Baadhi ya Wafanyakazi kwenye ofisi za TRA Kibo (Tegeta Branch) wana lugha chafu sana

Victor Mlaki

Verified Member
May 1, 2016
1,817
2,000
Jana nilikwenda kulipa kodi za biashara za Wazazi wangu ili kupata clearance na leseni kwenye ofisi niliyoitaja ila nilichokutana nacho kilinifedhehesha sana.

Niweke wazi kuwa ofisi hiyo ina wahudumu wazuri sana na wanaosali wateja ila huyu Dada niliyekutana naye alinikera sana kwa lugha yake chafu na dharau kwa wateja.

Ni Dada mmoja Mdogo tu ila ana kiburi cha kipuuzi sana ambacho sikutegemea kukutana nacho. Alikuwa anawajua Wazazi wangu na biashara zenyewe zilipo ila alinikera zaidi kusema " Mzazi wangu ni Mlevi" jambo ambalo siyo kweli na huenda alikuwa haelewi unachosema.

Core values za TRA zinaelekeza Professinalism, Integrity and Accountability. Ni vizuri hawa akina Dada wakakalishwa chini na kueleweshwa misingi hiyo ili waache kufanya kazi kwa mazoea.
 

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,848
2,000
Ila upande wa customer care kwa Tz ni terrible! Wahudumu hawajali wateja japo ikifika mwisho wa mwezi anatabasamu akienda benki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom