyo mama atakuwa anatumia nguvu ya pendo kufanya mambo mabaya na huo ndio ushirikina wenyewe.
Hiyo sasa ni akili ya Baba yako, wanaume wakati mwingine huwa na akili ndogo za kuwaza mbele, wewe hujawahi ona mke ana achiwa elf 5 na kuna watoto, lakini mchepuko anayeishi mwenyewe anapewa elf 20 kila siku? Hapo ni akili ya mwanaume, mandiko yanasema kaeni na wake zenu kwa akili unazani ni ujinga gani ulimaanishwa hapo?
 
One husband one wife huwa Ina work shida umalaya na watu kutokutulia, matokeo watoto wanaathirika vile mtu una shindwa ku balance
Huwa wanajuta tayari walishachelewa
 
Very true indeed madam,but wahanga ni wazee ,>60's.Kwa vijana ukihesabu muda wanaospend na washikaji ni 88% ya muda wao,na 6%with family 6%sleeping,hawajui homework imefanyikaje ya watoto na unakuta the last time kula chakula ya mkewe hakumbuki most of the time kula bar,huyu atampenda mkewe kweli,sometimes ndo maana wazee wetu walikua wanabeba lunch box....
Wanaume wasiku hizi ujuaji mwingi sana na maarifa hakuna
 
Pole sana brother na mimi yamenikuta kama yako.
Yan nimefukuzwa nyumbani mimi na mdogo wangu maana tukikaa nyumban tuna mkwaza mama wa kambo. Haya maisha yasikie tu kwa mwenzako ila omba yasikukute.
Yan mama wa kambo kamshika mzee haelewi chochote.
Na hii migogoro chanzo chake huwa ni mambo ya kumiliki mali. Mama wa kambo anaona akiwachukia nyie na kuwafanyia kila hila yeye na wanae ndio wata miliki mali zote ila anacho shindwa kujua ni kwamba Mungu ndio mtoa riziki zote unaweza ukamtesa mtu kesho akawa na mafanikio.
Mwingine unampa mali ila inaishia kupotea.
 
Fedha na dhahabu in Mali za bwana,refer Hagai-2;8

Hagai 2:8 -Fedha na dhahabu yote duniani ni mali yangu.

Kwa hiyo ukiona mama wa kambo na watoto wanavitaka waachie,
baba yako akikupa pokea asipokupa usimuulize,pambana tafuta vyako,Muombe Mungu atakupa,kwa kua vyote ni mali Zake,akiamua usizimiliki, hata bilgate akikupa utajiri wake wote anaweza kukunyan'ganya izo mali au Roho yake.

Kikubwa ni kupambana na kumwomba Mungu akupe nguvu ya Kuzitawala,usipokua na Nguvu ya Umiliki, leo ukipata 10M,utazitumia zote mpaka urudi kwenye elfu10 yako uliyoizoea kukaa nayo mfukoni.

Cha mwisho Muheshimu baba yako,narudia tena muheshimu tuu ata akikufanya nini, ikiwezekana kaa mbali nae au mkoa tofauti kabisaa,na amini yeye pia hakuzaliwa na mali alizikuta na akazitafuta hapa hapa Duniani, Usipo muheshimu ukamwonyesha kiburi na zarau hutoboi-kuna msemo unaosema mtoto hupata mali kutoka kwa babae-huu msemo una maana kubwa saaanaaaaa na ni controversial.
 
Hamna uchawi ni upendo tu kuwa uyaone maisha yalivo. Love is blind oooh
Hakuna upendo wa kutojitambua .upendo wa kweli ni zawadi toka kwa mungu wa kweli tunaujua wa uongo huwa ukimloga jumanne tunakwambia jumatano asubuhi .usiende mbali tafuta majina 3 za huyo mama na babako zama kwa masheik magomeni usifanye ujinga wa eti kumchomoa babako bila kuchafua nyota ya huyo mamdogo .mlozi huwa haachi kapige kubwa kabisa ya mnyama .
 
Fedha na dhahabu in Mali za bwana,refer Hagai-2;8

Hagai 2:8 -Fedha na dhahabu yote duniani ni mali yangu.

Kwa hiyo ukiona mama wa kambo na watoto wanavitaka waachie,
baba yako akikupa pokea asipokupa usimuulize,pambana tafuta vyako,Muombe Mungu atakupa,kwa kua vyote ni mali Zake,akiamua usizimiliki, hata bilgate akikupa utajiri wake wote anaweza kukunyan'ganya izo mali au Roho yake.

Kikubwa ni kupambana na kumwomba Mungu akupe nguvu ya Kuzitawala,usipokua na Nguvu ya Umiliki, leo ukipata 10M,utazitumia zote mpaka urudi kwenye elfu10 yako uliyoizoea kukaa nayo mfukoni.

Cha mwisho Muheshimu baba yako,narudia tena muheshimu tuu ata akikufanya nini, ikiwezekana kaa mbali nae au mkoa tofauti kabisaa,na amini yeye pia hakuzaliwa na mali alizikuta na akazitafuta hapa hapa Duniani, Usipo muheshimu ukamwonyesha kiburi na zarau hutoboi-kuna msemo unaosema mtoto hupata mali kutoka kwa babae-huu msemo una maana kubwa saaanaaaaa na ni controversial.
dunia sio laini hivo .mali za baba ni urithi halali sio hiali ya baba .hapa humwambii kazameni chimbo mkachungulie .
 
Back
Top Bottom