Baadhi ya viongozi wa Dini ni kama wamechanganyikiwa na hawajui waguse wapi, hii ni kwasababu ya kujiingiza kwenye maslahi

Baadhi ya viongozi wa Dini ni kama wamechanganyikiwa na hawajui waguse wapi, hii ni kwasababu ya kujiingiza kwenye maslahi

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,541
Reaction score
916
Baadhi ya viongozi wa dini nikama wamechanganyikiwa na hawajui waguse wapi, hii ni kwasababu ya kujiingiza kwenye maslahi badala ya kumtumikia Muumba madhara ya kuchanganya maji na mafuta kwenye chombo kimoja na mwisho kuishia kutengana

Kwa taarifa yao ni kuwa
-Muumba hawaelewi
-Serikali haiwaelewi
-Wananchi hawaelewi

Unafiki kwa Muumba ndio unawatafuna

Unafiki kwa Serikali ndio unawamaliza kwasababu hawakuisaidia kabla ya kupatwa na matatizo ya kugombanishwa na Wananchi wake

Unafiki kwa Wananchi unawamaliza kwasababu hawakuwasaidia kabla ya kupatwa na matatizo ya kugombana na Serikali yao

Wamejitokeza baada ya matatizo kuikumba Serikali na Wananchi wake

Sababu ya kuwa wanafiki wanahofia wakizungumza habari za Muumba zitawatafuna kwa kuwasuta na kuwalaani na hasa maandiko yake

Sababu ya kuwa wanafiki ni kwasababu wanahofia waki ikera Serikali itawafutia vibali vya kula

Sababu ya kuwa Wanafiki ni kwasababu wanahofia wakikera Wananchi watakosa sadaka wanazotumia kuwekeza na kujenga

Kama kweli ni viongozi wa Dini, walipaswa waisaidie Serikali mapema ili isiingie kwenye matatizo na Wananchi wake

Lakini pia wangewasaidia Wananchi mapema ili wasikosane na Serikali yao

Baadhi ya viongozi wa Dini wameacha kufanya kazi waliyotumwa na kujiingiza kwenye maslahi pamoja na Siasa za vuguvugu

Wanamiliki miradi mingi ikiwemo Ardhi, Taasisi, Shule, Bank, miradi ambayo imetokana na nguvu za Serikali na Wananchi wake

Imenunuliwa, kujengwa na kuendeshwa Sadaka

Wanakuja na siasa za vuguvugu na habari za Shetani

Wanachi na Serikali wanataka kupewa support kwenye nyakati za matatizo na hasa fedha kwaajili ya kusaidia Wahanga na sio umbea wa Shetani

Nikama hawana chakula cha kulisha Taifa nje na habari za Shetani, hadithi za BC zitasaidia vipi Taifa

Umbea wa Shetani utasaidia vipi Taifa, namna ya kusaidia Taifa ni kuchangia mifuko ya maafa, watoe fungu la fedha wanazoficha bank wasaidie Wahanga

Serikali na baadhi ya Wananchi ndiyo wanahangaika kumaliza majanga ya kila aina lakini wao hawajigusi huku wakijiita Viongozi wa Dini

Na hii ndiyo sababu

Muumba hawaelewi
Serikali haiwaelewi
Wananchi hawaelewi
 
Back
Top Bottom