Baadhi ya Wabunge wataka serikali 3

Baadhi ya Wabunge wataka serikali 3

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
mwanzo
bread_sep.gif
Habari
bread_sep.gif
kitaifa
bread_end.gif

KITAIFA

pinda%2526warioba.jpg

Na Julius Magodi

Imetumwa Jumapili,Novemba4 2012 saa 8:25 AM


KWA UFUPI


WAPENDEKEZA MAWAZIRI WASIWE WABUNGE, VITI MAALUMU VIFUTWE, URAIS MIAKA 35


WABUNGE jana walijilipua baada ya baadhi yao kupendekeza kuwa muundo wa Muungano ubadilishwe kuwa wa Serikali tatu na kwamba, mawaziri wasiwe wabunge.

Pamoja na mapendekezo hayo, wengine walitaka umri wa kugombea urais ushushwe na kuwa miaka 35, badala ya sasa ya miaka 45.

Wakitoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba mjini Dodoma jana, wabunge hao pia walitaka viti maalumu vya ubunge vifutwe, badala yake wanawake warejee kugombea ubunge majimboni.

Katika mkutano huo, zaidi ya wabunge 36 walitumia nafasi hiyo kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali yenye masilahi kwa taifa, waliyoona yanafaa kuingizwa kwenye Katiba Mpya, ambayo mchakato wa ukusanyaji maoni ya uundwaji wake, unaendelea.

Muungano
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alitaka muundo wa muungano ubadilishwe na kuwa wa Serikali tatu, badala ya uliopo sasa aliosema una kasoro nyingi.

Moja ya kasoro hiyo ni wawakilishi kuruhusiwa kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, huku wabunge wa Bara wakiwa hawana uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi.
“Mwenyekiti, tuwe na Serikali tatu katika muungano, vinginevyo kila mmoja abaki na chake," alisema.

Pia alitaka viti maalumu vifutwe, badala yake wanawake wawekewe majimbo ya wilaya, ambayo watagombea na wenzao.

Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo naye alitaka muundo wa muungano uwe wa Serikali tatu pamoja na kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika nafasi mbalimbali.

Alisema kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wasitokane na wabunge kwa sababu hawataweza kufanya kazi kwa ufanisi na ni mgongano wa kimasilahi.

Mbunge wa Mkanyangeni (CUF), Mohamed Mnyaa alitaka kuwapo na Serikali tatu katika muungano.

Alisema kama Tanzania Bara watakataa kuita nchi yao Tanganyika basi wanaweza kuiita jina lolote hata Mzizima.

“Muungano uwe wa Serikali tatu, Tanganyika wawe na nchi yao na sisi tuwe na Zanzibar yetu, kama bara hawataki kuiita nchi yao Tanganyika basi wanaweza kuiita hata Mzizima,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Chakechake, (CUF), Mussa Haji Kombo alitaka muundo wa Muungano uliopo ubadilishwe badala yake uwe wa mkataba.

Alisema muundo uliopo hivi sasa unawanyima haki Wazanzibar, akitoa mfano wa suala la mafuta alilosema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), haina uwezo wa kufaidi raslimali yake bila ya kuwasiliana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

“Tuvunje muungano huu, tuanzishe ushirikiano mpya wa mkataba,” alisema.

Mawaziri


Akitoa maoni yake, Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR- Mageuzi) Moses Machali alisema kuwa mawaziri wasiwe wabunge ili kuondoa mgongano wa kimasilahi.

Alisema kuwa ni vigumu kwa wabunge kumdhibiti waziri ambaye ni mbunge mwenzao kama ilivyo sasa.


Alipendekeza kuwa, Katiba Mpya itamke kuwa mtu akipatikana na kosa la kuhujumu nchi anyongwe pamoja na kuwapo kwa Serikali ya Majimbo, ambayo itasaidia Serikali kutoa huduma kwa wananchi.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Kessy alitaka umri wa mtu kuruhusiwa kugombea urais upunguzwe kutoka miaka 45 ya sasa hadi miaka 35.

Alisema kuwa umri huo utasaidia kupatikana rais kijana, ambaye anaweza kuhimili vishindo kwa kutembea mikoani bila ya kuchoka, badala ya kuwa na rais mzee atayekuwa akienda kutibiwa nchini India mara kwa mara.

Mbunge huyo alipendekeza pia wabunge wawe na kikomo kwa kutumikia vipindi viwili na kwamba, viongozi wastaafu wasiruhusiwe kuwapo bungeni akieleza kuwa hivi sasa wengi wanatumia muda mwingi kusinzia.

Kessy alipendekeza pia Baraza la Mawaziri lipunguzwe ukubwa akitaka wawe mawaziri 14 na manaibu mawaziri wawe 24.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, alitaka kuwapo Tume Huru ya Uchaguzi na mwenyekiti wake akiteuliwa na Rais, lakini athibitishwe na Bunge.
Pia alitaka viti maalumu vya ubunge vifutwe na badala yake wanawake waende katika majimbo kugombea sambamba na wanaume.


Msigwa alisema kuwa kuendelea kuwa na wabunge wa viti maalumu ni kuwafanya waendelee kujiona wanyonge, wakati hivi sasa kuna wanawake wenye uwezo mkubwa sawa na wanaume.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zakia Meghji alitaka muundo wa muungano uliopo ubaki kama ulivyo isipokuwa kero ndogondogo za muungano ziondolewe.
Alisema suala la uchumi wa Zanzibar linatakiwa kuangaliwa upya ili kuwafanya Wazanzibar kunufaika na raslimali zao.


Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisema muundo wa muungano ubadilishwe kuwe na rais mmoja na mawaziri wakuu wawili wa kutoka Zanzibar na Bara.

Alipendekeza Rais akae madarakani kwa kipindi cha miaka saba na baada ya hapo asiruhusiwe kugombea tena.

Zitto pia alizungumzia umri wa kugombea urais akitaka uwe miaka 35 na kwamba wanaotaka umri wa miaka 45 hawana hoja.

Mbunge huyo amekuwa akikaririwa akitaka umri wa urais uwe miaka 35, akisema anaweza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Kauli hiyo imekuwa ikimletea mgogoro mkubwa kati yake na viongozi wa chama chake akiwamo mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei.

Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alitaka umri wa kugombea urais uwe miaka 35, ili kutoa nafasi kwa vijana kushika nyadhifa za juu za uongozi wa nchi.
Pia alitaka Kiswahili kiwe lugha rasmi na kwamba mikataba yote muhimu ya uwekezaji isainiwe bungeni.


Nyangwine alitaka Katiba Mpya itamke kuwa watu wanaopatikana na makosa ya kuhujumu nchi wanyongwe.

Zitto pia alizungumzia umri wa kugombea urais akitaka uwe miaka 35 na kwamba wanaotaka umri wa miaka 45 hawana hoja.

Mbunge huyo amekuwa akikaririwa akitaka umri wa urais uwe miaka 35, akisema anaweza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Kauli hiyo imekuwa ikimletea mgogoro mkubwa kati yake na viongozi wa chama chake akiwamo mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei.

Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alitaka umri wa kugombea urais uwe miaka 35, ili kutoa nafasi kwa vijana kushika nyadhifa za juu za uongozi wa nchi.

Pia alitaka Kiswahili kiwe lugha rasmi na kwamba mikataba yote muhimu ya uwekezaji isainiwe bungeni.


Nyangwine alitaka Katiba Mpya itamke kuwa watu wanaopatikana na makosa ya kuhujumu nchi wanyongwe.


 
Nimeipenda WABUNGE wawe na kikomo cha kugombea EITHER DURU 2 au DURU 3;That's IT... Nimeipenda ile ya RAIS awe Kijana ili aweze kutembea NCHI nzima badala ya kupelekwa pelekwa INDIA kwa MATIBABU

Suala la MHUJUMI UCHUMI KUNYONGWA Hii Naipenda SANA

Hakuna VITI Maalum BRAVE kwa BULAYA kusema na ni vizuri
 
Unategemea nini kutoka kwa wanasiasa? wanataka kujiongezea nafasi za kisiasa. Serikali 3 hazina tija kwa Tanganyika wala Zanzibar zaidi ya kuongeza gharama na kurudisha nyuma maendeleo
 
Nakubaliana na zito tuwe na Rais mmoja na mawaziri wakuu wawili. Mabunge matatu madogo. Wizara 12 bara, 8 zanzibar na 5 za federation. Wizara zote ziainishwe kwenye katiba na majukumu yake. Rais awe na uwezo wa kuunda Wizara zisizo zidi 2 kudeal na mambo yanayojitokeza. Wizara zitakazo hitaji manaibu mawaziri ziwekwe na kila naibu awe na role siyo kama sasa ambavyo manaibu waziri wanafanya kazi wanazotumwa na mawaziri.

Mawaziri wakuu watapigiwa kura na wananchi na ndiyo watakao unda serikali mbili ya Zanziba na Tanzania. Jina la bara liendelee kuwa Tanzania na Serikali ya muungano itaitwa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Viongozi wote wa idara, wizara, taasisi, halmashauri wataomba ajira ka.a kawaida na kuthibitishwa na bunge. Watapewa mikata ya miaka mitano renewable based on performance.

Waziri watokane na mti yeyote na wathibitishwe na bunge.

Serikali za mitaa ziwe na madaraka kamili chini ya wenyeviti au mameya.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom