Baadhi ya vituko vya wana CCM ya Magufuli vs CCM ya asilia

Baadhi ya vituko vya wana CCM ya Magufuli vs CCM ya asilia

Hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho, Kila kitu kina mwisho wake, Lakini mwisho mkuu wa vitu vingi ni kufa au kusahaulika kabisa

Mimi ni mwana ccm lakini CCM yetu ni ile ile, Ni ile ile iyojaa utu na kuheshimiana. CCM ile ile ndio ccm a silia

Kwanini nimeuleta uzi huu hapa JF?

Mosi, Mwaka 2016 mpaka Mwanzoni mwa mwishoni mwa mwaka 2020, Bashiru Ally pamoja na Humprey Polepole walianzisha ccm mpya ndani ya ccm asilia yaani ndani ya ccm ile ile

CCM mpya iliendesha Propaganda na kuaminisha uma kuwa miradi yote ya Mwendokasi yaani BRT, Barabara zote za lami nchi hii, Shule zote za serikali mpaka zile tulizorithi toka kwa wakoloni kama Tabora boys, Pugu, Iyunga Technical zote zilijengwa na ccm mpya ya John Magufuli

CCM mpya iliaminisha uma kuwa uhuru wa nchi hii wa mwaka 1961, na taasisi zote kama TRA na Takukuru basi tulizipata kwa ushujaa wa John Pombe Magufuli

Madhara ya muda mfupi wa ccm mpya Leo yanawatafuna wenyewe kwenye uzinduzi na ukaguzi wa daraja jipya wami

CCM asilia nayo inajibu mapigo ya Madhara ya CCM mpya kuwa daraja la wami, Rais Samia ndio amelijenga na kuliplani kwa kulikamilisha ndani ya miezi 18 tu

Maswali ya kujiuliza

Je hizi barabara za Mwendokasi ambazo mwaka 2014 wakati wa kikwete zilifikia asilimia 70%, Lakini aliyezindua akasema nimejenga mimi mwenyewe kwa Fedha za ndani

Je hii barabara ya Mwenge kwenda Tegeta nyuki ya leni mbili ambayo ilianza wakati wa Kikwete, Lakini aliyezindua alisema Nimefanya Mimi

Daraja la Tanzanite pale Posta lilizinduliwa na mwana CCM asilia(Mama Samia) , Yeye alisema credit kwa Magufuli kwa uwazi kabisa na kwa kuheshimu mchango wake

CCM mpya ilifanya Propaganda kuonyesha viongozi wa zamani wa nchi hii si lolote wala chochote, Mbaya zaidi haya yalifanywa na vijana waliozaliwa baada ya uhuru

Heshima na Hekima ni muhimu kuliko siasa za maji taka, Siasa za maji taka za kujimwambafai, Kujiona upo juu ya sheria, kujiona wewe ni immortal, Kujiona wewe una akili kuliko wengine

Kuna mtu aliwahi sema usiite vitu ulivyovikuta duniani ni haramu kwani vilikuwepo kabla yako na hata ukipambana navyo bado utaondoka wewe kurudi ulikotoka na utaviacha vitu hivyo na uharamu wake kwani hukuviumba wewe
Kusema Samia ndio kajenga daraja la wami ni uongo wa mchana kweupe.
 
Mkuu Tindo
Hilo hapo ni jibu lako toka kwa sheiza
[emoji116]
Bahati mbaya umezungumzia kundi moja tena kwa mlengo hasi japo kichwa cha habari umeweka makundi mawili.

Kama uluvyosema ccm ni ile ile lakini haiwezi kuwa ile ile wakati wote. Kina Lowasa, kina Nchimbi, kina Kingunge ni wana ccm asili lakini 2015 waliiacha wakaenda Chadema.

Kundi lako hilo ndio liliifilisi ccm na kila mtu kujibinafsishia mali za chama. Hata mama Zakia Meghji alikuwa na skendo ya kuuza printer ya kuchapishia magazeti ya Uhuru ambayo ni ya chama. Wengine walichukua hadi mashule.

Mwenyekiti JK na wenzie kina Kinana aliokuwa anakula nao asali walijitahidi ila chama kiliwafia mkononi. Huo ndio ukweli.

Ni hao unaowaita ccm ya Magu ndio wamerudisha chama kwenye mstari. Kwani nani asiyejua ukivaa nguo za ccm ulikuwa unazomewa njia nzima? Machinga gani alithubutu kuweka nguo za ccm auze? Hata majumbani wana ccm waliogopa kuning'iniza bendera za chama maana nyumba inaweza chomwa.

Ukizungumzia miradi ipo ambayo aliianza JK ila iligubikwa na ufisadi na pengine isingewezekana. Mfano terminal 3 mkandarasi alilipwa pesa yote kulingana na vitabu ila mradi haukufika hata nusu ukawa umesimama. Magu alitia pesa na akapiga presha na muda mchache ukaisha.

Hiyo mwendokasi kweli iliisha ila ilishindikana kuanza, unajua kwa nini? Nauli ilipangwa 2000/= kituo hadi kituo na magari yote ya abiria yalipigwa pini kuingia town. Maana yake upande mwendokasi kwa lazima. Watu wachache waliuchukua huu mradi kujinufaisha. Ni Magu alikuja akawapiga chini na nauli ikawa 600/= na wengine akawatupa ndani.

Lakini usisahau hata hilo daraja la mwl Nyerere sio la serikali, ni la NSSF ndio maana kuna wafanyakazi wa NSSF pale na unachajiwa pesa. Miradi ya Magufuli ni purely ya wananchi. Hakuna pointi ya kulipia.

Hata huduma zilizoasisiwa chini ya ccm ya Magu zilikuwa nafuu sana. Mfano nauli za ndege, meli, vivuko, uwekaji wa umeme hususani vijijini kabla haijapanda na bado alitaka bwawa la umeme la mwl Nyerere lije kushusha bei ya umeme. Hapa kila chumba kingekuwa na jiko la umeme, hadi maharage tungechemshia umeme. Huduma ya maji safi ilikuwa ya uhakika na rahisi, ilipanda na kusuasua baada ya Magu kufa.

Hapa kubali tu Magu atabaki kuwa kielelezo cha uhuru wa akili namaamuzi, kiongozi mwenye maono na uthubutu kuwahi kutokea kwa kipindi hiki ndani na nje ya ccm, ndani na nje ya Africa.

Nukuu ya Uhuru Kenyatta kwa Samia: Magufuli ameanzisha njia, usitoke nje ya hiyo njia.
Haya yote bila Uhuru wa watu, na kumrudisha Ben Saanane, Azory Gwanda na wengine ni takataka tu, totally rubbish.
 
Haya yote bila Uhuru wa watu, na kumrudisha Ben Saanane, Azory Gwanda na wengine ni takataka tu, totally rubbish.
Aliondolewa Rais John Kennedy wa Marekani tena mchana kweupe na Marekani ipo sembuse hao.
 
Umesema ukweli kabisa. Wakati wa Nyerere sifa ilikuwa ni ubora wa sera. Baada ya uchaguzi wa 2010 kwenda mbele CCM ilipoanza kuzidiwa ushindani wa kisiasa, ndio kukazuka kizazi cha kumsifia rais kuwa kafanya nini. Tabia hii ya kumtaja mtu/rais ilianza rasmi baada ya project ya kujivua gamba.

Ilipofika kwenye utawala wa Magufuli tabia hiyo ikakita mizizi. Yeye aliingia hata madarakani kwa kujiita CCM ya Magufuli! Hii tabia sasa hivi ni muendelezo, utasikia pesa za mama, mara mama tunaomba utusaidie mradi huu nk. Cha ajabu hata viongozi wanaamini hizo fedha ni zao, na wanaweza kuzitoa watakavyo na sio sheria itakavyo. Magufuli yeye alikuwa anasema kabisa hapa mmechagua mpinzani siwezi kuleta maendeleo, na akawa anashangiliwa!
Sawa kabisa. Nyerere alitukera kwa udikteta na mlengo wake wa ukomunisti mwenyewe akiuvisha joho la “ujamaa” ili kuwahadaa marafiki zake social democrats wa Ulaya Magharibi. Alikuwa “haambiliki”.

LAKINI Nyerere hakuwa mwizi hata kidogo. Na naamini kabisa kuwa alipania kuiendeleza Tanzania kweli kweli (alikuwa na nia bona fide genuine - by P Mayala). Tatizo lake kubwa hakutaka mawazo mbadala na hakuwa tayari kugawana “utukufu” na mtu yoyote; alitaka kutambulika (sifa) peke yake. Alitaka kuwa kama Mao. Alipokwama kabisa aliachia ngazi kuliko serikali yake kuingia mkataba na IMF.

Kero yangu kubwa sana na Nyerere ni kutuachia katiba mbovu sana na mzimu (Ghost) wa CCM vinavyompa madaraka ya kimungu mtu mmoja kuhujumu taifa zima. I don’t understand why. Naamini alikuwa na akili kubwa kujua kuwa ni hatari sana kuwaamini binadamu na madaraka ya aina hiyo. Na kwa uroho (greed) uliotamalaki nchini, hivi ndivyo vitu vitakavyoendelea kudumaza na kubomoa taifa hili step by step hadi mwisho.
 
Chama kimezidi kukua.
Sasa hivi kuna CCM asilia hii iliasisiwa na Nyerere na sasa inaendeshwa na wastaafu.
Kuna CCM mpya - hii iliasisiwa na mwenda zake et al ila kwa sasa inaendeshwa na Sukuma gang na walinda legacy
CCM Kaole - hii inaendeshwa na walamba asali (wanaolinda teuzi zao) na wasaka teuzi... Huku ni usanii mtupu...kama kaole art group.
Hapa ndipo utapata wale wanaosema tuna ziada ya umeme huku mgao wa umeme ukiendelea.
Sasa wewe chagua uwe CCM ipi.
 
Nardia tena, bora kuberi kuliko ugolo. Vijana mnapotea kwa kuvuta ugolo.

Samia ruhusu kuberi vijana wajitambue
 
Back
Top Bottom