Baba Askofu anapowashughulikia wajane..........

Ama kwa hakika kweli kufa ni kufaana kikabisa-kabisa
Yawaje haya yawasibu wajane ambao kilio chao ni kanisa lao?
Nilifikiri wajane ni wa kuwaangalia kwa jicho la huruma.,.
Kumbe huyu Baba Askofu kaona ni kivuno...
Wajamani Baba Askofu acha kushughulikia wajane.........

Kiama kimetufika na wanaumme tunateketea.......
Kiama cha wanaumme sasa harusi ya Baba Askofu..........
Kiama cha wanaumme chadhoofisha familia......
Kiama cha wanaumme chazalisha wajane........
Wajamani Baba Askofu acha kushughulikia wajane............

Waumme wanapotoweka si kilio tu huacha bali familia huyumba.......
Yule "bread winner" akiwa kapuni mjane humlazimu kurithi mikoba yake.....
Lishe, pango, matibabu, karo na usafiri ni baadhi ya kero zake.....
Sasa kero za mjane Baba Askofu kwake ni kitoweo.........
Wajamani Baba Askofu acha kushughulikia wajane.............

Pesa za wafadhili za kuhudumia wajane sasa hutolewa kwa masharti.....
Masharti ya Baba Askofu ni moto na mchezo hataki............
Bila ya wajane kumtuliza kiu yake, patupu huambulia mgao wao.......
Kwa kubanwa kila upande wajane waona bora wamtumikie kafiri wapate mradi wao.....
Wajamani Baba Askofu acha kuwashughulikia wajane.........

Ruta umetumia lugha ya ushairi ambayo ujumbe wake unahitaji tafakari.

Baadhi ya wachangiaji hapa hawakukupata vizuri. Hasa maana ya Baba Askofu uliyotumia hapa.
 
Mwanaukweli umelonga ukweli kabisa na ndiyo kazi ya mwanafasihi simulizi.....[MENTION]@Mwanaukweli[/MENTION]
 
Wajane nao wanahitaji kuliwazwa jamani. Tatizo ni kwamba nani anatakiwa kuwaliwaza!

Mungi uko sahihi.....tatizo linakuja pale kero zao ndiyo shubiri yao..............[MENTION]@Mungi[/MENTION]
 
Ama kwa hakika kweli kufa ni kufaana kikabisa-kabisa
Yawaje haya yawasibu wajane ambao kilio chao ni kanisa lao?
Nilifikiri wajane ni wa kuwaangalia kwa jicho la huruma.,.
Kumbe huyu Baba Askofu kaona ni kivuno...
Wajamani Baba Askofu acha kushughulikia wajane.........

Kiama kimetufika na wanaumme tunateketea.......
Kiama cha wanaumme sasa harusi ya Baba Askofu..........
Kiama cha wanaumme chadhoofisha familia......
Kiama cha wanaumme chazalisha wajane........
Wajamani Baba Askofu acha kushughulikia wajane............

Waumme wanapotoweka si kilio tu huacha bali familia huyumba.......
Yule "bread winner" akiwa kapuni mjane humlazimu kurithi mikoba yake.....
Lishe, pango, matibabu, karo na usafiri ni baadhi ya kero zake.....
Sasa kero za mjane Baba Askofu kwake ni kitoweo.........
Wajamani Baba Askofu acha kushughulikia wajane.............

Pesa za wafadhili za kuhudumia wajane sasa hutolewa kwa masharti.....
Masharti ya Baba Askofu ni moto na mchezo hataki............
Bila ya wajane kumtuliza kiu yake, patupu huambulia mgao wao.......
Kwa kubanwa kila upande wajane waona bora wamtumikie kafiri wapate mradi wao.....
Wajamani Baba Askofu acha kuwashughulikia wajane.........

Siyo kuwashughulikia bali nikuwapatia msaada wa kimwili
 
hii ni danganya toto kabisaaa!unawezaje kuzuia kitu ambacho Mungu amekupa kifanya kazi yake af ukakizuia haya ndio madahara yake.well done babaa askofu!!!!
 
Baba Askofu lazima atakuwa anawashughulikia wote hata wale wake za watu natoa angalizo tu tu kwa wale wote wenye wake zao kuweni makini sana na Baba Askofu nimemvulia:yo:
 
But mkuu kuna kipengele kwenye matendo ya huruma cha kuwafariji wajane. (Nadhani kumfariji mtu kuna definition pana)
 
Mimi binafsi hawa maaskofu hasa wa makanisa yaliyochomoza nchini na duniani kote kama miiba ya michongoma wananikwaza sana. Wanafanya mambo kinyume kabisa na maandiko. Uzinzi na uasherati umetawala sana katika dini hizi. Kuwashughulikia wajane ndio kuwashughulikia kimwili na si kiroho hapo ndipo ninapokwazika. Hahahha tusubiri Yesu atakaporudi mara ya pili wa kuhukumiwa ni wengi.
 
Duh hii kali, Baba Askofu amegeuka na kuwa kifimbocheza cha Wajane mmmmh......................... ..

ndivyo walivyo kazi ya dini ni sehemu au njia ya kujipatia ugali lakini Mungu hawako naye hata chembe.....
 
Sasa huyu baba Askofu mbona mbona anakwenda kinyume na maadaili?
Na je hawa wajane hawamjengei mazingira ya kumtega kweli?

FirstLady hujui mnyonge hana haki hata kama anayo?[MENTION]@FirstLady[/MENTION]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom