Baba aliyemkataa utotoni amemkubali ukubwani……! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba aliyemkataa utotoni amemkubali ukubwani……!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 29, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hebu tuchukulie kwamba, umefuatwa, au unafuatwa fuatwa na mtu uliyewahi kuambiwa kwamba ni baba yako ambaye alikukataa tangu ulipokuwa mdogo. Baba huyu alikukataa katakata kwamba wewe sio mtoto wake wa kumzaa na tangu wakati huo hukuwahi kumtia machoni.

  Hii ina maana bila shaka kwamba, hawakuwahi kuishi na mama yako au labda hawakuwa wameoana. Umelelewa na mama au ndugu upande wa mama yako au na wasamaria wema tu. Baada ya kusoma na kupata mafanikio kiuchumi, baba huyu anakuja akiwa anataka umpokee na kumtambua kama baba yako aliyekuzaa. Huenda baba huyu amepigika kimaisha na ndiyo sababu ya kuja kwako au ameshitakiwa na dhamira tu. Hebu niambie, kama ni wewe ungefanya nini?
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Inategemea na circumstances zote zinazozunguka yeye kukataa na pia the real motive ya yeye kutaka kupokelewa na kutambuliwa sasa. Kama motive ni za kutaka kunufaika kiuchumi nk possibility kubwa ni kwa mimi kukubali kumtambua (kama kuna ushahi wa wazi kuwa yeye ndiye baba yangu) lakini kukataa kumpokea. Yote haya pia yatategemea/yatazingatia maoni ya mama na ndugu wengine pia.
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160


  mnh kila mtu na ashike hamsini zake,sana sana nitajifunza kuto-waabandon wanangu,nitahakikisha wanapata all love in the world na kuwajali....hayo ya baba km aliamua kuishi maisha yake na aendeleee hivyo hivyo...lol
   
 4. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nice thread, ajabu sana kuona watu wanakataa damu zao...na si utani nimeisha ona, na tutaendelea kuona, hi dunia kuna vituko na vituko havishi.

  Mtambuzi; Leo nimesoma thread yako mpaa nime furahi, si lazima uwe unatuletea vitabu ndo tufahamu, unaweza kuweka line chache tu kwenye thread zako na watu wakafahamu..
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hahahahahaaaaa
  nitamheshimu kama baba, tena mie huwa sijui kumung'unya maneno nitamuuliza ulikuwa wapi nilipokuhitaji?
  ulinikana kuwa mie sio mwanao nimebadilika nini hadi unione kuwa mie ni mwanao?
  mwisho aniheshimu kama mwanae nami nitamuheshimu kama baba, lakini nitamwambia wazi maswala ya kifedha hayanihusu wala asiniambie...... maana hastahili kufaidi jasho langu......

   
 6. kiagata

  kiagata Senior Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Cha msingi ni kuelewa kuwa amekufuata baada ya kupata mafanikio au amekufuata baada ya kugundua kuwa wewe ni mtoto wake?.Nadhani hilo ndio jambo la kuelewa mapema.Au amekukubali baada ya kugundua kuwa vipimo ya kisayansi kama DNA vimethibitisha kuwa wewe ni mtoto wake harali.Hilo ndio jambo la msingi.Huenda kuna watu wengi walibambikiwa watoto kuwa ni wao au waliporwa watoto kuwa siyo wao,wengine walijua wanadhurumiwa na wengine hawakujua kuwa wanadhurumiwa kutokana na ufinyu wa uelewa katika fani ya sayansi.Jambo la maana ni kuelewa kuwa uzinzi kabla ya ndoa au ndani ya ndoa ni tatizo ambalo linaweza kusababisha kupoteza haki ya mtu mtoto/ukoo na hata maisha. Jambo muhimu ni kufuatilia vipimo vya kisasa kabla haujatoa tamko la kukataa au kukubali suala la mtoto.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Inauma sana ukikataliwa na mzazi wako.
   
 8. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kama tu yeye alivyoweza kunikataa bila kujaribu kupata uthibitisho kuwa mi ni mwanae au la,vivyo hivyo namimi nitamkataa bila kuthibisha kama kweli ni baba yangu au la. Kama nimeweza kuishi maisha ya say 28yrs bila baba,sasa ivi ntashindwa nini?
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni kweli aisee, yaani unahisi ume-miss something, halafu baadae wakati umeshazoea maisha hayo ya kutokuwa na baba ndio anajitokeza...............!
   
 10. RR

  RR JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Kukataliwa na mzazi ni jambo baya kabisa liwezalo kumpata mtoto.
  Kumkubali? Kumkataa akija ukubwani?
  Waweza kumkubali ila usimpe yale anayohitaji toka kwako....unamkubali na kumwekea mipaka yake!
   
 11. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwanza nitamshukuru kwa kunitambua then tutaenda kupima dna km tukihakikisha ndie mzazi wangu,
  Najua atajieleza yote yaliyotokea kila kila kitu,nitakubaliu kumtambua km mzazi wangu,
  Nitamwomba amwombe msamaha mama na vile watakavokubaliana na mama mie sitaongeza lolote,
  Najua wamama husamehe then nitamsaidia kwa lile ninaloweza km mzazi wangu,kwan kisasi ni cha mungu pekee,na mungu alikuwa na sababu za kunifanikisha ili yeye aone na ajifunze kupitia kosa lake!

