Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Mambo Tanzanians!

Sasa kijana changamkia fursa chap ya uuzaji vyakula katika mahoteli makubwa makubwa na mama/ baba lishe ukipenda lakini.

1. Mboga mboga za majani

2. Kuku wa kisasa kilo kuanzia 1.6kg

3. Mchele

4. Unga sembe uwe laini

5. Unga ngano uwe laini

6. Mafuta ya kupikia ( alzeti, mawese au kawaida)

7. Matunda

Gharama

a) Usajili wa shughuli yako Tsh.20,000 brela hao.

b) Tafuta vitabu vya stakabazi uviweke nembo ya jina la biashara yako, Tsh.10,000

c) Daftari la kumbukumbu kwa wateja, Tsh. 5,000

d) Nauli ya kutafuta oda kwa wiki Tsh.15,000

e) Mtaji wa biashara kuanzia Tsh.50,000 na kuendelea

Ufupisho

* Mtaji = Tsh.50,000 na kuendelea itategemea unataka kusupply mzigo gani.

* Kiendesha mtaji = Tsh.50,000

Maelekezo

1. Sajili kikampuni chako cha "Sole Proprietor" kutoka BRELA kiroho safi uwe rasmi kibiashara.

2. Andaa mikataba yako safi, itengeneze mwenyewe hata ukishindwa gugo mifano ya mikataba ya kazi au biashara utajiongeza sasa na wewe cha kuandika. Kaa nayo uitunze muda ukifika itatumika.

3. Hakikisha unakuwa nadhifu muda wote pia jifunze lugha ya kibiashara.

4. Usiogope jengo lolote rafiki; jiamini vya kutosha bwana. Mfano ukienda hotelini ulizia mtu wa manunuzi wa hoteli au anayehusika na upokeaji oda ya bidhaa. Niamini utafurahia biashara yako.

5. Uwe na uwezo wa kiakili hapa namaanisha uwe mjanja mwepesi kusoma akili ya unayeongea nae. Ukikuta anajiweka anajua ung'eng'e na wewe tiririka vya kutosha ata ukiongea broken biashara ndivyo ilovyo mzee baba.

6. Ukikwama sehemu njoo hapa jukwaani tupeane maujuzi.

Angalizo: Usitoe hela hata iweje.

Karibu!
 
Mbona nikijumlisha napata 100,000/= then unakuja unasema mtaji 50,000/= hii imekaaje au ile 50,000/= nyingine sijui nauri, kusajiri nk sio sehemu ya mtaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Capital = Tsh.50,000

Working Capital = Tsh.50,000

Jumla ni Tsh.100,000/=

NB
Working capital inahusisha mtaji wezeshi wa kibiashara mfano matumizi ya aina yoyote niliyoyataja.

Mtaji/ Capital ni fedha itakayotumika kwa bidhaa au huduma tu. Haihusishi matumizi mengine

Hiyo ndio maana yangu.
 
1, 2 na 12 zinanihusu kabisa mkuu, yaani ujuzi nilionao naweza pata biashara zaidi ya 10, hobby yangu inanipa zaidi ya biashara 5, na kuhusu kuiga idea hapo nishaona idea kama 2 hivi kutoka majuu na zote ni fire.
Tatizo ni kuwa hayo yote hapo juu yanabaki ndoto za maisha yangu kwani sina hata shilingi kumi kuyaanzisha.
Pia nchi yetu haina mpango mzuri wa uwezeshaji, hasa kuwekeza katika maendeleo ya teknolojia ni zero error, siku hizi tunaona hata elimu imewekwa kisiasa, too sad. trust me, nipo blessed kinyama coz chochote nachotaka fanya nikiamua nafanya na unaweza usijue kama nafanya for first time. aisee inauma sana hii nchi ina wataalamu kibao sema mipango ndo mibovu.
 
Nilicho gundua Casha ni Aibu na wala sio ukosefu wa mawazo ya biashara.

Mi naamini watu wengi wana mawazo mazuri ya kuanzisha biashara bila hata mtaji wa shilingi moja ila shida kubwa ni Aibu kumfikiria mtu atanionaje

Ebu soma historia hii

kuna kijana mmoja alitoka katika familia duni sana kimaisha alikuwa anaishi na bibi yake alikuwa hana mama wala baba wazazi wake walitangulia mbele ya haki akiwa mdogo kwa hiyo alilelewa na bibi yake kwa tabu na masha alisoma mpaka kidato cha nne.

alipomaliza shule alihangaika asijue la kufanya mpaka siku moja alipokaa chini na kufikiri kwa undani zaidi nitafanya nini katika maisha yangu magumu kiasi hiki, wakati akitafakari akatokea mama moja akamuomba akamtupie taka kwani taka zake zilikua zimejaa kwenye viroba alivyohifadhia taka.

Kijana alikua hana kiburi bila ya kujivunga akanyanyuka na kwenda kutupa taka aliporudi yule mama akampa 1000 akatokea na mama mwingine akamwambia na mimi naomba ukanimwagie na zakwangu akaenda na yule mama akamlipa pia 1000 kwa jioni ile akawa tayari ana 2000 iliyo muwezesha kupata mlo wa jioni.

Siku ya pili aliamka asubuhi na kuanza kupita kila nyumba na kuanza kuulizia kama wanahitaji huduma ya kumwagiwa taka cha kushangaza kwa siku nzima alifanikiwa kupata sh.20000 alifurahi sana ingawa majirani walimuongelea ,walimdharau, na wengine walimbadilisha jina kabisa na kumuita mwaga taka hakujali alichojali ni nini anapata na maisha yake anayaendesha vipi,hakujali alijipa moyo na kusema hata wakiniita mwaga taka hawanisaidii shida zangu nazijua mwenyewe.

Aliendelea na kazi yake ya kupita nyumba hadi nyumba kukusanya taka mpaka akafanikiwa kutengeneza mkoko teni wa kuzolea taka hakuishia hapo akatengeneza mikokoteni mingine zaidi na kuanza kuajiri vijana wenzie ili wamsaidie akaendelea mpaka akafikia kiwango cha kufungua ofisi mtaani kwao ,akanunua magari ya kuzolea taka sasa ni tajiri mkubwa watu hawamwiti tena mzoa taka bali ni bosi mzee mkubwa mkuu ndio majina yake kwa sasa
ana magari ya kisasa kabisa ya kuzolea taka na kuzisaga na kuwa mbolea anauza mbolea na kukusanya taka vyote vinamuingizia hela.

Nachojaribu kusema ni kwamba watu wengi huzuia malengo yao kwa Aibu ya kumuogopa fulani, utamkuta msichana kamaliza shule ana ujuzi mzuri wa kutengeneza chapati au maandazi na mtaani kwao hakuna vitu hivyo anaogopa kutengeneza kisa aibu.

Kwahiyo biashara sio mtaji ni uwezo wa kufikiri tu na kuweka Aibu pembeni.
Vizuri
 
Shukran
Hello Tanzanians!

Kwa vijana mliosoma IT & Computer science mnaweza mkatengeza Mobile Software Application (Mobile App) nzuri ambayo itakayoweza kutoa huduma na wewe mtengenezaji ukawa Controller wa hiyo huduma.

Mfano, ukaamua kutengeneza Mobile App ya huduma ya Car Parking Spaces kwa mkoa wa Dar es Salaam yote. Mtu ambaye aidha ni mwenyeji au mgeni katika jiji hilo ataweza kuweka oda ya parking ya gari au chombo chake cha usafiri ili asikose mahali pakuhifadhi usafiri wake na hii itasaidia kuongeza usalama kuwa mkubwa na kutengeneza ajira za kutosha.

Ushauri wa tozo: Kula 10% ya mteja (customer) na 10% ya mwenye huduma (Space owner) au kinyume chake.

Mifano ya huduma nyingine;

1. Uuzaji wa vyakula vya bei nafuu (migahawa badhifu yenye bei isioumiza).

2. Huduma ya choo na bafu

3. Kumbi za harusi na sherehe

4. Kumbi za starehe na bar

5. Nyumba za kulala wageni classic ila bei isioumiza.

6. Maduka yenye kutoa huduma ya bidhaa mbalimbali masaa 24 siku 7 za wiki (24/7).

7. Vibanda vya huduma ya chipsi safi, kongoro, supu mkia wa mbuzi, makange nk

8. Sehemu zenye watu watoa huduma za ucheshi nk

9. Car wash

10. Vehicles parking

11. Sehemu ya kupumzika yaani open space free charge area nk

12. Utajiongeza na wewe

Haya mawazo hayahitaji mtaji zaidi ya Tsh. 50,000/=. Kijana msomi kazi ni kwako.

Kuhusu soko ni mkoa uliopo na wilaya zake hii inaitwa kutembelea nyota.

Karibu "wauza mawazo ya biashara"

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Network marketing
Habarini wana jukwaa hili. Naimani mko poa sana wa afya.

Niingie moja kwa moja kwenye mada, nina ndugu yangu anauza stationary na wadau wengi wanaoumzunguka eneo lake ni waendesha kirikuu (vigari vidogo vya mizigo).

Nimewaza sana, je ni biashara gani naweza invest ukiachana na vinywaji, chakula, karanga na chai?

Mawazo yako naomba Biashara ya mtaji mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilicho gundua Casha ni Aibu na wala sio ukosefu wa mawazo ya biashara.

Mi naamini watu wengi wana mawazo mazuri ya kuanzisha biashara bila hata mtaji wa shilingi moja ila shida kubwa ni Aibu kumfikiria mtu atanionaje

Ebu soma historia hii

kuna kijana mmoja alitoka katika familia duni sana kimaisha alikuwa anaishi na bibi yake alikuwa hana mama wala baba wazazi wake walitangulia mbele ya haki akiwa mdogo kwa hiyo alilelewa na bibi yake kwa tabu na masha alisoma mpaka kidato cha nne.

alipomaliza shule alihangaika asijue la kufanya mpaka siku moja alipokaa chini na kufikiri kwa undani zaidi nitafanya nini katika maisha yangu magumu kiasi hiki, wakati akitafakari akatokea mama moja akamuomba akamtupie taka kwani taka zake zilikua zimejaa kwenye viroba alivyohifadhia taka.

Kijana alikua hana kiburi bila ya kujivunga akanyanyuka na kwenda kutupa taka aliporudi yule mama akampa 1000 akatokea na mama mwingine akamwambia na mimi naomba ukanimwagie na zakwangu akaenda na yule mama akamlipa pia 1000 kwa jioni ile akawa tayari ana 2000 iliyo muwezesha kupata mlo wa jioni.

Siku ya pili aliamka asubuhi na kuanza kupita kila nyumba na kuanza kuulizia kama wanahitaji huduma ya kumwagiwa taka cha kushangaza kwa siku nzima alifanikiwa kupata sh.20000 alifurahi sana ingawa majirani walimuongelea ,walimdharau, na wengine walimbadilisha jina kabisa na kumuita mwaga taka hakujali alichojali ni nini anapata na maisha yake anayaendesha vipi,hakujali alijipa moyo na kusema hata wakiniita mwaga taka hawanisaidii shida zangu nazijua mwenyewe.

Aliendelea na kazi yake ya kupita nyumba hadi nyumba kukusanya taka mpaka akafanikiwa kutengeneza mkoko teni wa kuzolea taka hakuishia hapo akatengeneza mikokoteni mingine zaidi na kuanza kuajiri vijana wenzie ili wamsaidie akaendelea mpaka akafikia kiwango cha kufungua ofisi mtaani kwao ,akanunua magari ya kuzolea taka sasa ni tajiri mkubwa watu hawamwiti tena mzoa taka bali ni bosi mzee mkubwa mkuu ndio majina yake kwa sasa
ana magari ya kisasa kabisa ya kuzolea taka na kuzisaga na kuwa mbolea anauza mbolea na kukusanya taka vyote vinamuingizia hela.

Nachojaribu kusema ni kwamba watu wengi huzuia malengo yao kwa Aibu ya kumuogopa fulani, utamkuta msichana kamaliza shule ana ujuzi mzuri wa kutengeneza chapati au maandazi na mtaani kwao hakuna vitu hivyo anaogopa kutengeneza kisa aibu.

Kwahiyo biashara sio mtaji ni uwezo wa kufikiri tu na kuweka Aibu pembeni.
Yuko nchi gani huyu jamaa?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo Tanzanians!

Sasa kijana changamkia fursa chap ya uuzaji vyakula katika mahoteli makubwa makubwa na mama/ baba lishe ukipenda lakini.

1. Mboga mboga za majani

2. Kuku wa kisasa kilo kuanzia 1.6kg

3. Mchele

4. Unga sembe uwe laini

5. Unga ngano uwe laini

6. Mafuta ya kupikia ( alzeti, mawese au kawaida)

7. Matunda

Gharama

a) Usajili wa shughuli yako Tsh.20,000 brela hao.

b) Tafuta vitabu vya stakabazi uviweke nembo ya jina la biashara yako, Tsh.10,000

c) Daftari la kumbukumbu kwa wateja, Tsh. 5,000

d) Nauli ya kutafuta oda kwa wiki Tsh.15,000

e) Mtaji wa biashara kuanzia Tsh.50,000 na kuendelea

Ufupisho

* Mtaji = Tsh.50,000 na kuendelea itategemea unataka kusupply mzigo gani.

* Kiendesha mtaji = Tsh.50,000

Maelekezo

1. Sajili kikampuni chako cha "Sole Proprietor" kutoka BRELA kiroho safi uwe rasmi kibiashara.

2. Andaa mikataba yako safi, itengeneze mwenyewe hata ukishindwa gugo mifano ya mikataba ya kazi au biashara utajiongeza sasa na wewe cha kuandika. Kaa nayo uitunze muda ukifika itatumika.

3. Hakikisha unakuwa nadhifu muda wote pia jifunze lugha ya kibiashara.

4. Usiogope jengo lolote rafiki; jiamini vya kutosha bwana. Mfano ukienda hotelini ulizia mtu wa manunuzi wa hoteli au anayehusika na upokeaji oda ya bidhaa. Niamini utafurahia biashara yako.

5. Uwe na uwezo wa kiakili hapa namaanisha uwe mjanja mwepesi kusoma akili ya unayeongea nae. Ukikuta anajiweka anajua ung'eng'e na wewe tiririka vya kutosha ata ukiongea broken biashara ndivyo ilovyo mzee baba.

6. Ukikwama sehemu njoo hapa jukwaani tupeane maujuzi.

Angalizo: Usitoe hela hata iweje.

Karibu!
Wazo lako nimelipenda, naanza kulifanyia kazi sasa hivi, vipi gharama za kusajiri sole proprietorship ni shilingi ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom