Baba Haoni Kuku!

Baba Haoni Kuku!

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Hiki kisa kilinitokea mimi binafsi.
Siku moja bwana nikaamua kuingia kwenye banda la kuku kukagua hali. Nikamkamata jogoo mmoja na kumkagua vizuri. Nikagundua utitiri mwingi kwenye kilemba chake na eneo lote kwenye macho limejaa utitiri. Dawa ya haraka ya utitiri ni kupaka mafuta ya taa kwenye eneo lililoshambuliwa. Nikamwita kijana wangu mdogo (kama miaka 4 hivi) aniletee taa ya chemli, nikijua kwamba nitapata vimafuta kidogo vya taa kumpaka jogoo. Aliponisikia nahitaji taa ya chemli akageukana kuwatangazia ndugu zake: "Nyie! nyie! Baba haoni kuku, anahitaji taa haraka!"

Mpaka leo kila nikimwona huyu kijana nakumbuka alichosema siku ile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom