Mkuu
Tindo
Hilo hapo ni jibu lako toka kwa
sheiza
[emoji116]
Bahati mbaya umezungumzia kundi moja tena kwa mlengo hasi japo kichwa cha habari umeweka makundi mawili.
Kama uluvyosema ccm ni ile ile lakini haiwezi kuwa ile ile wakati wote. Kina Lowasa, kina Nchimbi, kina Kingunge ni wana ccm asili lakini 2015 waliiacha wakaenda Chadema.
Kundi lako hilo ndio liliifilisi ccm na kila mtu kujibinafsishia mali za chama. Hata mama Zakia Meghji alikuwa na skendo ya kuuza printer ya kuchapishia magazeti ya Uhuru ambayo ni ya chama. Wengine walichukua hadi mashule.
Mwenyekiti JK na wenzie kina Kinana aliokuwa anakula nao asali walijitahidi ila chama kiliwafia mkononi. Huo ndio ukweli.
Ni hao unaowaita ccm ya Magu ndio wamerudisha chama kwenye mstari. Kwani nani asiyejua ukivaa nguo za ccm ulikuwa unazomewa njia nzima? Machinga gani alithubutu kuweka nguo za ccm auze? Hata majumbani wana ccm waliogopa kuning'iniza bendera za chama maana nyumba inaweza chomwa.
Ukizungumzia miradi ipo ambayo aliianza JK ila iligubikwa na ufisadi na pengine isingewezekana. Mfano terminal 3 mkandarasi alilipwa pesa yote kulingana na vitabu ila mradi haukufika hata nusu ukawa umesimama. Magu alitia pesa na akapiga presha na muda mchache ukaisha.
Hiyo mwendokasi kweli iliisha ila ilishindikana kuanza, unajua kwa nini? Nauli ilipangwa 2000/= kituo hadi kituo na magari yote ya abiria yalipigwa pini kuingia town. Maana yake upande mwendokasi kwa lazima. Watu wachache waliuchukua huu mradi kujinufaisha. Ni Magu alikuja akawapiga chini na nauli ikawa 600/= na wengine akawatupa ndani.
Lakini usisahau hata hilo daraja la mwl Nyerere sio la serikali, ni la NSSF ndio maana kuna wafanyakazi wa NSSF pale na unachajiwa pesa. Miradi ya Magufuli ni purely ya wananchi. Hakuna pointi ya kulipia.
Hata huduma zilizoasisiwa chini ya ccm ya Magu zilikuwa nafuu sana. Mfano nauli za ndege, meli, vivuko, uwekaji wa umeme hususani vijijini kabla haijapanda na bado alitaka bwawa la umeme la mwl Nyerere lije kushusha bei ya umeme. Hapa kila chumba kingekuwa na jiko la umeme, hadi maharage tungechemshia umeme. Huduma ya maji safi ilikuwa ya uhakika na rahisi, ilipanda na kusuasua baada ya Magu kufa.
Hapa kubali tu Magu atabaki kuwa kielelezo cha uhuru wa akili namaamuzi, kiongozi mwenye maono na uthubutu kuwahi kutokea kwa kipindi hiki ndani na nje ya ccm, ndani na nje ya Africa.
Nukuu ya Uhuru Kenyatta kwa Samia: Magufuli ameanzisha njia, usitoke nje ya hiyo njia.