Baadhi ya wahitimu wa Darasa la saba kubadilishiwa namba siku ya Mtihani! Wizara itoe ufafanuzi

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,444
11,942
Salaam

Nimeamka asubuhi hii na kama ilivyo ada huwa nasoma habari mbali mbali kujua mambo yanakwendaje kisha ndio nielekee kwenye majukumu yangu, ghafla nakumbana na Video hii ya mtoto aliyehitimu darasa la saba akilalamika kubadilishiwa namba ili lengo afelishwe na nafasi yake apewe mwengine!!

Anajitambulisha na kuweka wazi kila kitu kuwa siku ya Mtihani alipewa mitihani isiyokuwa na namba yake na pindi alipouliza hakupewa jibu la maana na zaidi aliambiwa hayo mambo yaishie hapo hapo hata wazazi wake asiwaambie!!

Hali hii ikanipa wasi wasi na hasa kwa sababu na mimi nina binti yangu amehitimu juzi pia, hivyo nikamuita na kumuuliza iwapo amefanya mitihani kwa namba yake, majibu yakaninyong'onyeza zaidi!

Akaniambia mitihani yote iliyopita namba yake ni 29 lakini katika huu wa kumaliza walibadilishiwa siku hiyo hiyo na akapewa namba 30!

Mamlaka husika, Waziri wa Elimu na kila anae husika tunaomba mjitokeze tujue mbivu na mbichi maana hili jambo linaleta hasira mno.

Kuna mbinu gani? Kwa nini inakuwa hivi na lengo ni nini?

Wasi wasi ni mwingi sana juu ya Elimu yetu na namna inavyochezewa hasa tukiona kwengine huko hadi
inaundwa tume.

Huu ni uhuni wa kiwango cha SGR kwenye elimu ya watoto wetu.
Halafu uhuni wenyewe unafanywa na shule inayomilikiwa na taasisi ya dini.

Serikali inapaswa mara moja kuchukua hatua zifuatazo:
1. Msimamizi wa mitihani aliyekuwepo kukamatwa na kuchunguzwa.
2. Mwalimu mkuu wa hiyo shule kukamatwa na kuhojiwa.
3. Shule husika kuchunguzwa kwa kina na ikijulikana huo udanganyifu mara moja hiyo shule ifungwe.
4. Mitihani yote ya hiyo shule ya darasa la saba mwaka huu kuchunguzwa kwa kina.
 
Screenshot_20221014-103738_Instagram.jpg
 
Salaam

Nimeamka asubuhi hii na kama ilivyo ada huwa nasoma habari mbali mbali kujua mambo yanakwendaje kisha ndio nielekee kwenye majukumu yangu, ghafla nakumbana na Video hii ya mtoto aliyehitimu darasa la saba akilalamika kubadilishiwa namba ili lengo afelishwe na nafasi yake apewe mwengine!!

Anajitambulisha na kuweka wazi kila kitu kuwa siku ya Mtihani alipewa mitihani isiyokuwa na namba yake na pindi alipouliza hakupewa jibu la maana na zaidi aliambiwa hayo mambo yaishie hapo hapo hata wazazi wake asiwaambie!!

Hali hii ikanipa wasi wasi na hasa kwa sababu na mimi nina binti yangu amehitimu juzi pia, hivyo nikamuita na kumuuliza iwapo amefanya mitihani kwa namba yake, majibu yakaninyong'onyeza zaidi!

Akaniambia mitihani yote iliyopita namba yake ni 29 lakini katika huu wa kumaliza walibadilishiwa siku hiyo hiyo na akapewa namba 30!

Mamlaka husika, Waziri wa Elimu na kila anae husika tunaomba mjitokeze tujue mbivu na mbichi maana hili jambo linaleta hasira mno.

Kuna mbinu gani? Kwa nini inakuwa hivi na lengo ni nini?

Wasi wasi ni mwingi sana juu ya Elimu yetu na namna inavyochezewa hasa tukiona kwengine huko hadi
inaundwa tume.

View attachment 2386619

Back
Top Bottom