Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wamenyong'onyea baada ya ndoto za Ubunge "kuyeyushwa"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Kiukweli angalizo lililotolewa na Rais Magufuli kwa wateule wake wanaotamani ubunge limewanyong'onyeza baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wilaya.

Chalamila kwa mfano tulitegemea ataenda kumstaafisha mchungaji Msigwa pale Iringa mjini lakini ndio hivyo tena, nafasi yake imechukuliwa na msanii Pierre Liquid.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi hii ya kuwapiga biti hawa wakuu wa wilaya/mkoa ina maana gani?
Ina maana idadi ya watakaoishi kama mashetani lazima iongezeke. Unamzuia raia mwenzako, kwa sababu wewe ndio una haki zote, haki ya kugombea nafasi ya uwakilishi, na si ajabu awamu ijayo usiwepo kwenye huo ukuu wa wilaya au mkoa.
Na watu wameshikwa na kigugumizi hawajui mustakabali wao. Nguvu ya wananchi imepokwa na mtu mmoja, akiitwa dikteta, wanalalamika.
 
Waliteuliwa kwa mkakati maalumu.sasa wao kama wanataka kuondoka halafu nani atalinda kura za raisi
 
Saa Nyingine Ni Kuridhika Hauwezi Kuwa Na Kila Kitu
Nitamshangaa CDF Akienda Kugombea Busega Aje Awe Waziri Wa Ulinzi
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Hivi hii ya kuwapiga biti hawa wakuu wa wilaya/mkoa ina maana gani?
Walizidi uroho,,mtu una kazi nzuri,,mshahara wa milioni moja,,unapata wapi tamaa ya kazi nyingine,nyumba ya bure gari ya kutembelea na mafuta fulltank kila siku,posho za ziara yaani mda wote uko full,,hela ya mishikaki,viti moto na bia haipigi chenga
 
Nani anawapiga pini wasanii maana nao wamezidi hadi mkongwe wao Master J anautaka.
 
Kipi bora kati ya kuwa mkuu wa wilaya/mkoa huku ukiwa huna hakika kama kesho hautatumbuliwa na mteuzi wako na kuchaguliwa na wananchi watakaokupa uhakika wa ulaji kwa miaka mitano?
 
Unajua kuna vitu ukivi imagine unajikuta unaangua kicheko hata usiku wa manane mf unasikia mbunge wa iringa mjini mh Pierre liquid naomba ukae chini😀😆😀
 
Back
Top Bottom