Kampuni ya Abood muondoeni huyu kijana kazini ana lugha chafu na za maudhi sana

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Kampuni ya Abood muondoeni huyu kijana kazini ana lugha chafu na za maudhi sana

Sijawahi kuona watu wa ajabu kama hii kampuni ya Abood jana tarehe 15 November kuna kaparcel kwa kwenye bahasha nilikuwa naenda kumtumia mtu kimfikie hapo Chalinze

Nikaenda abood pale Kariakoo ofisini kwao wakanambia wao mizigo ya Chalinze hawatumi hapo bali wanatuma ofisi zao za Ubungo Shekilango

Mdogo mdogo huyo nikaenda kupanda mwendokasi hadi Ubungo nikaenda kwenye ofisi zao zilizopo kwenye ile sheli ya Engen.

Kufika namkuta kijana kavaa tishert ya Yanga mweusi , na muhudumu mwingine ana muonekano kama kiarabu hivi na wafunga mizigo wengine wa pale.

Nimefika kwanza huyo kaka alovaa tishert ya Yanga akanambia niende kwanza wanapofunga mizigo nikachukue mark pen niuandike vizuri huo mzigo maana bahasha ile niliandika kwa pen ya kawaida kufika kule nikanyimwa mark pen akanambia niende kwa wa dirishani ambaye ndo huyo kaka alovaa tishert ya Yanga

Nimefika dirishani hanihudumii yupo busy anachati na simu yake baadae akaniuliza huo mzigo unaotuma Chalinze uko wapi? Nikamuonyesha ile bahasha akaniuliza thamani ya mzigo nikamuambia ni elfu 10 maana zilikuwa ni earphones tu

Akanambia kuutuma huo mzigo Chalinze ni elfu 15 nikamuuliza hapo Chalinze elfu 15 kibahasha tu chenye earphone mbona ghali sana maana huwa natuma kwa 5000

Akabadilika hapo hapo akaanza kunambia kwanza hawatumi mizigo Chalinze na akaniamrisha kwa kejeli kuwa niondoke "Sepaa" kila mtuma mizigo alokuwepo pale alinionea huruma na wakashangaa sana mmoja akaja kunambia ndo tabia za huyo kaka

Nilikuwa na hasira hadi natetemeka huko njiani nilivyopoteza muda wangu na nauli kupanda na kushuka huyo kaka aiyekuwa anahudumia Abood na tishert ya Yanga wangemuondoa maana hana adabu mshenzi yule
 
Wewe ungeenda Mbezi mwisho upande wa daladala, pale ungekuta costa za Morogoro, chukua namba ya dreva, na namba ya mpokeaji weka juu ya bahasha, mpe dreva 5000 , ile namba ya dreva mtumie mpokeaji, na dreva mpe namba ya anayepokea, fasta tu masaa matatu mengi mzigo unapokelewa kikubwa mpokeaji awe fasta asiwe mtu wa kujivutavuta,
 
Wewe ungeenda mbezi mwisho upande wa daladala, pale ungekuta costa za morogoro, chukua namba ya dreva, na namba ya mpokeaji weka juu ya bahasha, mpe dreva 5000 , ile namba ya dreva mtumie mpokeaji, na dreva mpe namba ya anayepokea, fasta tu masaa matatu mengi mzigo unapokelewa kikubwa mpokeaji awe fasta asiwe mtu wa kujivutavuta,
Wazo zuri sana hili,Hata mie huwa natumia njia hii
 
Kutuma mzigo wenye dhamani ya 10,000 kwa gharama ya 5,000!!! Plus nauli ya kutoka huko kwenu mpaka Kariakoo na Kariakoo mpaka Ubungo. Yaani gharama ya kusafirisha earphone za hali ya chini hivyo zinafikia 70% ya bei ya kununua!!!!! Hizo earphone za hali ya chini hivyo zilikuwa na umuhimu gani kupelekwa mpaka Chalinze? Sio kusumbua watu tu.
 
Kutuma mzigo wenye dhamani ya 10,000 kwa gharama ya 5,000!!! Plus nauli ya kutoka huko kwenu mpaka Kariakoo na Kariakoo mpaka Ubungo. Yaani gharama ya kusafirisha earphone za hali ya chini hivyo zinafikia 70% ya bei ya kununua!!!!! Hizo earphone za hali ya chini hivyo zilikuwa na umuhimu gani kupelekwa mpaka Chalinze? Sio kusumbua watu tu.

Earphone unaelezwa amenunua 10000 kariakoo, usidhani ni zile za buku jero au bukubuku, hasa unavojua chalinze pale anaweza kupata earphone za aina hiyo? Hoja hapo hua ni gharama kampuni nyingine wanachaji kuanzia asilimia 10 ya mzigo yaani mzigo wa laki moja unachajiwa 10000 kulingana na uzito, hizo bahasha hua ni elfu tano tu kisela mzigo unafika, na labda yeye anauza kupitia mtandao na mteja yuko chalinze afanyeje asitume au? Lazima uelewe sio kila mtu aliko kuna bidhaa kama Dar au miji mikubwa mingine
 
Back
Top Bottom