  Naamimi ukweli wa kuachana kwao mpaka kunikana na kumtelekeza mama ni wao pekee na mungu ndio wanajua,hasa hasa nitamshukuru mungu kwa kumuweka huyo baba mpaka akaniona nimefanikiwa na kuhitaji msaada wangu mie aliyenikataa!
   
 12. RR

  RR JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Hata kama utakubali matokeo (kutokua na baba), ila nafsi yako haitapata amani hadi umfahamu baba yako.....
   
 13. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #13
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Nitamkataaaaa kata kata!
   
 14. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #14
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  hata ukimkataa ukweli unabaki kwamba ni baba yako..
  Ila ni ngumu sana kuwa na mapenzi nae..
   
 15. YNNAH

  YNNAH JF-Expert Member

  #15
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Jaman inategemea na mazingira ya baba kutomtunza huyo mtoto. Nina mfano hai juu ya hili,kuna mkaka alimpa mimba bint,wazazi wa yule bint hawakutaka hata kuiona pua ya yule mkaka na wakamuamisha kabisa bint yao ule mji. Huko alikoenda akajifungua na kumlea mwanae hadi amekuwa mtu mwenye kujitegemea. Kumbe yule mkaka alikuwa anafuatilia kila kitu kupitia rafiki wa bint,mwisho wa siku akajitojeza kwa mwanae. Je,baba hapo atakuwa na kosa?
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tukiwa na majibu mepesi tutapoteza maana halisi ya hii thread.
  Mutambuzi, labda utwambie wakati huo jamaa anakataa mtoto alikuwa single ama alikuwa keshaoa? Kama alikuwa keshaoa huoni alikuwa anajaribu kuinusuru ndoa yake! Kama alikuwa bado hajaoa yeye na huyu mama wa huyu mtoto hawakupanga mipango yao kabla ya kuleta huyu kiumbe duniani? Je walikuwa wako tayari kuwa wazazi?
  Kuna mambo mengine yanaweza kuchangia ila pia kuna wale play boy wanaochezea maisha ya wenzao.

  Sasa kumkubali ama kumkataa!
  Unaweza kumkataa kwa ajili ya hasira tu! Lakini kila ukimwona roho itakuuma tu as huyo ndo baba yako tu na hujawahi kuambiwa mwingine! Tena mbaya zaidi kama amechoka ndo atakutia huruma zaidi.
  Ki ukweli hutakuwa umetenda kosa kumkataa ila na hali yako uliyokuwa nayo (uwe tajiri ama maskini) ni vizuri mkaa chini na kuelewana. Mtu mzima anapokaaa chini na kuamua kujirudi ujue keshajua kosa lake! Amini iko siku utamhitaji mzazi wako! Kuna waliowahi kutamani kumwona mzazi wako japo mara moja tu na hampati.
  Mimi ntampokea tu na sitomuuliza chochote. Alifanya makosa amenitafuta kanipata hayo mengine tutayajua huko mbele.
  Mzazi yeyote mtamu sana bana hata kama ana miaka 100.
   
 17. k

  kiliochangu JF-Expert Member

  #17
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 1,122
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  hivyo vipimo kwanini vipimwe ukubwani na sio wakati mtoto mchanga ili kuwa na equal responsibility. Hii ni janja ya kukataa na kukwepa majukumu kwa visingizo kibao. Ili ukumbuke hakuna aliyewahi kukataa watoto akafanikiwa. huwezi jua yupi ana nyota ya mafanikio
   
 18. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #18
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Mkuu Mtambuzi, kwanza hongera kwa uzi mzuri wenye ujumbe murua. Binafsi, nina marafiki zangu wengi ambao wamekulia ujombani, hata baadhi yao kudiriki kutumia SURNAME za ujombani!!! Wengi wao ukisikiliza visa vyao utalia kwa jinsi vinavyosikitisha! Unakuta mtu baba yake ni Mgogo lakini anatumia sirname ya Kihaya coz mama yake ni mhaya na alitelekezwa na babaye pindi alipozaliwa tu!

  Kwa kuzingatia hali hii, kwakweli, haya mambo ya baba kuja kwako ushakua mkubwa lakini ulivyokua mdogo(mhitaji) alikuwa hataki kusikia habari zako!!! QUOTE=Mtambuzi;3405051]Hebu tuchukulie kwamba, umefuatwa, au unafuatwa fuatwa na mtu uliyewahi kuambiwa kwamba ni baba yako ambaye alikukataa tangu ulipokuwa mdogo. Baba huyu alikukataa katakata kwamba wewe sio mtoto wake wa kumzaa na tangu wakati huo hukuwahi kumtia machoni.

  Hii ina maana bila shaka kwamba, hawakuwahi kuishi na mama yako au labda hawakuwa wameoana. Umelelewa na mama au ndugu upande wa mama yako au na wasamaria wema tu. Baada ya kusoma na kupata mafanikio kiuchumi, baba huyu anakuja akiwa anataka umpokee na kumtambua kama baba yako aliyekuzaa. Huenda baba huyu amepigika kimaisha na ndiyo sababu ya kuja kwako au ameshitakiwa na dhamira tu. Hebu niambie, kama ni wewe ungefanya nini? [/QUOTE]
   
 19. m

  mkazamjomba Member

  #19
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa uangalie alipokukataa athari alizopata mama yako halafu mshirikishe mama yako muwe lenu moja kama umesamehe pia umshirikishe maumivu ya kukataliwa yana athari zake kama umesamehe asikufanye ATM
   
Loading...