Hii hotuba ya Gavana wa Bungoma Ken Lusaka mbele ya Polisi imewagusa wengi

Hii hotuba ya Gavana wa Bungoma Ken Lusaka mbele ya Polisi imewagusa wengi

Joined
Oct 5, 2025
Posts
83
Reaction score
343
Video ya Gavana wa Bungoma, nchini Kenya, Ken Lusaka, imekuwa gumzo mitandaoni baada ya kuwapa ukweli mchungu maafisa wa usalama.

Aliyasema hayo Januari 2024 kwenye uzinduzi wa kituo cha “Reinforcement” katika kaunti hiyo.

Katika hotuba yake iliyojaa busara na vionjo vya ucheshi, Lusaka amewataka askari kutumia "moyo wa utu" wanaposhughulika na raia. Gavana huyo alisisitiza kuwa hata katiba inaruhusu nguvu ya kiasi (reasonable force) na si ukatili.



"Na maafisa wa usalama (enforcement officers), najua mna kazi ngumu, lakini nataka kutoa mwito kwenu kwamba hata mnapotekeleza majukumu yenu ya kusimamia sheria, hebu tufanye hivyo kwa moyo wa kiutu. Tuwe na ubinadamu. Tunashughulika na wanadamu, kwa hivyo tusitumie nguvu kupita kiasi tunaposimamia sheria.

Kwa sababu hata Katiba inasema mtatumia nguvu ya kiasi (reasonable force). Hata ukizawadiwa bunduki—na sisi ambao tumepitia mafunzo, mimi pia nimefundishwa kutumia bunduki—unaitumia tu katika mazingira magumu na ya hatari sana. Hupigi risasi hovyo kwa sababu tu una bunduki.

Kwa hivyo, tunapoenda kwa hao wananchi, mjue kuwa hawa wananchi... tunaendesha serikali ya kisiasa. Nao ndio waliotuweka madarakani. Hivyo basi, hata tunapoenda kushughulika nao, tushughulike nao kwa sura ya kiutu.

Mkikumbuka kwamba nanyi pia mmetoka hapa hapa. Ni vile tu mmepata upendeleo wa kuwa maafisa wa usalama. Huyu mwingine unayempiga, pengine ni mama wa ndugu yako, ni mama yako, au ni baba yako. Kwa hivyo, tuwe na mtazamo huo mnapofanya kazi, ili tupunguze malalamiko kuhusu jinsi tunavyohudumia umma.

Ili utakapostaafu, watu waseme 'Ndiyo'... mnaona namtambua Mahanu kwa sababu alinifunza vizuri na anajivunia. Ukimwita anaweza kuja. Lakini kama umezembea na kuumiza watu, hata ukistaafu watu wanakuweka kwenye maombi (ya laana). 'Ee Mungu, sema neno moja tu na roho yetu itulie', au 'utuondolee huu mzigo ambao unatuumiza'.

Kwa hivyo, tambueni kwamba mnawatumikia watu wenu."
 
Back
Top Bottom