Baadhi ya vituko vya wana CCM ya Magufuli vs CCM ya asilia

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho, Kila kitu kina mwisho wake, Lakini mwisho mkuu wa vitu vingi ni kufa au kusahaulika kabisa

Mimi ni mwana ccm lakini CCM yetu ni ile ile, Ni ile ile iyojaa utu na kuheshimiana. CCM ile ile ndio ccm a silia

Kwanini nimeuleta uzi huu hapa JF?

Mosi, Mwaka 2016 mpaka Mwanzoni mwa mwishoni mwa mwaka 2020, Bashiru Ally pamoja na Humprey Polepole walianzisha ccm mpya ndani ya ccm asilia yaani ndani ya ccm ile ile

CCM mpya iliendesha Propaganda na kuaminisha uma kuwa miradi yote ya Mwendokasi yaani BRT, Barabara zote za lami nchi hii, Shule zote za serikali mpaka zile tulizorithi toka kwa wakoloni kama Tabora boys, Pugu, Iyunga Technical zote zilijengwa na ccm mpya ya John Magufuli

CCM mpya iliaminisha uma kuwa uhuru wa nchi hii wa mwaka 1961, na taasisi zote kama TRA na Takukuru basi tulizipata kwa ushujaa wa John Pombe Magufuli

Madhara ya muda mfupi wa ccm mpya Leo yanawatafuna wenyewe kwenye uzinduzi na ukaguzi wa daraja jipya wami

CCM asilia nayo inajibu mapigo ya Madhara ya CCM mpya kuwa daraja la wami, Rais Samia ndio amelijenga na kuliplani kwa kulikamilisha ndani ya miezi 18 tu

Maswali ya kujiuliza

Je hizi barabara za Mwendokasi ambazo mwaka 2014 wakati wa kikwete zilifikia asilimia 70%, Lakini aliyezindua akasema nimejenga mimi mwenyewe kwa Fedha za ndani

Je hii barabara ya Mwenge kwenda Tegeta nyuki ya leni mbili ambayo ilianza wakati wa Kikwete, Lakini aliyezindua alisema Nimefanya Mimi

Daraja la Tanzanite pale Posta lilizinduliwa na mwana CCM asilia(Mama Samia) , Yeye alisema credit kwa Magufuli kwa uwazi kabisa na kwa kuheshimu mchango wake

CCM mpya ilifanya Propaganda kuonyesha viongozi wa zamani wa nchi hii si lolote wala chochote, Mbaya zaidi haya yalifanywa na vijana waliozaliwa baada ya uhuru

Heshima na Hekima ni muhimu kuliko siasa za maji taka, Siasa za maji taka za kujimwambafai, Kujiona upo juu ya sheria, kujiona wewe ni immortal, Kujiona wewe una akili kuliko wengine

Kuna mtu aliwahi sema usiite vitu ulivyovikuta duniani ni haramu kwani vilikuwepo kabla yako na hata ukipambana navyo bado utaondoka wewe kurudi ulikotoka na utaviacha vitu hivyo na uharamu wake kwani hukuviumba wewe
 
Ccm unayoipigia upatu hapa kumbuka kabla ya Magufuli lilikuwa genge la majizi, wala rushwa, majambazi, majangiri, nk, mpaka ikafika wakati mkawa mnaogopa hata kuvaa magwanda yenu ya kijani kwa kuogopa kuzomewa mitaani.

Inashangaza sasa umesahau kuwa mnaweza tena kutembea kifua mbele kwa kuwa mnatembelea kwenye nyota ya Hayati Magufuli.

Subiri kidogo, nakuhakikishia ccm yako na hao akina mzee ndovu wenu intruding kule kule kwa zamani very soon!
 
Kuna CCM moja tu nayo ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani
 
CCM mpya iliendesha Propaganda na kuaminisha uma kuwa miradi yote ya Mwendokasi yaani BRT, Barabara zote za lami nchi hii, Shule zote za serikali mpaka zile tulizorithi toka kwa wakoloni kama Tabora boys, Pugu, Iyunga Technical zote zilijengwa na ccm mpya ya John Magufuli
Na Kuna wajinga waliamini😅😅
 
Ccm unayoipigia upatu hapa kumbuka kabla ya Magufuli lilikuwa genge la majizi, wala rushwa, majambazi, majangiri, nk, mpaka ikafika...
Ccm ni kikundi cha Kigaidi, huyo Magufuli ndio shetani kuliko hata Lucifer mwenyewe, kama yeye alijenga Ccm mpya ipendwe au kukubalika ni kwa nini avuruge uchaguzi wa 2020?

Sasa yupo kuzimu Jehenamu atajibu uhalifu wote aliowafanyia Watanzania.
 
Ccm unayoipigia upatu hapa kumbuka kabla ya Magufuli lilikuwa genge la majizi, wala rushwa, majambazi, majangiri, nk, mpaka ikafika wakati mkawa mnaogopa hata kuvaa magwanda yenu ya kijani kwa kuogopa kuzomewa mitaani. Inashangaza sasa umesahau kuwa mnaweza tena kutembea kifua mbele kwa kuwa mnatembelea kwenye nyota ya Hayati Magufuli.
Subiri kidogo, nakuhakikishia ccm yako na hao akina mzee ndovu wenu intruding kule kule kwa zamani very soon!
Magufuli mwenyewe alikua mwizi
 
Hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho, Kila kitu kina mwisho wake, Lakini mwisho mkuu wa vitu vingi ni kufa au kusahaulika kabisa...
Wapambe wa mkuu aliyepita walifikia kiwango cha kuanzisha somo pekee la historia ili sifa zake za kipekee zizidi kuinuliwa na kufundishwa kwa wanafunzi katika mitaala rasmi yao.
 
Hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho, Kila kitu kina mwisho wake, Lakini mwisho mkuu wa vitu vingi ni kufa au kusahaulika kabisa....
I’m sorry. Mleta mada pamoja na maelezo mazuri sana uliyotoa, lazima niongeze kwamba yote ni kielelezo cha ujinga mkubwa, actually upumbavu ulioletwa na CCM katika nchi hii.

Kuwasifia hao maRais kwa ujenzi wa miradi ya serikali ni ujinga wa hali ya juu. Ni kwa vile Watanzania wamepumbazwa kiasi cha kutoweza kuchambua na kuhoji masuala ya msingi ya kitaifa. Rais anapongezwa personally kwa ujenzi wa daraja, flyover, barabara? Eti legacy? Wtf?

Angalau Nyerere hatukumsifu wala kumkosoa kwa vitu hivyo. Na alivijenga kweli. Viwanda vikubwa vilivyowahi kuwepo katika nchi hii na kuajiri malaki vilijengwa enzi zake. Aliweka alama kila sekta. Lakini hadi leo tunampima kwa ubora na ubovu wa sera na aina ya uongozi wake jinsi ulivyoathiri maisha ya wananchi. Sio barabara, reli, ndege, nk.

Kwanza hawa wameiba sana kupitia hiyo miradi. Kujilinda wamejaza chawa, wapiga propaganda, wapotoshaji, mashushushu, na watu wasiojulikana nje na ndani ya vyombo vya dola. Ujinga unafiki kukithiri nchini. Chama chenyewe kilishajifia siku nyingi. Kilichobakia ni mzimu unaoshikiliwa na dola iliyopania kuendelea kulitesa taifa.
 
Sema ukweli huu!....

Kati ya....

CCM-Waizi na CCM-Wazalendo!
CCM-Mtandao na CCM wananchi!
CCM-Asali na CCM-Wanyonge!

CCM iliyoiua CCM ni CCM-Mtandao....ambayo ndiyo inayoendelea kuwatesa watanzania mpaka sasa!

Wewe mleta hoja,ni mmoja wa wale walioko CCM kwa ajili ya matumbo yao.

Jiulize swali hili!

Kabla ya uchaguzi mkuu 2015 hiyo CCM ya wanamtandao ilikuwa na hali gani kisiasa nchini?

Ni nini kilipelekea hadi JPM kukabidhiwa kijiti bila ridhaa ya wanamtandao?

Hali ile ile ndiyo itakayojirudia tena safari hii.

Tofauti ni kwamba safari hii hakuna atakayekuwa wa kupokea kijiti ili kuiokoa CCM mtandao!

Endeleeni kuweka mahusiano na jeshi la Polish-Ccm!
 
Ccm unayoipigia upatu hapa kumbuka kabla ya Magufuli lilikuwa genge la majizi, wala rushwa, majambazi, majangiri, nk, mpaka ikafika wakati mkawa mnaogopa hata kuvaa magwanda yenu ya kijani kwa kuogopa kuzomewa mitaani. Inashangaza sasa umesahau kuwa mnaweza tena kutembea kifua mbele kwa kuwa mnatembelea kwenye nyota ya Hayati Magufuli.
Subiri kidogo, nakuhakikishia ccm yako na hao akina mzee ndovu wenu intruding kule kule kwa zamani very soon!

CCM ya Magufuli haikuwa bora, bali ilitegemea mabavu. Kilicho wafanya wasizomewe sio ubora bali ni kikosi cha kuteka watu a.k.a watu wasiojulikana ndio walizuia kuzomewa. Usitake kujifanya kuwa ubora ndio uliwaokoa na kuzomewa. Nakumbuka hata kwenye uchaguzi polisi ndio walikuwa wanaratibu maboxi ya kura kuingizwa vituoni na kura za CCM. Inshort CCM ya Magufuli ilikuwa ya kikatili na sio ubora.
 
Back
Top Bottom